Tundu Lissu: Kama risasi 16 za 'watu wasiojulikana' waliotumwa kuniua hazikuninyamazisha, kuninyang'anya mshahara hakutaweza kuninyamazisha

w
Hesabu ni Rahisi Sana.
Na-Assume
Watanzania Wanaomsupport Lissu tuko= 5000000(5 million).

Kila Mmoja Atadeposit 2,000/= kila Mwezi karibia na Tarehe 15.

Total itakuwa 10,000,000,000(10 Billion).

Hii ni zaidi ya Mshahara,posho,pension na Marupurupu ya Mbunge Kwa Miaka 5.

Watanzania Tukiamua Tunaweza.

TUMCHANGIE TUNDU LISSU SASA.

TUNDU LISSU RAIS 2020.

"Mopao Mokonzi"
wewe ni mpuuzi...
 
Hesabu ni Rahisi Sana.
Na-Assume
Watanzania Wanaomsupport Lissu tuko= 5000000(5 million).

Kila Mmoja Atadeposit 2,000/= kila Mwezi karibia na Tarehe 15.

Total itakuwa 10,000,000,000(10 Billion).

Hii ni zaidi ya Mshahara,posho,pension na Marupurupu ya Mbunge Kwa Miaka 5.

Watanzania Tukiamua Tunaweza.

TUMCHANGIE TUNDU LISSU SASA.

TUNDU LISSU RAIS 2020.


"Mopao Mokonzi"
Hiyo hela utaitolea wapi? na nani atakae ratibu zoezi? ana-moyo? yuppo tayari kwa yatakayofuata? Kazi kwelikweli
 
na Magufuli wako ombaomba, yeye ni Nani ashindwe kuomba? Wapumbavu mliopungukiwa akili, hekima na huruma kwa wenzanu. Sasa wewe utapata faida gani Lissu akinyimwa mshahara wake?
Ndo hapo sasa!!! Watu hawana huruma ya mungu kabisa!!!
 
Kwenye interview marekani,uingereza na ujerumani ndio kwenye matibabu?

Njaa mbaya sana na haina baunsa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani anaugua kipindupindu useme yuko kwenye eneo maalum haruhusiwi kutoka? Ni wagonjwa wangapi wanaendelea na matibabu hospitalini huku wakiendelea na kazi kisha kwenda hospitali tena? Mimi mzazi wangu anaugua kisukari, lakini huwa anarudi kijijini kuendelea na shughuli zake, na huwa anarudi hapa Dar hospital kuonana na daktari kwa siku alizoandikiwa. Usilete tafsiri za wanasiasa uchwara kwenye hali za kawaida za matibabu. Kwa majeruhi yake tungemuona anabeba zege hapo sawa, lakini interview? akili za kuambiwa boss.

Tunaona watu wengi waliopata ajali hasa za viungo wakitoka na kurejea hospitali kama muendelezo wa matibabu yao. Au ww ukivunjika mkono na kuwekewa POP hutatoka hospitali na kurejea kufungwa jipya kulingana na tatizo lako mpaka siku umepona kabisa?
 
