Makamu Mkiti wa CHADEMA akiongea leo kwenye Forum ya Maria Space inayoongozwa na Mwanaharakati Maria Sarungi iliyoshirikisha watu zaidi ya elfu 6 duniani kote, amesema,
“Kama makundi mengine ya vyama vya kiraia, vyama vya siasa, NGOs, viongozi wa dini wanasita au wanaogopa dola kujitokeza, Chadema haitawasubiri hadi uoga wao uwaishe, Chadema itaongoza mapambano”.
Akaongeza kusema, suala la katiba ni la kila mtu kama mtu au vyama vingine vinaona katiba siyo muhimu kwao Chadema haitavilazimisha atakayeona umuhimu na aje, vyama vyenye mtazamo sawa na CCM vinaweza kuungana na CCM kupinga Katiba Mpya baadaye wananchi watakuja kulinganisha ni upande upi wenye hoja.