Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati

Mkuu kwa vifungu ulivyo nukuu mwenyewe huko juu, kampeni huanza baada ya nomination ya tume. Kwa tafsiri hiyo hakuna kitu kinaweza kuitwa kampeni so far sababu tume bado haijafanya nomination.

Ukiachana na tafsiri za kisheria, kwa maana tu ya kawaida unawezaje kusema mtu anafanya kampeni kabla ya uteuzi wa tume, je asipopitishwa na tume kugombea?

Unasema Magu alikuwa akitafuta wadhamini bali Lissu anafanya kampeni, unawezaje kutofautisha kutafuta udhamini na kufanya kampeni?

Je tume imeweka utaratibu wowote wa ni namna gani mtu akutane na wadhamini wake hadi useme anavyofanya Magu ni sawa na Lissu anakosea?
Unajadili kwa hasira sana ila ii kuwa wakati Magufuli anaongea na wana CCM ndipo alikuwa anatafuta wadhamini kama mgombea ndani ya chama chake, hakukusanya mkutano wa hadhara kutafuta wadhamini. Kosa hili limeshafanyika sana Tanzania lakini ni kinyume cha sheria,

Alipokuwa anaongea na wanachi njiani kutoka Lupaso, alikuwa anaongea nao kama rais wa Tanzania, na ni sehemu ya amjukumu yake katika position hiyo. Hapo ndipo power of incumbency inambeba, na huwezi kuitengua kwa sababu yeye ni Magufuli jiwe. bali ataendeleakuwa Rais hadi October 30.
 
Kwasasa JPM ni Mgombea urais anapoenda Dodoma kuchukua form au kutafuta wadhamini anaenda kama mgombea na sio rais,jaribu kutofautisha kazi za Rais na mwenyekiti wa CCM ,Alivyoenda Lupaso alienda kama Rais.

Ndio maana tunataka katiba mpya kuondoa hayo makando kando(Loop holes) kufanya kampeni kwa kujifanya eti ni rais na sio mgombea.
Sipati picha anayesikiliza hiyo kesi ya kampeni kama rais au kampeni kama mgombea. Akiwepo huyo mtafuta wadhamini
 
Hawa jamaa huwa wanapenda kumbeza Lissu kwa kila kitu kwa sababu za kisiasa, ila bro trust me...ni vigumu sana kumpata Lissu na hatia tena kwa makosa ya jinai, sababu sheria ameifanya kuwa sehemu ya maisha yake na ana slogan yake anasemaga, 'namna nzuri ya kutii sheria mbovu ni kuzivunja'.

Ndio maana wamembambika kesi nyingi sana na hawajafanikiwa kumpata na hatia so far. Kitu kingine, watanzania wengi hatuna uelewa wa sheria na mienenendo ya kesi mahakamani hadi kumpata mtu na hatia si mchezo.

Hata wengi wamefungwa sababu hawana wasaidizi wa sheria, nadhani pia ulimskia Lissu kule Nyamongo alitoa vifungoni watu zaidi ya 400 waliokuwa wamefungwa kinyume na sheria, imagine watu 400 ni kijiji kizima kipo jela kinyume na sheria ama sababu ya uonevu au maelekezo toka juu.

Kweli kabisa njia nzuri kutii sheria mbovu ni kuzivunja safi ,Lissu hawa mapolisi na AG makanjanja hawawezi kumpata.
 
Inabidi kuwa makini na hizo haki. Magufuli akiagize viongozi kukamilisha ujenzi wa mradi wowote, anaweza kuonekana anapiga kampeini, lakini siyo kweli atakeleza majukumu yake ya uraisi. Akiahidi kuwa serikali itafanya jambo fulani, bado ni mojawapo ya majukumu yake kama kiongozi wa serikali. Anaposema kuwa Mbunge fulani hakuleta matatizo ya jimbo lake serikalini kushghulikiwa ndiyo maana jimbo hilo halikuudumiwa kwa vile matatizo yake yalikuwa hayajulikani serikalini, bado ni sehemu ya kazi zake za uraisi. Kwa hiyo ukichambua sana utaona kuwa kuna mambo machache sana ambayo hawezi kuyasema kama raisi. Kubwa asiloruhusiwa ni kutumia majina ya chellengers wake kwenye mikutano yake ya kikazi kwa kuwaponda.
Anapowaambia wananchi ambao ndiyo wapiga kura kuwa msifanye tena makosa kama kipindi kile bali muwachague wanaotokana na ccm. Hiyo imekaaje??
 
Anapowaambia wananchi ambao ndiyo wapiga kura kuwa msifanye tena makosa kama kipindi kile bali muwachague wanaotokana na ccm. Hiyo imekaaje??
Unfortunately bado ni sehemu ya majukumu yake kama rais; it sounds unfair but legal.
 
Back
Top Bottom