Kwani hawa warasimu wote uliowataja si ndio kazi yao mpaka waambiwe kama ni tukio la uhalifu, let them get out of their fuckin offices as part of their routine responsibilities wengine wawe whistle blower.
Mkuu chukua hatua,kuna ofisi ya kijiji/mtaa,ofisi ya kata/tarafa/ kuna diwani,mbunge,Mkuu wa wilaya ,Mkurugenzi wa wilaya,Afisa elimu na hao waote ni viongozi.Ungeamsha hio bongo lala yako ofiki uwaone uwaeleze na wakueleze wanachofanya kutatua hilo tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
# HON_TUNDU_LISSU #
Hello Friends of Tundu Lissu,
Salaam,
Naomba nianze na afya yangu. Kwa ujumla naendelea vizuri. Operesheni sasa zimeisha; zimeishia kwenye namba 24, maana hii ya mwisho ilikuwa ni operesheni mbili kwa mpigo. Walitoa kipande cha mfupa upande wa kushoto wa kiuno na kukipigia kiraka kwenye goti la kulia kwa juu.
Vidonda vyote viwili vimepona, angalau kwa juu. Sasa ni mazoezi ya kukunja goti lenyewe na kutembea. Natakiwa kuonana na madaktari wangu kila baada ya wiki sita kwa ajili ya x-ray na CT scan. Next appointment ni tarehe 2 Aprili na inayofuata ni tarehe 14 May.
Kwa vyovyote vile, safari iliyobaki sio ndefu sana. Ndani ya mwaka huu nitarudi nyumbani. Kwa pamoja, tuanze kujielekeza kwenye hilo. Tutashauriana kwa pamoja kuhusu tarehe na utaratibu mzima wa kurudi nyumbani.
Haya ya Ndugai na watu wake, na walio nyuma yao, tukabiliane nayo. Tutayaweza. Nguvu ya nuru, upendo na haki siku zote ni kubwa kuliko nguvu ya giza, chuki na dhuluma.
Nawashukuruni sana na Mungu wetu awabariki sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni stori tu na itapita Kama nyingine.SERIKALI YA WATU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAITARUDISHWA NYUMA KAMWE MPAKA WAKATI USIO NA KIPIMO

Hakuna kilichoisha. Watu bado wana kumbukumbu ya yeye kupigwa risasi. Watanzania waishio ndani na nje ya nchi pamoja na nchi wafazili hawatasahau mambo haya. Hata kama hayaongelewi haina maana kuwa yamekwisha.
 
Wema Mungu huko pamoja na wewe, watanzania wapenda haki tuko tayari kukuchangia, hawa mashetani pamoja na hila zao mbaya kwako, zitashindwa. Na wakati unakuja, watalia na kusaga meno.
DA mnavyotiana moyo kama mfa maji vile anatapatapa najua ataokoka katikati ya kina kirefu poleni sana
 
Yule mbunge wenu mkono yeye hajahudhuria miaka 2 na bado analipwa stahiki zake,ccm lissu anawauma sana nguvu mnayotumia mgefanya kununua korosho,mbaazi yote
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Wote tunajua karibia kazi zote za wabunge zinakwenda sambamba na malipo ya allowance ( posho), ikiwemo kuhudhuria bungeni pamoja na vikao vya kamati.

Pale jimboni mbunge ana ofisi na kuna katibu ambaye humsaidia mbunge katika kutekeleza majukumu yake hivyo hata kama mbunge hayupo ofisi yake ipo na kazi zinaendelea kwa sababu tunaishi katika dunia ya teknolojia.

Juzikati hapa mbunge wa Tarime mjini alikuwa mahabusu kule Segerea jijini Dsm karibia km 1000 kutoka jimboni kwake lakini ofisi yake iliendelea kutoa Huduma ikiwemo kununua mabati na vifaa vingine kwa shule mbalimbali.

Binafsi sijawahi kuwasikia wapiga kura wa Singida mashariki wakilalamika kukosa Huduma za ofisi ya mbunge, ndio kusema kazi zinafanyika.

Point yangu ni kuwa Tundu Antipas Lisu kunyimwa posho mbalimbali ni sawa kabisa kwa utaratibu wa jinsi ya kulipwa posho hizo umeanishwa.
Ila kwenye kuzuia mshahara wake napata taabu kidogo na ndio najiuliza kwani mbunge anatakiwa afanye kazi zipi ndipo alipwe mshahara....... Kazi ambazo kwa sasa hazifanyiki pale Singida mashariki kwa sababu Lisu yuko katika sayari nyingine?

Ikumbukwe kuwa bunge letu ndio kioo na kitovu cha kuonyesha namna haki inavyopaswa kutendeka ili sisi wengine tujifunze kupitia hapo.... Na lisituachie shaka hata kidogo kwa kila uamuzi linaochukua.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom