Tundu Lissu(CHADEMA), iga mfano wa mbunge Elibariki Kingu (CCM)

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
3,802
2,000
Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi mkoani Singida.Kutokana na upungufu wa zahanati na madawati kwenye jimbo lake ameamua kukataa posho za vikao vya bunge na kumwandikia spika azielekeze pesa hizo kwenda kutatua matatizo ya wananchi jimboni kwake singida magaribi.Jumla ya fedha za posho kwa miaka mitano ni zaidi ya millioni 200.

Jambo hili ni la kupongezwa sana kwa mbunge huyu kijana Elibariki Kingu, ameonyesha kweli anachukizwa na umasikini wa wapiga kura wake na si kupiga makelele tu with zero actions kama wabunge wengi wanavyofanya.

Tundu Lisu (chadema) ni mbunge wa mkoani singida pia na jimbo lake ni masikini kuliko majimbo yote mkoani hapa. Huduma za Maji, barabara, elimu, afya etc, ni mbovu mno jimboni kwa Lisu.

Swali kwa nini sasa Lisu asipeleke hela ya posho kutatua kero za wananchi jimboni kwake?

Pesa za posho zaidi ya million 200 unapeleka wapi na jimboni huonekani??

Kweli mbunge wa CCM Elibariki Kingu awe na uchungu kwa wananchi wake kuliko wewe Tundu Lisu mbunge wa CHADEMA?

Tundu Lissu jitafakari vinginevyo uchaguzi wa 2020 utang'oka .
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,704
2,000
Nonsense, huwezi maliza matatizo kwa petty things of that nature, labda kwa wasiojielewa. You have to mobilize the people themselves for self help! Una hela gani za kuwatatulia matatizo yao? Labda kofia, kanga na fulana! Posho, nonsense!
 
usatrumpjr

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,218
2,000
uyo kingu kuna kifungu kina mbana yy kufanya hayo?serikali kuu iko wapi km wabunge wakifanya izo kazi?alieweka posho kwa wabunge alikua na lengo ilo?mpeni mbunge mamlaka ya kukusanya kodi jimboni kwake ili aweze tatua hizo changamoto
 
bhulalo

Member
Mar 21, 2017
14
45
. Unajua kazi ya kupeleka huduma za afya, barazara ni za serikali na si za Mbunge. Kazi ya mbunge kwa wapiga kura wake ni kusimamia bajeti iliyoainishwa na serikali ktk jimbo lake iweze kufika kwa wakati. Na wakati wa implimentation, mbunge atashirikiana na wananchi wake. Au nakosea? Kunyima watu posho zako kwa lengo la kupana matumizi ni uzandiki, kujipendekeza, idhamu ya uoga , kusafisha kikombe nje kumbe ndani kimeoza na kuna funza. Lisu ana dependants wangapi wanaomtegemea kiuchumi ? Atakaaje posho inayomsaidia kuendesha maisha yake. Tafuta hoja nyingine upost tuchangie hapo umepost hewa.
 
Chloroquine

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
209
225
Kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana una hakika 100% kuwa kahongwa na watu wa madini ngoja waje wenyewe ukatoe ushahidi ili kama ni kweli basi aelekeze fedha hizo jimboni.
 
Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,174
2,000
Kiongozi hutakiwi kutumia malipo ya ujira wako kuwahudumia wananchi wako bali unatakiwa kusimamia kwa dhati wapate au wapewe yale mahitaji yao kutoka sehemu husika kama serikali.Kwa hiyo kama jimbo au majimbo mengi hayana mahitaji muhimu ya wananchi ni kutokana na umasikini wa nchi yetu na siyo wabunge au viongozi kutumia sehemu ya malipo yao kuwahudumia bali ni kuishauri serikali jinsi ya kuongeza mapato ili iweze kuwahudumia wananchi wote kwa ujumla.
Mfano;Huwezi kukabidhiwa shirika au taasisi kama CEO then utumie baadhi ya malipo yako kulipa wafanyakzi mahitaji yako bado hayatapokelewa kama uhitaji wao na siyo sahihi bali unatakiwa kusimamia kilichopo na kutengeza njia za kuongeza fursa na kuongeza mapato ili wafanyakzai waweze kufaidika
 
Denis denny

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
5,789
2,000
Haya kamwambie bwana yako Kingu Tundu Lisu haombi kwa Spika afanye kitu fulani bali anafanya mwenyewe
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,171
2,000
Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi mkoani Singida.Kutokana na upungufu wa zahanati na madawati kwenye jimbo lake ameamua kukataa posho za vikao vya bunge na kumwandikia spika azielekeze pesa hizo kwenda kutatua matatizo ya wananchi jimboni kwake singida magaribi.Jumla ya fedha za posho kwa miaka mitano ni zaidi ya millioni 200.

Jambo hili ni la kupongezwa sana kwa mbunge huyu kijana Elibariki Kingu, ameonyesha kweli anachukizwa na umasikini wa wapiga kura wake na si kupiga makelele tu with zero actions kama wabunge wengi wanavyofanya.

Tundu Lisu (chadema) ni mbunge wa mkoani singida pia na jimbo lake ni masikini kuliko majimbo yote mkoani hapa. Huduma za Maji, barabara, elimu, afya etc, ni mbovu mno jimboni kwa Lisu.

Swali kwa nini sasa Lisu asipeleke hela ya posho kutatua kero za wananchi jimboni kwake?

Hivi karibuni Lissu amehongwa na mafisadi wa madini na kuanza kuwatetea hadharani bila aibu. Sasa Tundu Lisu ukichukua hela uliyohongwa na mafisadi uakajumlisha na ile ya posho za bunge ukazipeleka kutatua tatizo la maji jimboni kwako huoni kuwa ni jambo la maana sana?

Pesa za posho zaidi ya million 200 unapeleka wapi na jimboni huonekani??

Kweli mbunge wa CCM Elibariki Kingu awe na uchungu kwa wananchi wake kuliko wewe Tundu Lisu mbunge wa CHADEMA?

Tundu Lissu jitafakari vinginevyo uchaguzi wa 2020 utang'oka .
Hakuna kitu kibaya kama KUMHUSISHA lISU NI VITU VYA AJABU AJABU
 
Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
380
1,000
Suala sio kuiga je hajafanya ipasavyo jimbo ni kwake? Je, wananchi wake wanaona hajafanya au ni wananchi wa majimbo mengine ndio wanapiga kelele tu
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
32,571
2,000
Jimbo la Elibarick limejaa nyumba za tembe, ndiyo maendeleo hayo? mpuuzi kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom