Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

CCM wanajikanyaga sana ..yaani mwaka huu sijui kama kuna rangi wataacha kuona
Naipenda sana Siasa hasa ya Tanzania especially nikiona Watu wanavyojiingiza mzima mzima bila ya kuweka Akiba ya Maneno
 
Mpekuzi blog
Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa hapo chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.

Tundu Lissu alijipa Kazi ya Utabiri Masikini ya Mungu

Leo Hii yupo Kitandani Ulaya anauguza Vidonda wenzie huku wapo kwenye Chereko za kukaribisha Mwaka Mpya 2018
 
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu.

Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais?

Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma.

Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala.

Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
IMG-20180110-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom