Tundu Lissu ili kusaidia umma wa watanzania,kishauri chama chako kifungue kesi kupinga uteuzi wa wakurugenzi ambao umekiuka Sheria ya Utumishi wa Umma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,304
Kwanzani nikupongeze na pia nikushukuru kwa andiko lako kuhusu wakurugenzi ambalo umelitoa kumjibu Mwigulu Nchemba ambae nashindwa hata kumuita Dr. baada ya kusoma bandiko lako.

Baada ya kusoma majibu yako kwa Mwigulu,binafsi nakushauri wewe ukiwa kama Mwanasheria Mkuu wa chama, usiishie tu kumjibu Mwigulu,bali ukishauri chama chako kifungue kesi kupinga uteuzi wa wakurugenzi hawa ambao haukuzingatia sheria ya utumishimi wa umma kama ulivyoeleza katika andiko lako na hatua hii itakuwa na maana zaidi kuliko kuanika tu ukiukwaji wa sheria uliofanywa na watawala.

Kama chama cha siasa kisheria hakiwezi kufungua kesi ya aina hiyo,basi lolote lifanyike ili jambo hili lifikishwe mahakamani kama alivyofanya wakili karume na mteja wake bwana Wangwe.

Tuko tayari hata kuchangia gharama za kesi za aina hii maana ni za masilahi ya Taifa ni si CHADEMA kama chama cha siasa.

Tulinde sheria na katiba ya nchi yetu kwa vitendo na wakati ni huu.
 
Ni ushauri mzuri sana, japo viongozi madictator huwa hawaogopi mahakama bali huogopa nguvu ya umma.
 
Nadhani kuna kikwazo mahali. Mambo mengi yamekuwa yakidaiwa kukiuka sheria lakini mashtaka hayafunguliwi mahakamani. Mzee Neema alipovishutumu vyama vya upinzani alinyamazishwa kwa kuambiwa uteuzi wake kwenye Bodi ya Parole ni kinyume cha sheria kwani yeye siyo Jaji! Baadaye tukasikia na uteuzi wa Katibu wa Bunge nao ulikiuka sheria! Angalau uteuzi wa AG limepelekwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom