Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
 
Kwa jinsi hiyo mikataba ilivyoandaliwa na inavoikaba Serikali zoezi la kuijadili upya ni kizungumkuti. Labda wanasheria wangeshauri kitaalam nchi itajiondoa vipi kwenye shimo hilo la mikataba mibovu bila kukiuka haki za wahusika kama zilivyoainishwa ndani ya mikataba hiyo.
 
Alivyomtaja Evo Morales kanifurahisha

Evo ni jembe

Evo Morales
Hugo Chavez
Castro

Marafiki walioshibana ambao ni anti imperialist's,wamewasumbua sana USA ,walikataa kuuza nchi zao ,ardhi zao..walikuwa mabest na evo&hugo walimsaidia sana Castro ,mafuta na gas yao iliwasaidia wacuba

Long live Evo
Jembe lililobakia
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
 
Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
 
Kwa jinsi hiyo mikataba ilivyoandaliwa na inavoikaba Serikali zoezi la kuijadili upya ni kizungumkuti. Labda wanasheria wangeshauri kitaalam nchi itajiondoa vipi kwenye shimo hilo la mikataba mibovu bila kukiuka haki za wahusika kama zilivyoainishwa ndani ya mikataba hiyo.

Ukimsoma vizuri Lissu ametoa suluhisho ambalo kama Taifa linaweza likafanya,hivyo pamoja na kumlaumu Rais Magufuli kwa kutoa angalizo,ametoa na SULUHISHO.

Soma paragraph yake ya Mwisho
 
Bure kabisa!! wakati mwingine shughukisha akili yako kidogo Mh. Hivi serikali inapopata taarifa kuwa mchanga unaosafirishwa si makinikia bali ni mchanga wenye dhahabu unataka Rais wa JMT afanye nini?? Aache tu kwa kuwa kuna mkataba wa kusafirisha mchanga au unatafuta kiki??

Tatizo sababu amesema Lissu angeyasema haya Kigwangala au Nchemba mngepiga MAKOFI.Anyway msome taratibu,ameongelea SHERIA zinazotubana na namna ya kuziepuka SHERIA hizo/MIKATABA hiyo ya hovyo.

Ni wewe kurudia kuisoma au kuendelea kufikiria Kama BASHITE
 
Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
Mchanga kama kutetesi una dhahabu na wala si makinikia kama makubaliano yalivyo! Unataka uruhusiwe mchanga usafirishwe ushahidi utapata wapi?? Hebu tumieni akili kidogo basi..
 
Mambo yanayohitaji Sheria yaendeshwe kutumia Sheria. Mikataba ni Sheria. Ni vyema tukafuata maana kila mkataba una kipengele cha hamna ya Ana kuu una au kusuluhisha iwapo kutakuwa na mgogoro wa kimaslahi kwa pande yeyote ile. Tunachokifanya sasa kwa upande wa madini hakipo katika kipengele chochote. Zaidi sana ubabe huu utauingiza taifa katika majanga ya malipo makubwa sana ya fidia. Tunajiandaa kujikaangaa kwa mafuta yetu wenyewe. Sijui ni laana gani hii tuliyoipata nchi hii!!!
 
Tatizo sababu amesema Lissu angeyasema haya Kigwangala au Nchemba mngepiga MAKOFI.Anyway msome taratibu,ameongelea SHERIA zinazotubana na namna ya kuziepuka SHERIA hizo/MIKATABA hiyo ya hovyo.

Ni wewe kurudia kuisoma au kuendelea kufikiria Kama BASHITE
Kama mkataba/sheria inamruhusu kusafirisha makinikia na badala yake anasafirika mchanga wenye dhahabu na wala si makinikia then mwenye kosa ni mwekezaji mwenyewe. Kwenye hili Lissu amakurupuka au anataka wampe kazi au tayari wameshampa kazi ya kuwa tetea mafisadi wa dhahabu
 
Mambo yanayohitaji Sheria yaendeshwe kutumia Sheria. Mikataba ni Sheria. Ni vyema tukafuata maana kila mkataba una kipengele cha namna ya ama kuvunja mkataba au kusuluhisha iwapo kutakuwa na mgogoro wa kimaslahi kwa pande yeyote ile. Tunachokifanya sasa kwa upande wa madini hakipo katika kipengele chochote. Zaidi sana ubabe huu utauingiza taifa katika majanga ya malipo makubwa sana ya fidia. Tunajiandaa kujikaangaa kwa mafuta yetu wenyewe. Sijui ni laana gani hii tuliyoipata nchi hii!!!
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom