Tundu Lissu hataipita njia ya Yusuph Manji, ni 'mjanjamjanja'

Hana cha ujanja wowote, si kakataa ku cooperate (kupimwa mkojo) basi ataendelea kukaa mahabusi mpaka Polisi watakapo kamilisha upelelezi kwa kutumia vyanzo vingine

Kama angekubali kupimwa mkojo nadhani mda huu angekuwa mtaani

Unajua sheria zinazotaka kumpima mtu mkojo na damu??Ni mahakama peke yake na inamfumo wake,hayo mengine mje mumsingizie anatumia Sembe la CCM.
 
Tundu Lissu ni moja ya watu wa kipekee tuliobaki nao Tz.

Sisemi kama nakubaliana au sikubaliani na ayafanyafo Mh. TL, la hasha, nawaza tu kwa sauti. Hivi kwa uwezo wa kiakili na weredi wa masuala ya kisheria alio nao Mh. TL, si angeweza kujikalia kimya akipiga dili zake mbali mbali na kujilimbikizia ukwasi wa kutisha? Lakini mbali na hayo yote jamaa, yupo busy kuendesha mapambano juu ya yale anayoyaamini hayapo sawa.

Mbona kuna wapinzani wengi tu ikiwemo mpaka katika chama chake wamejikalia kimya wakila mkate wao kimya kimya bila bugudha? Natamani sana tungemuelewa TL, natamani sana mtu huyu angekuwa kwenye mifumo yetu ya kiutawala. Namshukuru sana Mungu kwamba nimeishi na kumuona mtu mwenye haiba kama ya TL Zaidi ya wengi ambao nimesoma tu historia zao bila kuona mwenyewe uwepo wako. Nadiriki kusema huyu jamaa sio mbinafsi Zaidi tu ya kile kiburi chake cha weredi.

Kwa matendo ya huyu jamaa, naamini anajua hakika duniani ni mahala pa kupita tu, hivyo kuendelea kuishi miyoyoni mwa watu ni lazima ufanye jambo Fulani ambalo litaacha utambulisho wako. Jambo hilo si pesa, majumba wala cheo isipokuwa ni mawazo ambayo yana mlengo wa kuiboresha jamii inayokuzunguka.

Pamoja na yote Mh. TL ni hazina kwetu ambayo naamini ana kitu kikubwa ndani yake lakini tu siasa zetu hazipendi watu wa aina yake. Naamini baada ya miaka mingi kupita huyu jamaa atakuja kukumbukwa sana na vizazi vijavyo.
 
Mfanyabishara maarufu nchini Tanzania na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kwasasa yuko mahabusu huku akiwa na mashtaka kadhaa mahakamani. Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA; Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS naye yuko mahabusu tayari kwa kufikishwa mahakamani. Inaelezwa, uchunguzi unaendelea.

Manji alikamatwa. Akahojiwa. Akawekwa mahabusu. Akapelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kufanyiwa vipimo vya mkojo. Akafunguliwa mashtaka ya kutumia madawa kabla ya mapya ya vifaa vya kijeshi na nyaraka mbalimbali. Lissu alikamatwa. Akahojiwa. Akawekwa mahabusu. Akapelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Akagoma kupimwa.

Hakika, Lissu hawezi wala haitakuwa rahisi kupitishwa njia aliyopitishwa Yusuph Manji. Lissu ni 'mjanjamjanja' wa kisheria. Anajua anachokisema au anachokifanya. Anajua cha kukataa na kukubali. Anajua cha kupimwa na cha kukataa kupimwa. Anajua kutetea wengine na yeye mwenyewe mahakamani.

Kilichobaki ni kumpeleka mahakamani na kumsomea mashtaka tu kwa kile alichokuwa akishikiliwa na kuchunguzwa kwacho.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
Hahaha nachekaga Sana nikisoma ...[HASHTAG]#bastola[/HASHTAG] ya nini tena??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LISU NI MHAINI AWEKWE KIZUIZINI

Na Thadei Ole Mushi.

Mwalimu wangu alishawahi kunifundisha kwenye history kuwa siku zote unapopanga kufanya MAPINDUZI hakikisha unakubaliana na matokeo haya mawili

1.Ukifanikiwa katika mapinduzi yako watakuita SHUJAA ,MWANAMAPINDUZI, NA KILA JINA LA KISHUJAA.

[HASHTAG]#ILA[/HASHTAG]

2. Ukishindwa kwenye mapinduzi hayo watakuita jina moja tu "MHAINI".

Kinachomtokea TUNDU kwa sasa ni hili jibu la pili huyu anatakiwa awekwe KIZUIZINI kama watanzania wengine waliokwisha kujaribu kusaliti nchi yao na kuwekwa kizuizini.

[HASHTAG]#Anachotakiwa[/HASHTAG] kukithibitisha Lisu ni Udikteta wa Raisi magufuli. Kama kuteua msukuma kuwa kiongozi mahali ndio Udikteta basi atuthibitishie.

[HASHTAG]#Najua[/HASHTAG] wote wanaochaguliwa au Kuteuliwa na Mh Raisi wanapendekezwa na mamlaka za Uteuzi baada ya kufanyiwa vetting. Je Lisu yupo kwenye mamlaka za uteuzi ili aseme mapendekezo ya mamlaka hizo yamepuuzwa na Raisi?

#Je Mh Raisi ndio anayetoa vibali vya wakatoliki kufanya kazi nchini na si Uhamiaji? Kama ni uhamiaji je wakatoliki hawaruhusiwi kufanya kazi hapa nchini? Je hao wamisionari wa kilutheri walioambiwa wakapange foleni kule Uhamiaji walitaka nani awape kibali cha kufanya kazi nchini? Je uhamiaji waliwanyima kibali kwa kuwa ni walutheri?

[HASHTAG]#Nimemsikiliza[/HASHTAG] Fatma Karume wakili wa Lisu akitoa tafsiri ya kosa la Uchochezi kuwa ni kumchochea mtu kufanya uhalifu na yeye haoni kama lisu alimchochea mtu.

[HASHTAG]#Huyu[/HASHTAG] naye akili hazipo sawa haoni aliyechochewa kabisa ila anasahau kuwa Lisu anawaaminisha watanzania kuwa Raisi Magufuli anapendelea kabila lake pamoja na Dini yake. Haoni kuwa anawachochea makabila mengine na dini nyingine?

[HASHTAG]#Mataifa[/HASHTAG] mengi yanaingia matatizoni kwa kauli za kichochezi kama hizi. Je wasukuma na wakatoliki wanaofanya kazi maeneo mengine wabaguliwe? Lisu anataka haya makabila na dini nyingine zifanye nini? Nyumbu hawaoni uchochezi huu wanasahau vita haina macho...

[HASHTAG]#Nitashangaa[/HASHTAG] kama upande wa Jamhuri watamuachia huru kwa kauli hizi. Kama mkimuachia basi mtakuwa kawashinda kuwa kweli analiyoyasema yanafanywa kweli na Raisi.

Ole mushi
 
Kwa maoni yangu naona wanampandishia Lissu chati yake kisiasa kuliko kama wangeamua kumpotezea kwa alichosema! Kwa sasa idadi ya sympathisers wake inazidi kuongezeka na naamini kabisa kuna ccm wengi wako kwenye kundi hilo pia kutokana na ujasiri wake wa kuweza kusimama hadharani na kumnyooshea kidole mtukufu sana!

Au ndio sikio.la kufa halisikii dawa...
Hapo ndo wanasikia rahaaaa moyoni wakimkamata hvy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
\

Kwa mantiki hiyo mnataka kumbakiza matumizi ya madawa ya kulevya? Hivi kwa nini ninyi binadamu mnachezea sana raslimali watu za taifa ambazo kama mngezitumia kwa hekima zingeipaisha sana hii nchi katika nyanja zote na kwa watu wa viwango vyote? Mna nini nyie?
polisi mnatia aibu sasa hayo ya kupima mkojo yametokea wapi?
 
Tundu Lissu ni moja ya watu wa kipekee tuliobaki nao Tz.

Sisemi kama nakubaliana au sikubaliani na ayafanyafo Mh. TL, la hasha, nawaza tu kwa sauti. Hivi kwa uwezo wa kiakili na weredi wa masuala ya kisheria alio nao Mh. TL, si angeweza kujikalia kimya akipiga dili zake mbali mbali na kujilimbikizia ukwasi wa kutisha? Lakini mbali na hayo yote jamaa, yupo busy kuendesha mapambano juu ya yale anayoyaamini hayapo sawa.

Mbona kuna wapinzani wengi tu ikiwemo mpaka katika chama chake wamejikalia kimya wakila mkate wao kimya kimya bila bugudha? Natamani sana tungemuelewa TL, natamani sana mtu huyu angekuwa kwenye mifumo yetu ya kiutawala. Namshukuru sana Mungu kwamba nimeishi na kumuona mtu mwenye haiba kama ya TL Zaidi ya wengi ambao nimesoma tu historia zao bila kuona mwenyewe uwepo wako. Nadiriki kusema huyu jamaa sio mbinafsi Zaidi tu ya kile kiburi chake cha weredi.

Kwa matendo ya huyu jamaa, naamini anajua hakika duniani ni mahala pa kupita tu, hivyo kuendelea kuishi miyoyoni mwa watu ni lazima ufanye jambo Fulani ambalo litaacha utambulisho wako. Jambo hilo si pesa, majumba wala cheo isipokuwa ni mawazo ambayo yana mlengo wa kuiboresha jamii inayokuzunguka.

Pamoja na yote Mh. TL ni hazina kwetu ambayo naamini ana kitu kikubwa ndani yake lakini tu siasa zetu hazipendi watu wa aina yake. Naamini baada ya miaka mingi kupita huyu jamaa atakuja kukumbukwa sana na vizazi vijavyo.
Km uko kichwani kwangu
Sikuwahi kuomuona sokoine nimemsoma tu kwangu Tundu Lisu ndio baba lao. Wazalendo wote inabidi wajifunze kwa jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom