Tundu Lissu: CHADEMA haijapokea ruzuku hata senti 5, Baraza Kuu kukaa Machi au Aprili

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,606
2,000
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Ndg Tundu Lissu amesema, chama hakijapokea ruzuku yeyote toka serikalini na kama kuna mtu ana ushahidi kuwa wamepokea basi auonyeshe, kaongeza kusema, fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa ni chanzo kimoja tu cha mapato ya chama, kuna vyama havina ruzuku lakini vinaendesha shughuli zao. Chadema kina wanachama 6,700,000 hao wanachama ndio watakaoendesha shughuli za chama.

"Hatujapokea ruzuku yoyote. Katibu Mkuu wa @ChademaTz aliandikiwa barua na Msajili wa Vyama vya siasa aende kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ruzuku. Katibu mkuu alikataa, kama wanasema tumepokea ruzuku, waoneshe ni sehemu gani tumepokea na kusaini" Ndg. @TunduALissu.

Kuhusu wanachama 19 waasi waliofukuzwa Lissu kasema, kazi ya Kamati Kuu ni kusimamia katiba na misingi ya chama na wala sio kusimamia kanuni za Bunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la aliyewapokea.

"Kamati Kuu ya @ChademaTz imeketi na kuamua kuwa wabunge 19 ambao wameasi na kukiuka maamuzi ya chama tuliwafukuza uanachama, kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu tangu 1965 tulipoingia rasmi katika mfumo wa chama kimoja mpaka leo, Mbunge akipoteza uanachama wa chama cha siasa anapoteza na ubunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la wanaowapokea na kuwapa fedha za umma wakati si wabunge”.

"Ni kweli wabunge 19 tuliowafukuza wamekata rufaa. Kwenye kikao cha kamati kuu wiki iliyopita tumefanya maamuzi kuwa, kikao cha Baraza Kuu kitaitishwa kati ya mwezi Machi na Aprili, hatuwezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu eti tu kwa ajili ya kuwasikiliza hao waasi" @TunduALissu.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,852
2,000
Angeongea Mbowe au Mnyika waweza kuamini CHADEMA haijapokea ruzuku, Ila mtu yupo Ulaya tena kwenye LOCKDOWN aje kujua ya account za chama bongo!? Au wanacheza na akili za NYUMBU wa ufipa wakamtumia Lissu kuwatuliza. Mchaga kwenye shilingi hajawahi kuniangusha.
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Mzalendo aliyekimbia nchi yake?

Baada ya kushambuliwa na watu inaosemekana hawajulikani na CCTV camera zilizonasa tukio, zikaondolewa na watu wanaojulikana halafu upelelezi ukakwama kisa aliyekua mgonjwa hayumo nchini, nadhani kwa mazingira hayo ndiyo maana akaona akae sehemu salama zaidi kuliko nchini ambako wewe na baadhi yenu mko salama na hamna sababu za kuondoka.

Au mkuu na wewe umewahi pigwa risasi japo mbili tu humuhumu nchini, halafu upelelezi wa tukio haukufanyika na umeamua kukaa salama salmini japo unapokea vitisho vya kuuawa na TCRA wala hawahangaiki na wale wanaokutishia?
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,803
2,000
Kiukweli Chadema kwa hili walipaswa kubariki mapema tu na kushukuru kupata bahati walau kwa lugha yeyote hisani, upendeleo hao covid19. Bado kama taifa tunayo safari ndefu kudai katiba bora sambamba na tume huru.
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Angeongea Mbowe au Mnyika waweza kuamini CHADEMA haijapokea ruzuku, Ila mtu yupo ulaya tena kwenye LOCKDOWN aje kujua ya account za chama bongo!?.. au wanacheza na akili za NYUMBU wa ufipa wakamtumia Lissu kuwatuliza. Mchaga kwenye shilingi hajawahi kuniangusha.
Makamu mwenyekiti wa chama anajua taarifa nyingi kuliko mwanachama wa kawaida, bila shaka kuna mawasiliano miongoni mwao viongozi waandamizi wa chama,
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
6,548
2,000
Baada ya kushambuliwa na watu inaosemekana hawajulikani,na CCTV camera zilizonasa tukio,zikaondolewa na watu wanaojulikana halafu upelelezi ukakwama kisa aliyekua mgonjwa hayumo nchini,nadhani kwa mazingira hayo,ndiyomaana akaona akae sehemu salama zaidi kuliko nchini ambako wewe na baadhi yenu mko salama na hamna sababu za kuondoka....
Mkuu umesoma Historia? Unajua kwanini Nelson Mandela alipendwa sana Afrika Kusini? Unajua kwanini Jacob Zuma alipendwa sana kuliko "Mtangulizi" wake Thabo Mbeki? Ukiwa na hayo majibu, tutaongea!!!!!
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,123
2,000
Kiukweli CDM kwa hili walipaswa kubariki mapema tu na kushukuru kupata bahati walau kwa lugha yeyote hisani, upendeleo hao covid19. Bado kama taifa tunayo safari ndefu kudai katiba bora sambamba na tume huru.
Unataka kumdanganya nani hapa JF?
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Kiukweli CDM kwa hili walipaswa kubariki mapema tu na kushukuru kupata bahati walau kwa lugha yeyote hisani, upendeleo hao covid19. Bado kama taifa tunayo safari ndefu kudai katiba bora sambamba na tume huru.
Washukuru kivipi?
Yaani wao wanajua uchaguzi ulikua kituko, halafu wapewe viti hivyo, washukuru?
Wataonekana ni wajinga sana hao CHADEMA.
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Mkuu umesoma Historia? Unajua kwanini Nelson Mandela alipendwa sana Afrika Kusini? Unajua kwanini Jacob Zuma alipendwa sana kuliko "Mtangulizi" wake Thabo Mbeki? Ukiwa na hayo majibu, tutaongea!!!!!
Kwa Mandela najua moja ya sababu ni moyo wake wa kusamehe kwa maslahi mapana ya nchi yake na vilevile yeye ni moja ya watu waliofanikisha uhuru wa S.A kupatikana.

Huyo Zuma sijajua kama alipendwa kwa jinsi alivyoshutumiwa kufanya mambo yanayosemekana ya hovyohovyo.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,852
2,000
Makamu mwenyekiti wa chama,anajua taarifa nyingi kuliko mwanachama wa kawaida,bilashaka kuna mawasiliano miongoni mwao viongozi waandamizi wa chama,
Mkuu hutamuona Mbowe wala Mnyika anaongelea hii ishu ya akina Mdee. Tatizo mmefungwa na mahaba ya chama hamko tayari kuangalia upande mwingine wa shilingi. Nasisitiza Mchaga hajawahi kuniangusha kwenye shilingi. Kuna mambo mkijakiyajua huko mbeleni mtajiona wajinga sana. CCM na CDM ni walewale tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom