Tundu Lissu: Je, mkataba wa uwanja wa ndege Chato upo wapi? Mkataba wa Madini upo wapi? Adai haijawai kupelekwa bungeni

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Members, Mahojiano aliyoyafanya Mwandishi Jenerali Ulimwengu kupitia Jeneralionline pamoja na Tundu Lissu kuna mambo ya msingi Tundu Lissu amehoji.

Mosi: Je, mkataba wa kujenga uwanja wa ndege Chato lini ulipelekwa bungeni? Ni Mtanzania gani anafahamu kilichoandikwa ndani ya mkataba huo, Adai serikali inaleta maneno matamu tu kama zamani.

Pili, Mkataba wa stiglers gorge lini ulipelekwa bungeni ili kuhakiki kinachoandikwa na kusemwa ni kweli, adai haya mambo ya kuficha mkataba hakuna mwenye uchungu na rasilimali zetu, adai kwanini iwe siri.

Tatu, adai kwenye madini ni maneno tu yanazungumzwa, mkataba wa madini kati ya Barrick na Tanzania hujawahi peleka bungeni kujadiliwa, adai wanaongea tu majukwaani kupamba the mambo. Tundu Lissu anadai hakuna anayepigania madini nchi hii kwani mikataba imekuwa ikifichwa awamu zote mpaka sasa.

Tundu Lissu anadai yeye amekuwa akiomba mikataba iwe wazi tangu enzi za Mkapa mpaka sasa hii mikataba mipya inafichwa.

Je, kuna anayefahamu ukweli wa mambo haya, Mkataba wa uwanja wa ndege Chato nani anafahamu?

Je, na huu mkataba wa Barrick na Tanzania nani aliwahi kuuona, nini yameandikwa ndani ya mkataba?

Je, na ujenzi wa Stiglers Gorge nini kimeandikwa ndani ya mkataba na lini bunge lilijadili?
 
Huyo alisema tutashitakiwa MIGA tunamsubiri kwa hamu wamptishe awe mgombea wa CHADEMA hatapata hata Diwani mmoja
Mkuu kama una mkataba weka hapa, Hoja hujibiwa kwa hoja

Ukitukana ina maana wewe uwezo wako wa kujibu hoja na kufikiri ni mdogo

Weka mkataba hapa au Jibu hoja

Povu la nini kiongozi Jibu hoja mikataba ipo? Ilipelekwa bungeni?
 
Hakuna nchi yoyote dunuani ambayo huweka mikataba wazi, hayo ni mambo ya kiserikali, kawadanganye wasiojua. Hata yeye (Lissu ) akiwa Rais hataweka mikataba yote hadharani, hizo ni porojo za kisiasa tu.
Members, Mahojiano aliyoyafanya Mwandishi Jenerali Ulimwengu kupitia Jeneralionline pamoja na Tundu Lissu kuna mambo ya msingi Tundu Lissu amehoji.

Mosi: Je, mkataba wa kujenga uwanja wa ndege Chato lini ulipelekwa bungeni? Ni Mtanzania gani anafahamu kilichoandikwa ndani ya mkataba huo, Adai serikali inaleta maneno matamu tu kama zamani.

Pili, Mkataba wa stiglers gorge lini ulipelekwa bungeni ili kuhakiki kinachoandikwa na kusemwa ni kweli, adai haya mambo ya kuficha mkataba hakuna mwenye uchungu na rasilimali zetu, adai kwanini iwe siri.

Tatu, adai kwenye madini ni maneno tu yanazungumzwa, mkataba wa madini kati ya Barrick na Tanzania hujawahi peleka bungeni kujadiliwa, adai wanaongea tu majukwaani kupamba the mambo. Tundu Lissu anadai hakuna anayepigania madini nchi hii kwani mikataba imekuwa ikifichwa awamu zote mpaka sasa.

Tundu Lissu anadai yeye amekuwa akiomba mikataba iwe wazi tangu enzi za Mkapa mpaka sasa hii mikataba mipya inafichwa.

Je, kuna anayefahamu ukweli wa mambo haya, Mkataba wa uwanja wa ndege Chato nani anafahamu?

Je, na huu mkataba wa Barrick na Tanzania nani aliwahi kuuona, nini yameandikwa ndani ya mkataba?

Je, na ujenzi wa Stiglers Gorge nini kimeandikwa ndani ya mkataba na lini bunge lilijadili?
 
Mkuu kama una mkataba weka hapa, Hoja hujibiwa kwa hoja

Ukitukana ina maana wewe uwezo wako wa kujibu hoja na kufikiri ni mdogo

Weka mkataba hapa au Jibu hoja

Povu la nini kiongozi Jibu hoja mikataba ipo? Ilipelekwa bungeni?

Sheria inayotaka mikataba ijadiliwe bungeni na wewe iweke hapo tuone kama imevunjwa katiba, ukikosa mwambie tundu akusaidie.
 
Kwa hizi nondo tusahau Lissu kugombea Urais, yule bwana hana roho ya kuvumilia mawe kama haya.

Exactly. Katika vitu asivyoweza kuvumilia Magufuli na kusikia ni ukweli ambao utamuacha yeye na fedheha. Ukweli wa hivyo yeye huuita kutukanwa. Sababu hasa ya yeye kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ni ili aweze kudhibiti ukweli.
 
Bado hujajibu hoja yake kupata au kutopata diwani hata mmoja ni Jambo lakawaida! Swali wewe umeuona mkataba wa CHATO?
Du! Lissu akirudi hadithi itageuka hapa,maana CCM hawana hayo majibu,kila kitu anafanya Meko hata wao hawajui

Katika watu waliofeli hata kabla ya wakati ni lisu, kwanza kabisa swali moja tu atakaloulizwa ni kwamba,

Kwa nini mpaka sasa hatujashitakiwa na kunyolewa na MIGA kwa chupa?

Hatapata jibu, na majibu akijitahidi atasema, tanzania hakuna flyover, hiyo ya ubungo ni daraja tu, ma flyover yako ulaya.😁😁😁
Eti huyo ndo awe tishio?
 
Exactly. Katika vitu asivyoweza kuvumilia Magufuli na kusikia ukweli ambao utamuacha yeye na fedheha. Ukweli wa hivyo yeye huuita kutukanwa. Sababu hasa ya yeye kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ni ili aweze kudhibiti ukweli.
Kiongozi anaependa kusifiwa na kuabudiwa ni ngumu kukubali kukosolewa hata mara moja.

Mbaya zaidi anajiona yeye ndio kila kitu yaani hakuna mwenye uwezo kumzidi kati ya Watanzania ml 60.
 
Katika watu waliofeli hata kabla ya wakati ni lisu, kwanza kabisa swali moja tu atakaloulizwa ni kwamba,

Kwa nini mpaka sasa hatujashitakiwa na kunyolewa na MIGA kwa chupa?

Hatapata jibu, na majibu akijitahidi atasema, tanzania hakuna flyover, hiyo ya ubungo ni daraja tu, ma flyover yako ulaya.
Eti huyo ndo awe tishio?
Mkuu unafahamu maana ya MIGA?

Mambo haya ndio maana yanakuwa siri sana hasa mikataba

Serikali nyingi duniani zimesaini makubaliano na umoja wa mataifa kuhusu kulinda wawekezaji

Tanzania tumesaini mikataba mingi sana, Mpaka sasa kwenye MIGA convention hatujajitoa, Tunajua Madhara ya kujitoa kwenye hiyo mikataba kwani tutakuwa tumejitenga na dunia

Hivyo siri zinazoendelea ni kutokana na mambo hayo ya makubaliano ya kimataifa MIGA

Nani atakupa mkataba wa madini kwa sasa, Kuna mambo mengi nyuma ya pazia kiongozi

Hata Mkapa alisaini mikataba ya kuleta hao wachimba madini ilikuwa siri

Ametoka madarakani ndio tunapiga kelele sasa

Haya yanayoendelea huko stiglers gorge, SGR ni siri tu

Je ni mikopo inajenga stiglers gorge?
Je ni mikopo inajenga SGR?

Yote hayo yapo kwenye mkataba, Majukwaani Tunaambiwa Fedha za ndani
 
Back
Top Bottom