Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: CHADEMA na ACT-Wazalendo tumekataa kuyatambua matokeo ya Uchaguzi wala kushiriki kwenye Bunge

Nimecheka kwa nguvu, eti kashapigwa kwenye box la kura. Ni hivi, hilo utatamani maisha yako yote lakini haitakaa itokee. Sana sana itabidi Tiss, polisi, nk ndio wawe wanawezesha ccm kutangazwa washindi. Kilichofanyika kwenye box la kura wote tumekiona, imedhihirika ccm haina uwezo tena wa kushinda kwa kura halali za wananchi. Imeisha hiyo.
Mkuu! Nikikuonyaga humu kwamba Lisu wenu hatapata zaidi ya 20% na nikakupa sababu.

Nikaiona hapa unajipinda kusema ule ulikuwa aiyo uchgauzi bali uchafuzi na huku umeshiriki mwanzo mpka mwisho, nakuona hujielewi, na huna tofauti na mleta mada au member mwingine wa humu anaeitwa mmawia
 
Kwa Tanzania naona upinzani ni maneno tu ikija ishu ya vitendo ndipo unagundua upinzani wenyewe haupo.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Unapoongelea kuwa Upinzani Tanzania haupo jaribu kufikiri je kinachosababisha Upinzani ukose nguvu Tanzania je ni nini? Ni viongozi wake au wanachama wake?? Ni serikali inayoongozwa na CCM kwa kivuli cha mfumo wa vyama vingi lakini haitaki upinzani Tanzania??.
Je ni Elimu ya Watanzania walio wengi kutoelewa maaana,faida,hasara na umuhimu wa Vyama vingi?. Je vyombo vya ulinzi na usalama ni nguzo muhimu au mhimili wa kutambua mfumo wa vyama vingi au vina mashaka na mfumo huo??. Jitahidi kutathmini kwa kina kwa kuzingatia weledi wa Tanzania katika Afrika na dunia nzima ukifikiria je hii ni Tanzania inayozingatia Ahadi kumi za Tanu kama tulivyokuwa tumezoea pamoja na kuwa na imani ya Azimio la Arusha???
 
Eti na familia yako. Yaani Lissu tapeli yule akupotezee muda wako. Tangu Rais amefungua milango ya kutengeneza mabilionea wa Tanzania sisi tumemuelewa na sasa tunavyeka mapori kuanza kilimo cha umwagaliaji.Mtabaki kuwa walalamikaji na kupoteza muda kwa subiri Lissu awe rais.
Wacha tulime kazi kazi tu mengine acha wafia siasa wafie huko na kelele za kwenye mitandao.
 
Kama huu ndio msimamo uliotokana na maamuzi ya vikao vya chama, yule Mbunge aliyepo Bungeni lini atakoma kuingia kule kama Mbunge na mwanachama wa CHADEMA?

Hii kitu inaweza kwenda kuleta mtafaruku mkubwa.
Acha aende Bungeni hiyo ni haki yake kama CHADEMA haitamtambua Ubunge unaweza ukakoma na akagombea tena kupitia chama kilichompa fadhila kwa kivuli cha CHADEMA kikiwa na malengo yake watampitisha kihalali kwenye chama chao na ataendelea kuwa Mbunge,hilo halitaiathiri CHADEMA hata kidogo kuliko muda huu yeye kuwa Mbunge kama mwakilisho wa CHADEMA akiwa na meno butu.
 
Mkuu! Nikikuonyaga humu kwamba Lisu wenu hatapata zaidi ya 20% na nikakupa sababu.

Nikaiona hapa unajipinda kusema ule ulikuwa aiyo uchgauzi bali uchafuzi na huku umeshiriki mwanzo mpka mwisho, nakuona hujielewi, na huna tofauti na mleta mada au member mwingine wa humu anaeitwa mmawia

Ingekuwa kulikuwa na Uchaguzi hata Mimi ningesononeka, Ila sio kile nilichokiona kwa macho yangu. Nilihakikisha najiridhisha na mchakato mzima ili nisiwe na shaka na matokeo. Nasema hivi bila kupepesa macho, ule haukuwa Uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ila wewe kwakuwa ulichotamani kusikia ndio ulichopata, una haki ya kushangilia, lakini usitamani kujua ukweli wa kilichofanyika kama kweli hujui, maana utaishia kufedheheka.

Mimi hapa nilipo roho hainiumi maana ukweli naujua, sana sana nameishia kulipuuza rasmi zoezi la upigaji kura. Yaani uvae nguo, utembee uchi, ufahamu CCM haina uwezo tena wa kushinda kwa kura halali za wananchi, na haitakaa iwe na uwezo huo fullstop.
 
Ingekuwa kulikuwa na uchaguzi hata Mimi njngesononeka, Ila sio kile nilichokiona kwa macho yangu. Nilihakikisha najiridhisha na mchakato mzima ili nisiwe na shaka na matokeo. Nasema hivi bila kupepesa macho, ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ila ww kwakuwa ulichotamani kusikia ndio ulichopata, una haki ya kushangilia, lakini usitamani kujua ukweli wa kilichofanyika kama kweli hujui, maana utaishia kufedheheka.

Mimi hapa nilipo roho hainiumi maana ukweli naujua, sana sana nameishia kulipuuza rasmi zoezi la upigaji kura. Yaani uvae nguo, utembee uchi, ufahamu ccm haina uwezo tena wa kushinda kwa kura halali za wananchi, na haitakaa iwe na uwezo huo fullstop.
Haya bwana
 
Lissu ni tapeli ,mchumia tumbo kwa mgongo wa huruma ya Watanzania haijawahi tokea katika historia ya Siasa nchi hii.
 
Lissu ameshapoteza mvuto tokea ameondoka kwa kukimbia nahisi hana tena impact yeyote, hawezi mapambano bora angebaki mbunge mstaafu tu akawa anakosoa serikali ingetosha, viatu vya kuutaka urais bado hajaiva.
Thabo Mbeki alikimbia SA, je alipoteza mvuto? ANC kilifutwa SA, je kilikufa? Tumia akili unapotoa maoni.
 
Nawasikiliza, hawana jipya, raia tulishawakataa. Ila waache wamalizie chenchi za mabeberu maana walishapewa advance kwa kuwaahidi kuwauzia nchi.
Raia uliyewakataa ni wewe individual, Mimi sijawakataa. U CCM wako usijifanye kuwawakilisha wa Tz wote. Jiwakilishe kama wewe, usitusemee.
 
Nimemsikiliza vizuri sana Lissu. Amekwepa kabisa kusema kama CHADEMA ilishinda uchaguzi au la. Kaishia kusema CHADEMA 'haijapoteza' wala CCM 'haijashinda' uchaguzi huu. Je, huu sio ujanja ujanja wa matumizi ya lugha kisheria na kisiasa? Si kweli kwamba anakwepa kusema waziwazi kwa sababu hana ushahidi kwamba CHADEMA imeshinda Urais au Ubunge katika jimbo lolote na isitangazwe mshindi na tume ya uchaguzi? Ana ushahidi wowote (credible evidence) kwamba CCM imeiba kura? Hata pale ambapo walionesha mitandaoni kile walichoita 'ushahidi' wa kuibiwa kura hawakuchukua hatua muafaka za kisheria aidha kupitia tume ya uchaguzi au mahakama. Kwa nini?

Sote tunafahamu, vyama vya upinzani havijawahi kukiri hadharani kushindwa uchaguzi, hasa wa Uraisi, hapa nchini. Hata hivyo, katika chaguzi zilizopita, pale ambapo walifungua kesi mahakamani kuhusu kuibiwa uchaguzi wa Wabunge majimboni, pale ambapo walikuwa na ushahidi wa kutosha (credible evidence), walipewa ushindi. Kwa nini awamu hii wamekwepa kabisa kufungua kesi yoyote japo wanadai kuna ushahidi wakutosha?

Kuhusu Zitto: Maelezo kwamba vikao vya ndani ya chama vitakavyoamua kuhusu kujiunga ama kutokujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, na kitendo cha Maalim kutamka neno 'Mh. Rais' ni dalili kwamba wamekubali yaishe, na ni swala la muda tu - watapeleka jina. Pia, nyongeza ya Lissu, kwenye jibu la Zitto, kwamba 'there's always room for negotiation with the oppressor' ni dalili nyingine kwamba soon jina litapelekwa.

Jumuisho la maoni yangu: Uchaguzi umeisha na CCM kimeshinda kwa ujumla. Hata kama kuna 'irregularities' katika mchakato mzima, sio kwa kiwango cha kusababisha uchaguzi wote kwa ujumla uwe haramu au haukuwepo kama wanavyodai.

Badala ya vyama vya upinzani kujadili changamoto za uchaguzi bila hata kuwa na ushahidi wa maana, ni bora sana kujikita katika kuhangaikia jambo la msingi zaidi ambalo ni Harakati za Upatikanaji wa Katiba Mpya.
 
Unamjua Mungu au unasema tu,yeye asikilizi maombi ya mwenye dhambi na maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu,,hapo nimekupa kidogo kuhusu Mungu mkuu sasa sijajua wewe unamahanisha Mungu yupi!?
Mungu wa CCM ni mwizi, mnafiki, muuaji, mkuu wa wasiojulikana, mtekaji.
 
Mkuu Erythrocyte (Any cells that carry oyxgen around the blood system) a red blood cell, which (in humans) is typically a biconcave disc without a nucleus. Erythrocytes contain the pigment haemoglobin, which imparts the red colour to blood, and transport oxygen and carbon dioxide to and from the tissues.

Baada ya kutoa tafsiri ya kitalaamu ya utambulisho wako jukwaa lingetarajia kubeba sifa hiyo

To be precise you are wasting your precious time and resources to pose as a mouthpiece advocating a man of blasphemy. And to get it right the route you are taking is too narrow for you to walk over to the other side dof the alleyed river.

Both Hon. Seif & Jussa at different occasion responded in an interview that they are still considering the Isles revolutionary government invitation to form a GNU as prescribed in the Zanzibar constitution, so why is he emerging to speak out something tasteless to amicable leadership agreement?

It is of no doubt you are being financed to sooth the desperate expectations of the radical enthusiastic political supporters who might have been brainwashed to chant the impossible.
unajua sana kiingereza , Hongera !
 
Kwa Zitto, wewe ni kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na mpaka sasa bado mmekataa matokeo, tunajua Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ameandika barua kwa chama chako kuunda baraza au serikali ya umoja wa kitaifa na chama chako kimesema kimepokea barua na kinafanya mkutano wa ndani. Kama mnakataa matokeo kwanini mmepokea barua na kitu gani mnaenda kuzungumza?
[Kuna sehemu hili swali limejibiwa? Au ndiyo tusubiri mpaka parapanda ikilia
 
Kuna sehemu hili swali limejibiwa? Au ndiyo tusubiri mpaka parapanda ikilia...
endeleeni kuedit maandishi , ni wapi ulikoni quote nimeweka andiko hilo ? kutengeneza uongo na kuuweka JF ni kosa kwa mujibu wa sheria za jf na inaweza kukupa Ban ya milele
 

Similar Discussions

32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom