mpekuzi blog
kwa nini ukawa wameamua lowassa awe mgombea wao wa urais??..... Tundu lissu amelijibu swahi hili kwa ufasaha kabisa hapo chni:
edward lowassa anajiunga na chadema na atakuwa mgombea urais wa chadema na wa ukawa. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.
na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi chadema tulimweka kwenye orodha ya mafisadi kutokana na kuhusika kwake na kashfa ya richmond mwaka 2007.
kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: Kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.
na kwa nini washirika wetu wa ukawa nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.
kwa mara ya kwanza tunaona ccm ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua ccm na mfumo tawala ni edward lowassa. Sisi chadema tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.
tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.
kwa kuingia kwake chadema na ukawa, lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.
na lowassa ataiporomosha ccm kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:edward lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au ccm na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??
sisi chadema na ukawa tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni ccm na mfumo tawala.
tumemkaribisha edward lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza ccm na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
Vita vya Iraq, Marekani na washirika wenzake walikuwa wamepania kumtoa Sadam, na kweli walifanikiwa, lakini hawakuwa na plan ya maana juu ya Iraq baada ya kumuondoa Sadama, nini kimetokea Iraq? Vivyo hivyo Libya, nini kimetokea baada ya kumuua Gadaffi?
Turudi Tanzania, kwa miaka 20 sasa CHADEMA wamekuwa wanatueleza jinsi ufisadi unavyotuangamiza. Na ni miaka 7 saba tangu Dr Slaa ataje majina ya watu aliowaita vinara wa ufisadi. Leo hii wanatuambia kuwa wanataka kuondoa CCM kwa sababu ndiyo imelea ufisadi, lakini hapo hapo wanaanza kusajili watu wale wale waliowaita vinara wa ufisadi kutoka chama kile kile wanachokiita cha mafisadi. Tena wanasijili walioawaita vinara wa ufisadi. Hivi CHADEMA wana mpango gani ni hii nchi baada ya kuiondoa CCM? Post Sadam era or Post Gadaffi style?
Jambo la pili, Watanzania tuendelee kuamini kuwa CHADEMA wanaweza kuwamudu 'vinara wa ufisadi? Nasema hivyo kwa sababu, ndani ya wiki mbili, Lowassa ameweza kubalisha karibu kila kitu cha CHADEMA, amebadili mgombea, amebadili misingi ya waliyokuwa wanajivunia (anti ufisadi) na mbaya zaidi hata ndimi za viongozi wa CHADEMA kazibadilisha, sasa hivi wanamuita mtu shupavu, kiongozi safi! Kama amefanikiwa hayo ndani ya wiki mbili tu, kwanini tusiamini Lowassa atawapigisha deki na kuwapangia zamu ya kuosha vyombo hao CHADEMA?
fisadi lowassa hana jipya, CHADEMA nilikuwa naona wanaakili nao wameingia kwenye mtego. Mbowe sijui kahongwa tshs ngapi
Msimamo ni upi? Kuwa mpinzani wa kudumu?Nilidhani huyu ana msimamo kumbe wale wale njaa yangu jazz band. . . . .
Hizi ni feelings za kimmu haziapply kwenye politics.So far Lowassa anastahili credit
anayoyafanya kwa CHADEMA ni sawa na mtu kufanikiwa kumuoa mwanamke uliewahi kumbaka na kumuulia mumewe zamani
halafu mwanamke huyo sasa yuko in love na wewe na unapeleka posa na inakubaliwa kwa vigelegele
few people can....
we bibi hulali
Ni Lowasa.sasa nyie mnayemwona fisadi miaka yote mmemlinda sasa ndio mpaaze sauti? Mtakoma
Mkuu umekuwa kimya sanaSo far Lowassa anastahili credit
anayoyafanya kwa CHADEMA ni sawa na mtu kufanikiwa kumuoa mwanamke uliewahi kumbaka na kumuulia mumewe zamani
halafu mwanamke huyo sasa yuko in love na wewe na unapeleka posa na inakubaliwa kwa vigelegele
few people can....
Kumbe nawe unafatiliaga aya mamboNani tena huyu kafukua huku hahahahahah
hahaha, unajua jana EDO kastua wengiKumbe nawe unafatiliaga aya mambo