Tundu Lissu: Dr. Slaa ni muongo, watanzania mpuuzeni. Maneno yote tatizo ni Urais

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Akihojiwa na redio station mh.Lissu anasema ameshangaa sana maneno aliyoyasema leo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Anasema Dr.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi January na mwezi April akathibitishwa na kamati kuu,

Anaendelea kusema ameshangaa Dr.Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dr. Slaa mwezi wa tano ndo alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima

Anasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.

Anasema dr. slaa asiwadanganye watanzania tatizo ni urais na mchumba wake.

Anasema ameacha siasa tangu siku ya kikao cha kamati kuu alipoandika barua ya kujiudhuru kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu?? kwanini anaendelea kutumia gari la chama la katibu mkuu na nyumba aliyonunuliwa na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote toka CHADEMA??

Sikiliza hapa chini alichosema Tundu Lissu.

Mahojiano ya Tundu Lissu na VOA Swahili

 

Attachments

  • f5530f04-c028-4ad0-8eb6-f0be30236066_original (1).mp3
    5.5 MB · Views: 36,461
Kama Dr Slaa ni muongo basi wewe Lissu ni muongo wa kutupwa naona unaizengea nafasi yake,lakini na wewe tunakuonya na domo lako chafu na ubishi wako chunga sana hao jamaa unless uko kwa kuchumia tumbo. Rais ni John Pombe Magufuli hayo matanuri yenu ya uongo yawachome wenyewe. Mnadhihirishia watu nyie sio viongozi kwa kumwambia Dr Slaa alilala nje,ni kama sasa mnawasha moto uwake vizuri nadhani Chadema busara imewapitia mbali na utajiri wa gesi umewatia wazimu. Mtaisoma tu namba mwaka huu
 
Kama Dr Slaa ni muongo basi wewe Lissu ni muongo wa kutupwa naona unaizengea nafasi yake,lakini na wewe tunakuonya na domo lako chafu na ubishi wako chunga sana hao jamaa unless uko kwa kuchumia tumbo

Mkuu ukweli ni upi hapo sasa
 
Tatizobla watanzania bado hatujajitambua....badala ya kupima analoliongea mtu kama linamashiko kwa Tanzania tuitakayo mnaleta umbea mtupu.Mtu kama Lissu kuongelea personal issue kama hizi naanza pata hisia kwamba kweli mtaalamu huyu wa sheria nchini aliwai kuwa kichaa mana kuna mtu bungeni alishawai sema ni mgonjwa wa akili.
 
Back
Top Bottom