Uchaguzi 2020 Tundu Lissu huna cha kutufundisha kuhusu Rais Magufuli, ni bora ukajikita kunadi Ilani ya CHADEMA

Saccos wana ilani kwani?. Ilani yao ni matusi, na kutembeza bakuli kwenye kampeni zao ndicho wajuacho. Taifa hili linahitaji kiongozi shupavu, Mzalendo, mwenye nia ya dhati ya kuwaleta maendeleo kwa watanzania. Bungeni tuliwapa nafasi, badala ya kutuwakilisha vyema nyie ni kupinga kila kitu, kususa,safari hii mtaula wa chuya. U Rais mpaka udiwani ni kijani tupu.
 
Bajeti ya mataga kumtetea mgombea wao mtandaoni imefyekelewa mbali. Bakini kupiga propaganda kwenye magroup huko
 
Kwani Elitwege unafundishwa au unaelezwa kuwa Magufuli ni mtekaji, muuaji na mvunjaji mkuu wa katiba ya nchi!
 
Saccos wana ilani kwani?. Ilani yao ni matusi, na kutembeza bakuli kwenye kampeni zao ndicho wajuacho. Taifa hili linahitaji kiongozi shupavu, Mzalendo, mwenye nia ya dhati ya kuwaleta maendeleo kwa watanzania. Bungeni tuliwapa nafasi, badala ya kutuwakilisha vyema nyie ni kupinga kila kitu, kususa,safari hii mtaula wa chuya. U Rais mpaka udiwani ni kijani tupu.
Endeleeni kujidanganya hadi vijijini lisu kawashika watu nilikuwa kamsamba huko sumbawanga ila vijana wanamkubali balaa hadi nikashangaa
 
Wenye akili zetu imara tunamuelewa vizuri sio huyo mzee wa makodi kila kona afu ndo ananunua ndege hizo hela zetu na kulipa wasanii kwenye kampeni bora lisu anaomba sio lazima kuchangia ila huyo jamaa ole usitoe kodi
 
Jana hadi wazee walivaa sare za chadema mbalizi maisha yamebadilika sana siku hizi zamani huwezi kuta mzee yupo chadema
 
W

Wenye akili zetu imara tunamuelewa vizuri sio huyo mzee wa makodi kila kona afu ndo ananunua ndege hizo hela zetu na kulipa wasanii kwenye kampeni bora lisu anaomba sio lazima kuchangia ila huyo jamaa ole usitoe kodi
we endelea kuota ukiamka nstue tujadili
 
Amani iwe nanyi.

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu, ukiacha Mgombea Urais wa CCM rais Magufuli anayetetea nafasi yake ananadi vizuri ilani ya chama chake, Wagombea wa vyama vingine hata ilani ya chama hawana!!

Mfano mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lisu ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kampeni akijaribu kuwafundisha watanzania kuhusu rais Magufuli alivyo! Yani Lisu badala ya kunadi ilani na Sera ya chama chake anatumia muda wote wa kampeni akitaja jina la Magufuli! Hivi Magufuli ndiyo ilani ya chadema?

Nikuambie tu Tundu Lisu, sisi watanzania huna cha kutufundisha kuhusu rais Magufuli.

1. Magufuli ametutumikia akiwa waziri kwa miaka 20 tangu enzi hizo kwenda Mtwara unatumia siku mbili kwenye meli, mpaka enzi hizi ambazo Mtwara unatumia masaa sita tu kufika ukiteleza kwenye lami, mjenzi wa mabarabara yote hayo ni Magufuli ,hivyo tunamjua huna cha kutufundisha.

2. Magufuli tulimchagua sisi wenyewe October 2015 tukiwa tunamjua na tumehangaika kwa miaka 5 akikomesha rushwa ufisadi,elimu bure, flyover na akirejesha nidhamu serikalini. Wewe Lissu ndiyo uje kutufundisha leo kuhusu Magufuli?

3. Tundu Lisu ulituambia tukibadili sheria za madini tutashitakiwa MIGA tukuulize je tumeshitakiwa MIGA?
Umekuwa mbunge kule Singida kwa miaka 10 je una lipi la kukumbukwa na wananchi wa jimbo lako?
Lisu umekuwa rais wa TLS je una lipi la kukumbukwa hapo?

Kwa ufupi sisi wananchi tunatakiwa tufundishwe kuhusu wewe Lisu ni mtu wa namna gani kwa sababu huna kitu cha kuonekana ulichowafanyia wananchi zaidi ya makelele na kutukana serikali.

Tundu Lisu wewe siyo mzalendo wa nchi yetu hivyo hufai kuwa rais na hutakaa uwe rais wa Tanzania na tarehe 28 October tutakupa fundisho kali la kwamba watanzania siyo wajinga wa kuchagua mtu yoyote hata mtetezi wa mabeberu.
 
Kila mmoja ana haki ya kunadi sera zake, kuonyesha kwa nini achaguliwe, pia kuelekeza kwanini mwenzake asichaguliwe, hiyo ndio siasa! Na kila mmoja anafanya hivyo, sio Lissu pekee, ingawa unamuona yeye tu, vumilia!
 
Tume ya uchaguzi na takukuru naamini hawako vizuri, kwasababu mambo mengi yanakiukwa, uweze kuomba kura hapo hapo unatoa amri ya kutekeleza ujenzi wa miundo mbinu ambayo haipo hata kwenye bajeti, hii ni rushwa! Vyombo vinavyosimamia vinapaswa kuvunja kabisa!
 
Binafsi nimehudhuria mkutano wa CCM kuanzia Bukoba Mjini na Biharamulo. Kagera na haswa Biharamulo wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea wa CCM John Magufuli, yanayosemwa ni uzushi tu..ukweli usemwe, Kama hukua eneo la tukio usipoteze muda kubishana
watu wameenda kuwatazama akina Ali Kiba kuona show ya bure
 
Penye chadema weka ccm and vice versa Penye Tundu Lissu weka magufuli and vice versa ....
 
Amani iwe nanyi.

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu, ukiacha Mgombea Urais wa CCM rais Magufuli anayetetea nafasi yake ananadi vizuri ilani ya chama chake, Wagombea wa vyama vingine hata ilani ya chama hawana!!

Mfano mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lisu ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kampeni akijaribu kuwafundisha watanzania kuhusu rais Magufuli alivyo! Yani Lisu badala ya kunadi ilani na Sera ya chama chake anatumia muda wote wa kampeni akitaja jina la Magufuli! Hivi Magufuli ndiyo ilani ya chadema?

Nikuambie tu Tundu Lisu, sisi watanzania huna cha kutufundisha kuhusu rais Magufuli.

1. Magufuli ametutumikia akiwa waziri kwa miaka 20 tangu enzi hizo kwenda Mtwara unatumia siku mbili kwenye meli, mpaka enzi hizi ambazo Mtwara unatumia masaa sita tu kufika ukiteleza kwenye lami, mjenzi wa mabarabara yote hayo ni Magufuli ,hivyo tunamjua huna cha kutufundisha.

2. Magufuli tulimchagua sisi wenyewe October 2015 tukiwa tunamjua na tumehangaika kwa miaka 5 akikomesha rushwa ufisadi,elimu bure, flyover na akirejesha nidhamu serikalini. Wewe Lissu ndiyo uje kutufundisha leo kuhusu Magufuli?

3. Tundu Lisu ulituambia tukibadili sheria za madini tutashitakiwa MIGA tukuulize je tumeshitakiwa MIGA?
Umekuwa mbunge kule Singida kwa miaka 10 je una lipi la kukumbukwa na wananchi wa jimbo lako?
Lisu umekuwa rais wa TLS je una lipi la kukumbukwa hapo?

Kwa ufupi sisi wananchi tunatakiwa tufundishwe kuhusu wewe Lisu ni mtu wa namna gani kwa sababu huna kitu cha kuonekana ulichowafanyia wananchi zaidi ya makelele na kutukana serikali.

Tundu Lisu wewe siyo mzalendo wa nchi yetu hivyo hufai kuwa rais na hutakaa uwe rais wa Tanzania na tarehe 28 October tutakupa fundisho kali la kwamba watanzania siyo wajinga wa kuchagua mtu yoyote hata mtetezi wa mabeberu.

Mimi natofautina sana na hoja yako nimesoma ilani ya CCM na nimesoma ilani ya CDM kwa kifupi ilani ya CCM ni ile ile ya kufikiria serikali italeta maendeleo katika hii nchi. Ilani yote imejaa serikali itajenga shule, itajenga hospital, itajenga barabara itajenga reli itajenga viwanja vya michezo itajenga bwawa la Umeme na kadhalika.

Lakini haisemi baada ya kuwa na ilani za kufanya vitu hivyo zaidi ya miaka 50 inakuwaje wananchi bado wanaendelea kuwa masikini wanakabiliwa na maradhi pamoja na ujinga. Kimsingi hakuna kimya katika hiyo ilani. Haisemi ni namna gani wananchi wanaweza kujipatia maendeleo yao.

Ukisoma ilani ya CDM kwa kiasi kikubwa inazungumzia mambo mapya yanayoweza kuleta mabadiliko kwa mwananchi, kwanza inazungumzia ugatuzi wa madaraka jambo ambalo litasaidia kuondoa ufisaji wa rasilimali za nchi.

Pili inaongelea sekta binafsi kwasababu hiyo ndiyo njia pekee ya kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwasababu sekta binafsi ndiyo inayoajiri watanzania wengi kuwa na sera ya kukuza sekta binafsi ni sawa na kuwa na sera ya kuwaendeleza wananchi moja kwa moja badala ya kuwa ombaomba kwa serikali.

Wanazungumzia kodi, kila mtu anaona biashara nyingi zinakufa sababu ya kodi kubwa ni vema kuangalia kodi itozwe kiasi gani ili kuweza kukuza biashara na hivyo kuwa na wito mkubwa zaidi wa kupata kodi kuliko utitiri wa kodi ambayo matokeo yake ni kuua biashara na kusababisha hali ya umasikini zaidi kwa watanzania walio wengi.

Tatu CDM inazungumzia uhuru wa wananchi kufanya shuguli zao na kuuza mazao yao popote wanaopona pana Soko zuri badala ya serikali kuwapangia na hivyo kulazimika kuuza mazao ya kwa hasara na hivyo kuzidi kuwa masikini.

Nne CDM inazungumzia kumjali mfanyakazi kwa kumalipa vizuri pamoja na kuwalipa wastaafu malipo Haya yanapofanyika yanasababisha kuleta nafuu ya maisha kwa wafanyakazi, wastaafu pamoja na wategemezi wao. Lakini pia wanapozungumzia wakulima kuruhusiwa kuuza mazao yao popote penye soko zuri pamoja na kupunguza utitiri wa kodi wanalenga kutatua kilio kikubwa cha watu kuwa na maisha magumu wakati nchi yetu ni tajiri sana.

Kwa ujumla sera ya CCM ni kuendeleza Uchumi dola ambao haujawahi kumnufaisha mwananchi wa kawaida na badala yake sera hiyo ilijaribiwa na awamu yankwanza ikashindwa.

Sera ya CDM ni ya ugatuzi wa madaraka pamoja kushirikisha sekta bianfsi katika miradi ya maendeleo ambayo ni nzuri inafanya miradi mingi itekelezwe kwa ufanisi bila nchi kuingia kwenye madeni makubwa na hivyo kutumia sehemu kubwa ya mapato yake kulipia deni.

Kwakweli kwa vyovyote vile ili wananchi waweze kupata maendeleo yao hatuwezi kuendelea na sera zile zile miaka nenda rudi ipo haja ya kuangalia upya nini kifanyike jambo ambalo CCM haijafanya imebakia na mazoea ambayo hayawezi kutuletea mabadiliko tunayohitaji.
 
Back
Top Bottom