WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 5,610
- 5,276
Upinzani labda wa wasukuma au genge la wahuni kutoka ccm.Upinzani mpya unaoanza kujipanga awamu hii pengine unaweza kuja kuwa na mchango katika kuipaisha Tanzania kiuchumi na kisiasa miaka 20 ijayo.
Huu wa kina Mbowe, Lissu, Bulaya, Mdee na Sugu biashara ndio imeshaisha, walichokifanya kiwe kizuri au kibaya kitabakia kuwa sehemu ya historia.
Wapinzani ambao baadhi yao ni wanafunzi wa vyuo vikuu na wanataaluma wengineo ndio watakaokuwa na tija kwa taifa kwa siku zijazo.
JPM alichoweza na anachoweza ni kufanyia kazi kile anachopewa kwa maana ya ilani ya uchaguzi na maagizo yake yote. Profesa Kitila Mkumbo alisema ukweli kwamba upinzani usipobadilika utapotea lakini ni ujumbe unaowahusu wale walioshindwa kuna kundi jingine litaibuka na kuja na mikakati mipya ya kisayansi.
Hilo kundi jipya la wapinzani lenye hulka mpya za kisiasa za kiupinzani ndilo litakaloisumbua CCM huko tuendako.