Tundu Lissu ieleze dunia kuwa kuna mbunge wa CCM amedai ana ushahidi wa tukio la wewe kushambuliwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,483
2,000
Mhe.Lissu, upatapo nafasi nyingine huko uliko, ieleze dunia kuwa kuna mbunge wa CCM katamka Bungeni kuwa ana ushahidi wa tukio la wewe kushambuliwa na uitake serikali kupitia Jeshi la Polisi imuhoji mhusika.

Waambie walimwengu wapime dhamira ya serikali kupitia kauli ya mbunge huyo anaepaswa kuwa shahidi na waeleze kuwa wakishindwa kumuhoji, basi dunia ijiongeze kujua ni kina nani walihusika.

Tena ieleze dunia unashangaa kwanini muhusika hajatakiwa kupeleka ushahidi wake Bungeni kama ambavyo wabunge wa upinzani hutakiwa kuleta ushahidi pindi wanapotoa tuhuma ndani ya Bunge.

Lissu kauli hii ni kete nyingine kwako hivyo usisite kuitumia.

Watu hawa wanaangamia na kudhalilika kwa kukosa maarifa!!

Hatutaraji watalalamika kuwa unawachafua maana hapa utakuwa unawasaidia wajisafishe.

CCM na serikali mje haraka kumkana Mollel, kauli yake inawatega nyinyi. - JamiiForums
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Nitashangaa kama huyo Mollel haijaitwa polisi hadi dakika hii, kwenda kusaidia uchunguzi "wanaodai" umekwama.
 

LIKE

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
4,526
2,000
utawala wa sheria laiti ungekuwa ni rahisi kuutekeleza huyu mbunge Mollel angelikuwa ameshaitwa kwenye ile Kamati maarufu ya Kinga,Maadili na Madaraka ya Bunge

kama alivyomuita CAG kwa Instagram pale aliponukuliwa akiliita bunge ni dhaifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,331
2,000
Bora ya kudeki kuliko ya kutetea mtu muuaji kisa tu anakulipa book 7!
Mkuu kuna kitu nimekigundua.Hawa wanaotetea unyama aliifanyiwa Lissu si wa kujibishana nao.Nia yao ni kuandika ubishi,upuuzi na mambo ya hovyo ili waharibu nyuzi.Wapuuzwe waletapo utoro na kama kweli wana hoja wajibiwe.
 

triss tie

Member
Jul 14, 2013
9
45
mi binafsi ningrpenda hats Kama uchunguzi was kumtambua aliehusika na shambulio la tundu lissu basi hata ipatikane riport kua CCTV camera ilikuaje zkatolewa baada tu ya shambulio la mbunge tundu lissu!!!.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom