Tundu Lissu: Hakuna atakayefanya kazi za CCM akajiita mwana CHADEMA tukamwacha

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
0
Wanabodi,

Ametoa kauli hiyo alipoulizwa na Mtangazaji wa ETV Kuhusu usaliti unaofanywa na Wanaoumbuliwa na Kamanda BEN Saanane. Amedai wanafanya hayo wamkimlenga Dr kwa Mapendo watanzania waliyo nayo anzia akiwa Mbunge wa Karatu na URAIS.

Hivyo kuna kundi linawatumia kwani linamwona Dr Slaa ni tishio linatumia fedha nyingi kuwapa wamwangamize. Akashukuru USALITI wao umebainika na chama kitawashulikia kwa mujibu wa taratibu bila kujali wao ni wakina nani.

Wazee wa PM7 Mmeshanipata?

Wana JF Habari ndiyo hiyo toka kwa Mnadhimu wa Kambi RASMI.

Changia maoni juu ya mtazamo wa kamanda Lissu dhidi ya wakina masalia or PM7, Hatua watakazochukuliwa.
 

123Kape

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
464
0
yaani hapa patamu me nafikiri huyu zitto amekwishatuwia mzigo mzitto....anang@ata na kupuliza ka panya....anajua kula na vipofu sasa hakujua kumbe wengine chongo wamemwona:A S angry:
 

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,379
2,000
Safi sana tupo na ninyi kamanda Lissu. Msiwafukuze kwenye chama. Cha kufanya ni kutowashirikisha shughuli yoyote ya chama. Halafu tukabizini sisi umma kazi ya kuwashughulikia. Hatutawaacha wakanyage jukwaani kuhutubia wakijifichia kivuli cha chadema. Labda wapande kwa jukwaa la ccm waliokuwa wakiifanyia kazi kwa kusaliti chama.
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!
.
 

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,350
2,000
Nashauri waitwe na waulizwe,,, mwenyekiti awe prf safari,mbowe na slaa wasiwepo,wahojiwe na kamati ya pr safari.
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
No individual is bigger than CHADEMA,,,

Well said by Kamanda Lissu,,,, Kuna watu wanatembelea nyota na umaarufu wa zamani na hivyo wanaona wivu chama kinavyokuwa na kuwa na Makamanda wengi makini hivyo wao wanafunikwa...

Wiki hii nzuri sana, kuna wachawi wengine wanaitwa MAYAN walikuwa wanatishia kuwa leo ndio doomsday watu wote tutakufa lakini muda waliotabiri umepita na watu tuko poa. Hivyo hatuogopi huo uchawi wao wa Leka Tutigite
 

Kanundu

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
889
0
Hakuna aliye juu zaidi ya chama. Kama ni watu kuwa na damu ya CHADEMA, ni wale walio tangulia mbele ya haki kwa kukatizwa maisha yao wakati wa harakati za kukipigania/kuendeleza chama. CHADEMA iwashughulikie kulingana na taratibu za chama.

Na kwa vile ni viongozi wa juu wa chama, ni vyema CHADEMA ikaonyesha mfano wa hali ya juu kwa kutoa adhabu kali hasa kwa mtu aliye lewa majivuno na kujitapa kwamba ameitoa mbali CHADEMA.

Suala kwamba hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote sio hoja ya msingi kwetu. Hoja ya msingi kwetu ni kwa vipi unakisaliti chama!!!!!

Washughulikiwe ili kuwa mfano kwa wengine.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,792
2,000
Hao wasaliti Umma umeshawajua na wanafahamika. Na mfadhili wao huyo Mchawi anajulikana.

Hao vijana waende kwenye maombi wakaombewe ili hayo mapepo ya uzezeta yawatoke. Waache njaa zao uchwara maana wananchi wana njaa za ukweli na wananchi wanategemea CHADEMA kwa ukombozi.

Waachwe tu wasifukuzwe na watengwe katika shughuli za CHAMA kama wao walivyoanza kujitenga na kufanya njama za Kubomoa Chama. Kumbe yule Mjumbe wa NEC wa magamba (ChimpA MZee) aliyesema CDM itakufa alikuwa anajua hiyo failed mission!!!

Watajiondoa wenyewe hao wasaliti na Watalaaniwa maana Watanzania wanataka ukombozi.

yeye aendelee kuruka ruka na mamiss, hata kuoa bado unataka ustate man, aaa wapi.

Hongera BEN Saanane!!! Big up and Hongera Mamuya, uko juuu!!!!
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Hao wahuni wa PM7 ni lazima wafukuzwe ili tujue kwamba chama chetu kipo serious na mamluki wote, muda huu hakuta kuwa na propaganda za kudanganya watu kuwa wamefukuzwa kwa ajilii sijui ya ukanda na ukavila kwani ushidi upo wazi na kila mtu anajua kutokana na kazi nzuri ya kijana wetu @Ben sanane, tumeona mpaka mesage za Zitoo kwa Ben na za kafulia juu ya kuhujumu chama pia kama Audio Ben anazo pia za hao PM7 na huyo Prezoo wao.

CHADEMA FUKUZENI WAHUNI HAO.
 

Kisiya Jr.

Senior Member
Nov 21, 2011
102
0
Mi binafsi nawashangaa sana mnamsifia BEN SAANANE na kumuona ni brave and hero. That z non sense and hopeless for the critical thinkers.

Mi binsfsi naona kiwembe kitakachowanyoa kimwanzie yeye kama kweli hatumiwi na Dr.Slaa kuwachafua wengine,maana kama ametumika kambi mbili zote zinazozozana ni dhahili shahili huyu ni chumia tumbo.

Anaonekana ni mpika majungu kibuhu kwa manufaa yake,na pale yanapokwama anajifanya mtu mwema sana.

Kwa mwenye akili ashajua kama jamaa ni Petro na Yuda kwa wakristo mtakua mnanielewa.

Zitto na kundi lako mmejimaliza kisiasa kwa njia mbili,

1.Kuhujum viongozi wenzenu kwa utashi wenu wenyewe

2.kufitinishwa na Saanane bila kujua.
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,718
2,000
Mtu ana pokuja na hoja ya kusema kwamba sijawai kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya cdm kama defence si dhani kama ushahidi tosha wa kuto weza kusaliti chama!

Na huu si ushahidi ya kwamba kuwa kwakuwa mtu alishakuwa mwanachama wa chama kingine zaidi ya chadema ndio ana weza kuwa msaliti

hizi hazitoshi kuwa hoja ya kutoweza kusaliti chama.

Pengine mtu anaweza akawa hajawai kuwa mwanachama wa chama kingine lakini akatumika kusaliti chama!

Nimefurahishwa na kauli ya Mh Tundulissu!
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,230
2,000
Sasa ZZK anasubiri nini? Aanzishe yeye kuchomoka, halafu wafuatie wale masalia kama walivyofuatana kuweka threads humu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom