Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hawezi kushinda Uchaguzi wa 2020, Dkt. Magufuli ana nafasi kubwa ya kushinda

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi kwa wagombea wa nafasi ya uraisi 15 huku wengine wakishindwa kufanya kampeni na wengine kujitoa na huyu Tundu Lissu kupata wafuasi wengi lakini wanaokwenda kumshangaa kupona kufa baada ya risasi 38 na 16 kumpata mwilini.

Majority ya Watanzania wana imani kubwa sana na Serikali ya awamu ya 5 kutokana na yale yaliyofanyika hivyo sio rahisi kwa Tundu Lissu kushinda uchaguzi

Mh. Magufuli atashinda uchaguzi huu kwa asilimia kubwa kutokana na Watanzania kujenga imani naye.

Matamshi ya Tundu Lissu na Maalim Seif kwenye uchaguzi huu ni matamshi ya shari na sio ya amani na Watanzania hawapendi machafuko hivyo sio rahisi kabisa kushinda.
 
Hilo halina ubishi

Watoto wa kitaa wanasema mzee Magu kawafundisha kuchapa kazi. Eti siku hizi hakuna pesa za deals.....Na wanamsifu kwa hilo.

Nikiwahi kusema Tundu ni sawa na mfanyabiashara wa beer na kitimoto anayeamua kwenda kuwekeza Mecca au madina
 
Sijui unaishi wapi nchi hii?

Hakuna namna Magufuli anaweza kushinda bila hila na anajua ukweli huu ndio maana ameisuka NEC kwa watu wake wa ukoo.

Magufuli mwenyewe hajiamini hata kidogo ndio maana mtu mzima anapiga magoti kuomba achaguliwe licha ya kujitapa miaka 5 na madaraja anayojenga. Ongea ukweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom