Tundu Lissu(CHADEMA), iga mfano wa mbunge Elibariki Kingu (CCM)

Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi mkoani Singida.Kutokana na upungufu wa zahanati na madawati kwenye jimbo lake ameamua kukataa posho za vikao vya bunge na kumwandikia spika azielekeze pesa hizo kwenda kutatua matatizo ya wananchi jimboni kwake singida magaribi.Jumla ya fedha za posho kwa miaka mitano ni zaidi ya millioni 200.

Jambo hili ni la kupongezwa sana kwa mbunge huyu kijana Elibariki Kingu, ameonyesha kweli anachukizwa na umasikini wa wapiga kura wake na si kupiga makelele tu with zero actions kama wabunge wengi wanavyofanya.

Tundu Lisu (chadema) ni mbunge wa mkoani singida pia na jimbo lake ni masikini kuliko majimbo yote mkoani hapa. Huduma za Maji, barabara, elimu, afya etc, ni mbovu mno jimboni kwa Lisu.

Swali kwa nini sasa Lisu asipeleke hela ya posho kutatua kero za wananchi jimboni kwake?

Pesa za posho zaidi ya million 200 unapeleka wapi na jimboni huonekani??

Kweli mbunge wa CCM Elibariki Kingu awe na uchungu kwa wananchi wake kuliko wewe Tundu Lisu mbunge wa CHADEMA?

Tundu Lissu jitafakari vinginevyo uchaguzi wa 2020 utang'oka .
Na wewe unachekesha sasa tshs 200m kwa miaka mitano unaona ni pesa ya kutatua matatizo ya jimbo? Jimbo haliwezi kuendelea kwa posho ya mbunge sahau kabisa. Wala nchi haiwezi kuendelea kwa posho za wabunge. Hizo posho kwanza wabunge wote hawastahili kulipwa kwasababu wanalipwa mishahara na kukaa mbungeni ndio kazi yao. Huwezi mlipa mfanyakazi posho kwa kufanya kazi inayomlipa mshahara. Sasa hapo ni suala la mfumo na sio issue ya mbunge mmoja mmoja kutopokea posho kwa utashi wake au kupokea
 
Lisu is for the nation and Kingu is for Singida Mang'aribi do you notice the difference? Shallow minded .
 
Huyu jamaa ndio mbunge anaejitahidi kwa vitendo ambae angalau huwa namuona kwenye media.
Ningekuwa Tume ya Uchaguzi Ningeunganisha Majimbo yote mawili ili wananchi wachague nani anawafaa naamini huyo wa CCM anawafaa zaidi. Kusije kuwa na mtu anawachelewesha raia wake kwa kichaka cha mambo ya kitaifa
Then kazi ya kitaifa afanye nani??

Lissu anakusanya kodi???
 
Huyu jamaa ndio mbunge anaejitahidi kwa vitendo ambae angalau huwa namuona kwenye media.
Ningekuwa Tume ya Uchaguzi Ningeunganisha Majimbo yote mawili ili wananchi wachague nani anawafaa naamini huyo wa CCM anawafaa zaidi. Kusije kuwa na mtu anawachelewesha raia wake kwa kichaka cha mambo ya kitaifa
Mchunguzeni kingu nyuma ya kapeti labda mseme kwa ninyi msio mjua lakini kwa wanaomjua kijana huyu hatari. Hizo zahanati na posti zake nyingi hebu fuatilieni hata vyanzo vya pesa mtajua.sio mfuko wa jimbo tu
 
Kazi ya Mbunge si kujenga wewe,Jiongeze,Tatizo hapo lumumba wengi lasaba kama akina Bashite
 
Sijawahi kumuona Lisu jimboni tangu uchaguzi uishe
18920617_136254853593666_446456989372536255_n.jpg
 
Inaonekana mtoa mada hujawahi fanya kazi, au hujui maana ya kazi na malipo. Hivi unaweza kufanya kazi ambayo haikulipi? Tuache unafiki.

Posho ni haki ya mbunge kutokana na kazi anazofanya. Maendeleo ni kazi ya serikali. Kwanini mkurugenzi au mkuu wa wilaya wasitoe posho zao kuleta maendeleo kwa watu wanaowaongoza!
 
Habari nzuri kwani anawajari wananchi, Lissu mtamuona akija kuomba kura. Kuna pesa wanapewa pia za kusaidia maendeleo ya jimbo, Lissu atakuwa anazitumia kutafutia kiki.

Hongera Mbunge
 
Nyie ndio wale mnafikiri shida za wananchi zinatatuliwa kwa sahani ya ubwabwa na kofia!
 
Habari nzuri kwani anawajari wananchi, Lissu mtamuona akija kuomba kura. Kuna pesa wanapewa pia za kusaidia maendeleo ya jimbo, Lissu atakuwa anazitumia kutafutia kiki.

Hongera Mbunge
Tatizo huna akili,mfuko wa jimbo haupo mikononi mwa mbunge pekee,kasome ng'ombe wewe
 
Mkuu umeanza hata kutamani mali ya jirani yako., imeandikwa usitamani katika amri kumi za Mungu. Hzo ni ela zake.. hata angekuwa anapata billions as long as ni fedha halali ni zake. Tuache kupenda vitonga, nenda kagombee na wewe tuone kama hyo m200 utawapa.
 
mleta mada (Naamini ni Kingu mwenyewe).. ulishalipa madeni ya wale wahindi wa Igunga, na deni la mkopo CRDB)
 
Kwa maoni yako wabunge wanaotoa misaada ni wajinga??
Kutoa msaada siyo dhambi, ni jambo la busara.Point yangu ni kwamba, msaada haulazimishwi .. na wala haipaswi kuhoji eti kwanini fulani asitoe msaada. Msaada hutolewa pale mtu anapoguswa na jambo fulani, na awe na uwezo wa kulimudu. Sio kwa kuwa unajua anapata m200 basi ndo atoe...haipo ivo mkuu...
 
Hongera sana,huyu mbunge ni mchapa kazi tangu akiwa mkuu wa wilaya
 
Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi mkoani Singida.Kutokana na upungufu wa zahanati na madawati kwenye jimbo lake ameamua kukataa posho za vikao vya bunge na kumwandikia spika azielekeze pesa hizo kwenda kutatua matatizo ya wananchi jimboni kwake singida magaribi.Jumla ya fedha za posho kwa miaka mitano ni zaidi ya millioni 200.

Jambo hili ni la kupongezwa sana kwa mbunge huyu kijana Elibariki Kingu, ameonyesha kweli anachukizwa na umasikini wa wapiga kura wake na si kupiga makelele tu with zero actions kama wabunge wengi wanavyofanya.

Tundu Lisu (chadema) ni mbunge wa mkoani singida pia na jimbo lake ni masikini kuliko majimbo yote mkoani hapa. Huduma za Maji, barabara, elimu, afya etc, ni mbovu mno jimboni kwa Lisu.

Swali kwa nini sasa Lisu asipeleke hela ya posho kutatua kero za wananchi jimboni kwake?

Pesa za posho zaidi ya million 200 unapeleka wapi na jimboni huonekani??

Kweli mbunge wa CCM Elibariki Kingu awe na uchungu kwa wananchi wake kuliko wewe Tundu Lisu mbunge wa CHADEMA?

Tundu Lissu jitafakari vinginevyo uchaguzi wa 2020 utang'oka .
Aige mawazo ya kijuha hayo ya wAbunge wote wa magamba mjengoni sawa na kichwa kimoja cha Lissu jipange upya aiseeee
 
Back
Top Bottom