Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kama unajinasibu unanusa ufisadi, muulize Mbowe michango ya Wabunge iko wapi?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Ndugu Tundu Lissu mgombea wa CHADEMA unapokuwa jukwaani unaongea kwa jazba na kuonyesha kuwa wewe hutaki ufisadi na matumizi mabaya. Tena unaongea kwa kukakamaa kama unataka kumkaba mtu aliyekwapua mali ya umma.

Tundu Lissu, Wabunge wa chama chako walichangishwa pesa na pesa hizi zilikuwa kwa ajili ya uchaguzi. Lakini ilikuja kubainika kuwa pesa hizo zimekwapuliwa na wajanja kihuni.

Kama unajinasibu kusema unanusa ufisadi kwenye miradi inayotekelezwa na serikali ya CCM basi jikakamue umuulize Mbowe ziko wapi hizo bil 8.8? Hizi pesa zingekusaidia wewe na chama chako kunadi sera zenu kwa ufanisi.

Maana unatuchosha kila kukicha mara ndege za ATCL ni ufisadi, mara uwanja wa ndege Chato ni ufisadi mara Dotto James anajichotea pesa hazina. Basi kama wewe ni mpinga ufisadi kweli kweki anza na hizi ambazo zipo wazi zilikwapuliwa na chama chako ili utuhakikishie kweli wewe unapambana na ufisadi.
 
Ndugu Tundu Lissu mgombea wa Chadema unapokuwa jukwaani unaongea kwa jazba na kuonyesha kuwa wewe hutaki ufisadi na matumizi mabaya. Tena unaongea kwa kukakamaa kama unataka kumkaba mtu aliyekwapua mali ya umma....

Ndugu yangu wabunge wenyewe wangapi?

Maana unaongea utadhan chadema wana wabunge Mia mbili

Hao wabunge wanajua pesa zao zinakwenda wapi so ww tulia tu Coz wanatoa ela kwa matakwa yao
 
Ndugu yangu wabunge wenyewe wangapi?

Maana unaongea utadhan chadema wana wabunge Mia mbili

Hao wabunge wanajua pesa zao zinakwenda wapi so ww tulia tu Coz wanatoa ela kwa matakwa yao
Wabunge zaidi ya sabini walikwapuliwa pesa zao. Na pesa zilikuwa kwa ajili ya uchaguzi
 
Matumizi ya fedha Zilizo katwa Kwa wabunge ni Kwa mujibu wa Katiba ya CDM na Nadhani hawapaswi kuingiliwa Katika hili, Kama wabunge wenyewe Hawa lalamiki zaidi ya wale tu Walio fika bei.

Kwahiyo, Wala Hakuna haja ya kujua fedha halali walizo changia kuimarisha chama ni tatizo Kwako.. Basi unashida ya uelewa wa mambo ya siasa, Mtoa Post acha ushabiki soma Katiba...!! Ya CHADEMA
 
Mwanajeshi wa TAKUKURU amemhoji Mbowe kuhusu michango ya CHADEMA itakuwa Lissu? Mwanajeshi atupe kwanza mrejesho wa mahojiano na Mbowe kuhusu michango ya CHADEMA. Hata mwanachama wenu Lijualikali alihojiwa lakini kimya..
 
Ndugu Tundu Lissu mgombea wa Chadema unapokuwa jukwaani unaongea kwa jazba na kuonyesha kuwa wewe hutaki ufisadi na matumizi mabaya. Tena unaongea kwa kukakamaa kama unataka kumkaba mtu aliyekwapua mali ya umma...
Mwenyekiti wa CCM katamba peke yake miaka 5 akiwananga wenziwe. zamu yake imefika sasa!

achana na Mbowe!
 
Mwanjeshi wa TAKUKURU amemhoji Mbowe kuhusu michango ya CHADEMA itakuwa Lissu? Mwanajeshi atupe kwanza mrejesho wa mahojiano na Mbowe kuhusu michango ya CHADEMA. Hata mwanachama wenu Lijualikali alihojiwa lakini kimya..
Lissu ndio akazie msumari Mbowe apelekwe mahakani maana Lissu hapendi ufisadi. Tena kesho aliongelee hili jukwaani.
 
Back
Top Bottom