Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

DxR

Member
Jun 5, 2015
71
39
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu.

Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais?

Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma.

Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala.

Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA

Haya kuhusu,go Edo
 
...Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Hiyo ndio sababu ya muhimu kabisa kwa wenye matumaini ya mabadiliko. Ndugu zangu tusiipoteze hii nafasi adimu.

CCM kuwa chama pinzani, na UKAWA kushirikiana kushika nchi ndio uelekeo tunaouhitaji.
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA

Mafuriko na kimbunga vinakuja kufunua nyeti za mkwere kimbia
 
Wanaukumbi.
https://www.facebook.com/pages/Tundu-Antiphas-Lissu/510837455738370?fref=nf

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 
Loading.....................tutasikia mengi
Kamanda umekuwa mkiwa sana aisee sijui itakuaje nilivyokuwa nakusoma unavyomshambilia Lowassa.

Pole sana utafanye na wenye chama ndiyo wameishaamua.

Mtu asiyesimamia chochote basi ataanguka kwa chochote.
 
So far Lowassa anastahili credit
anayoyafanya kwa CHADEMA ni sawa na mtu kufanikiwa kumuoa mwanamke uliewahi kumbaka na kumuulia mumewe zamani
halafu mwanamke huyo sasa yuko in love na wewe na unapeleka posa na inakubaliwa kwa vigelegele
few people can....
 
Back
Top Bottom