Mh.Tundu Lissu tunaomba utuache kwanza!!!Samahani saana

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Habari wakuu!!

Ninavyofahamu Mimi kwa upeo wangu mdogo pale MTU binafsi unapodhulumiwa haki yako nazani kila mmoja hujisikia vibaya na utapambana kwa hali yeyote uipate haki yako hata kama yule aliyekudhulumu alitumia sheria kukunyang'anya haki yako..

Najua fika kwamba haki inayoliliwa sasa na SJMT kutokana na makosa yaliyofanyika hapo nyuma itatugharimu saana kwani mchukua haki ana Nguvu kubwa mnooo..

Watanzania tufike wakati tuachane na UNAFIKI...hivi unazani wakati wa biashara za utumwa Mkoloni aliwahi waza kwamba anadhulumu? Nina imani kama angewaza hivyo Africa tusingekuwa hapa tulipo.

Hawa jamaa hawana uzuri saana kwetu, Siku zote ni watu wa maslahi yao kwanza..

Ktk hili namuunga mkono CinC wetu 100% hata kama tutarudi nyuma kama wazimbambwe Nina imani sisi wabongo ni wajanja zaidi ya Wazimbabwe..

Mh. Lissu naomba utuache kwanza kama vipi nenda Mjengoni ukampe mkuu mkakati wa kudai haki yetu.
 
Hawa jamaa hawana uzuri saana kwetu, Siku zote ni watu wa maslahi yao kwanza..
watu wanapawsa kuelewa tu hili na kuacha kuleta blabla zao kwenye mambo ya msingi,heri nusu shari kuliko shari kamili ni bora tuanze upya kwa manufaa ya kizazi kijacho hata kama itatugharimu lakini sio kuachie haya majaamaa yaendelea kutunyonya damu.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki JPM.
 
Muanze upya wakati ndio nyie nyie mmetufikisha hapa tulipo??? Mkataifishe mali za wote waliotufikisha hapa tulipo akiwemo huyo chenge wenu hadi mkapa mpaka dhaifu sio mnasema tunaanza upya wakati waliotufikisha hapa hapa tulipo bado wapo sehem ya hayo "MWANZO MPYA"
 
Sawa tuwaaache Mapimbi mpaka 2020..Zamu yenu bado!!
Mkuu huna hoja utasemaje akae pembeni wakati lisu amekuwa akipambana na wezi wa madini toka akiwa kijana mdogo hadi analala selo kila siku kule nyamongo na buhemba???? Alitoka hadi nje siku mnapitisha muswada kwa hati ya dharura huku magufuli akibaki ndani na alipiga kura ya Ndiooooooo then baada ya kumzomea na kumpuuza leo yamewakuta ndio mnatala akae kimya!!! Hapana hapana serikali mmeongea yenu acha opposition nao watoe maoni yao afterall nyie hamna moral authority ya kumkemea lisu maana ndio mmetufkisha hapa tulipo
 
Tume ya uchunguzi imefanya makosa makubwa yatayotugharimu sana kama taifa. Wamekuja na kuapply theory za darasani kwenye suala la uhalisia ambalo lina complexity zinazofanya theory isiwe 100%

Moja ya hasara kubwa ambalo ni intangible lakini ambalo lina impact kubwa ni kwamba Tanzania sasa tutaonekana kama nchi ya wapumbavu. Hili la mchanga na lile la Dangote linaziambia FDI kuwa Tanzania siyo pakugusa.
 
Lawama kwa sasa sio sahihi hebu kwa pamoja tujisahihishe tulipokosea tayali mkuu ameshaonesha ana nia njema na taifa hili
Sisi kwa nafasi zetu kwa weledi wetu wa elimu tulizonazo mnasaidia vipi tutoke kwenye dhuruma hii
Tuache vijembe vya nani alipigana vipi huko nyuma
Swali ni je tunatokaje humu bila kusababisha taflani?
Anayenielewa hebu aje hapa na mwelekeo mpya
 
watu wanapawsa kuelewa tu hili na kuacha kuleta blabla zao kwenye mambo ya msingi,heri nusu shari kuliko shari kamili ni bora tuanze upya kwa manufaa ya kizazi kijacho hata kama itatugharimu lakini sio kuachie haya majaamaa yaendelea kutunyonya damu.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki JPM.
Akosaye huadhibiwa msituletee ngonjera zenu hapa.
Ni kwamba hatuko radhi nanyi.
 
Nina imani hakuna anayefurahi Kuna nchi yetu inaibiwa madini yake mchana kweupe na wapinzani walikuwa wa kwanza kulalamikia aina ya mikataba Serikali iliyoingia na wawekezaji wa kuchimbaji wa madini lakini Serikali haikusikia.

Mpaka utawala wa Dr Kikwete ukatoa zoezi la kupitia upya mikataba upya ili kuangalia tunapata nini.

Na Sasa kamanda Rais Dr Magufuli ameamua kuunda Tume ili kuweka kila kitu wazi kuhusu madini na wizi unaofanyika.
 
Wewe mwehu kabisa, mbona hujamuuliza Lowasa na Sumayi?
Wapo kwenye chama chenu kwani??? Nmesema huwezi taka kuanza upya huku bado hao waliotufikisha hapo ni part ya MWANZO MPYA kumbuka chenge ni mmojawapo ila bado ni mwenyekiti wa bunge!!!! Hao kina mkapa na kikwete mtaifishe mali zao maana ndio wana final say sio mnaleta maneno maneno huku watu walijimilikisha hadi vimgodi huko......... baada ya hapo ndio muanze upya
 
Machadema majizi yanashirikiana na ACACIA
Ndio waliosainj mikataba ovyo namna hii na wawekezaji????

Je walibaki ndani na kupitisha miswada ya usimamizi wa nishati kma hizi kwa kura za ndio tena kwa hati ya dharura???

Embu tuanziea apo kwanza
 
Nashangaa kwa nini watu wana kuwa na wasiwasi na hatua tunazochukua kama nchi, badala ya kutafuta wapi tutatokea kama adui yetu akikimbilia tunakokuogopa, kwangu mimi pamoja na kuwa mimi si mwanasheria lakini kuna matobo mawili nayaona bayana.
  1. Uaminifu, katika hili hawa acacia kama kweli walikuwa wanazidisha uzito wa makontena tofauti na walivyo declare kama ilivyotajwa na ripoti huo ni wizi na uvunjifu wa uaminifu kitu ambacho kinavunja kiini cha mkataba wowote ule duniani.
  2. Kiwango kikubwa cha madini tofauti na walivyo declare hili ni kosa kubwa linavunja kiini cha mkataba pia linaweza kusababisha upande mmoja kukataa kuendelea na mkataba na yasiwepo madhara yoyote.
  3. Hakuna mahali popote duniani ambapo wizi au uvunjifu wa uaminifu unapewa tuzo
Cha msingi tuwe na uhakika na ripoti kuwa ni ya kweli, kweli tupu bila kusingizia chochote nina uhakika lazima wataomba po. Hawatakubali heshima yao ipotee duniani kuwa walikuwa wanatuibia hata hiyo sehemu yetu ndogo waliyopaswa kuilipa.
kwa taarifa tu ni kuwa yapo mashirika, taasisi na watu wengi tu duniani ambao wanapambana na makampuni ya kimataifa yanayoziibia nchi masikini, wanasubiri tu tulianzishe wajiunge kwenye vita. Shida tu huwa ni pale mwibiwaji hatoi ushirikiano. Kumbukeni change ya rada, ndege ya rais sio sisi tuliolianzisha, walilianzisha wazungu haohao wasiotaka raslimali za nchi masikini ziibiwe.
 
Habari wakuu!!

Ninavyofahamu Mimi kwa upeo wangu mdogo pale MTU binafsi unapodhulumiwa haki yako nazani kila mmoja hujisikia vibaya na utapambana kwa hali yeyote uipate haki yako hata kama yule aliyekudhulumu alitumia sheria kukunyang'anya haki yako..

Najua fika kwamba haki inayoliliwa sasa na SJMT kutokana na makosa yaliyofanyika hapo nyuma itatugharimu saana kwani mchukua haki ana Nguvu kubwa mnooo..

Watanzania tufike wakati tuachane na UNAFIKI...hivi unazani wakati wa biashara za utumwa Mkoloni aliwahi waza kwamba anadhulumu? Nina imani kama angewaza hivyo Africa tusingekuwa hapa tulipo.

Hawa jamaa hawana uzuri saana kwetu, Siku zote ni watu wa maslahi yao kwanza..

Ktk hili namuunga mkono CinC wetu 100% hata kama tutarudi nyuma kama wazimbambwe Nina imani sisi wabongo ni wajanja zaidi ya Wazimbabwe..

Mh. Lissu naomba utuache kwanza kama vipi nenda Mjengoni ukampe mkuu mkakati wa kudai haki yetu.
We darasa la ngapi? Mh, tunasafari ndefu kama ndio nyinyi
 
Lawama kwa sasa sio sahihi hebu kwa pamoja tujisahihishe tulipokosea tayali mkuu ameshaonesha ana nia njema na taifa hili
Sisi kwa nafasi zetu kwa weledi wetu wa elimu tulizonazo mnasaidia vipi tutoke kwenye dhuruma hii
Tuache vijembe vya nani alipigana vipi huko nyuma
Swali ni je tunatokaje humu bila kusababisha taflani?
Anayenielewa hebu aje hapa na mwelekeo mpya
Tatizo mkuu hata namna ya kujinasua hapa strategy inayotumiwa ni ya hovyo. Hali it aka yote peke kea hasara zaidi huko mbeleni.
 
Katika mambo kama haya...ndipo unaposhangazwa na akili za wanasiasa wanaoitwa wa upinzani katika taifa hili...........

Mambo waliyokuwa wakiyapigania yafanyike yakifanyika wanayapinga......

Yakitokea mambo mabaya kwenye wao ndio wa kwanza kupiga vigere gere na kupandikiza siasa.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom