Tundu Lissu: CCM imeanza kucheza rafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu: CCM imeanza kucheza rafu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, May 21, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tundu Lissu: CCM imeanza kucheza rafu

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kimekishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeanza mkakati wa kununua shahada za kupigia kura za vijana wanaoonekana kushabikia vyama vya upinzani katika mikoa yote nchini.

  Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu, alisema jana kuwa viongozi na makada wa chama hicho kuanzia ngazi za mashina na matawi wamekuwa wakikusanya taarifa za wananchi waliojiandikisha karika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Alidai kuwa katika kutekeleza mkakati huo, makada hao wa CCM wanashirikiana na maofisa watendaji wa kata na vijiji ambao katika uchaguzi mkuu watakuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi.

  Alisema Chadema imepata ushahidi unaoonyesha kuwa sensa ya wapiga kura inayofanywa na CCM ni maandalizi ya kuharibu uchaguzi wa mwaka huu kwa kutoa rushwa kwa wapiga kura wenye mwelekeo wa kuviunga mkono vyama vya upinzani.

  Lissu alisema Jumamosi iliyopita, wanachama wa Chadema wa kijiji cha Nkhoiree, kata ya Ihanja Jimbo jipya la Singida Magharibi kulimkamata kada mmoja wa CCM akiwa katika zoezi la kuchukua taarifa za wapiga kura.

  Alisema katika purukushani za kumkamata, kada huyo alifanikiwa kukimbia na kutoroka, lakini wanachama na wafuasi wa Chadema walifanikiwa kukamata nyaraka alizokuwa nazo.

  Alisema nyaraka alizokamatwa nazo ni muhtasari wa kikao cha CCM kata ya Ihanja ambayo inawataja pia Mwenyekiti wa kata na Katibu wa kata hiyo ya Ihanja.

  Lissu alisema ajenda namba 5 ya muhtasari huo inahusu maazimio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoelekeza makatibu wote wa matawi yote ya CCM wafanye sensa ya wapiga kura wote wa vyama vya upinzani kujua wako wangapi hasa vijana wa rika la kati ili kupata idadi yao Tanzania nzima.

  Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hizza, alipoulizwa alisema hizo ni taarifa za uongo kwani CCM inachofanya ni kuhakiki wanachama wake na si kuhangaika na wapinzani.

  Alisema zoezi hilo ni la kawaida na limekuwa likifanyika miaka mingi iliyopita hivyo hakuna kitu kipya.

  Alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha kila mwanachama wa chama hicho amejiandikisha katika daftari la wapiga kura.

  "Tunahakikisha kila mwanachama wetu anajiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi apige kura na ambaye hatafanya hivyo hataruhusiwa kupiga kura za maoni ndani ya chama," alisema Tambwe.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Katika hili ndipo CCM hufanikiwa kuvipiku vyama vcya upinzani katika chaguzi kwa njia za haramu kabisa. Nakumbuka mwaka 2005 nilizozana na kumfukuza kumikumi mmoja wa CCM aliyekuja nyumbani kwangu kutaka kufanya kazi ya kuorodhesha wapiga kura.


  Nilimweleza kazi hiyo siyo yake, na kama anataka kujua idadi ya wanachama wa CCM katika mtaa wake si anayo list tayari kwa kuwa yeye alikuwa ni kumikumi wao kwa miaka zaidi ya sita?

  Baadaye niliambiwa na wengine kuwa kazi hiyo ya kuorodhesha waliojiandikiusha – wenyewe wanaita kuhakiki wanachama wa CCm – ilikuwa inaendlea kila mahali katika jijini Dar na sehemu nyingine nchini, na kwamba kila kada wa CCM akiorodhjesha majina zaidi ya 50 hulipwa kati ya 50,000/-! Na 100,000/-! (Ndiyo maana waliiba Benki Kuu!)

  Sikulitia maanani sana suala hilo wakati ule, lakini siku chache kabla ya uchajaguzi wakati orodha za wapiga kura zilipowekwa hadharani, jamaa wengi, hasa wapinzani (pamoja nami) hatukuamo katika orodha. Tulikuwa tunaulizana (kwani wanachama wa chama chetu cha upinzani tulikuwa tunajijua katika mtaa wetu): Inakuaje wapinzani tu ndiyo majina yao hayamo?

  Tulijaribu kuwasiliana na watu wa Tume katika ofisi yao kuu, lakini nako tulikuta mamia ya watu wanalalmika hivyo hivyo, wengi wao wakijitambulisha wao kwa wao kuwa ni wanachama wa upinzani.

  Basi mradi tulizungushwa tu na NEC – baadaye tukaambiwa tujiorodheshe kwa kutaja jimbo, kata na kituo tulikojiandikisha, na kuambiwa mambo yatarekebishwa.

  Kwa mshangao wetu hayakurekebishwa, kwani siku ya uchaguzi, majhina yalikuwa hayamo, na vurugu kubwa zilizuka hapa Dar katika vituo vingi kutokana na majina ya wapiga kura kutoonekana.

  Baadaye nilitafakari sana: Inakuwaje majina mengi ambayo hayakuonekana yalikuwa kutoka vyama vya upinzani tu? Ilielezwa, kwa mfano, Jimbo la Temeke peke yake zaidi ya watu laki moja (1,000,000) hayakuonekana katika vituo mbali mbali vya kupiga kura.

  Nikapata jibu: CCM ilishirikiana na Tume ya Uchaguizi (NEC). Ni hawa hawa makada wa CCM waliokuwa wanajidai kuhakiki wapiga kura wao (kwa kuwaorodhesha). Hayo majina (ya wana-CCM), baada ya kuwasilishwa na kupitia ngazi mbali mbali za mfumo wa chama hicho – yalifika NEC, ambao walikuwa wameagizwa kurejea kwenye daftari la kila kituo na kuyaondoa majina ya wale siyo wana-CCm (kutoka kila orodha ya vituo) na hivyo kubakiza majina ya wale ya wana-CCM. Yumkini majina machache ya wapinzani yalibakizwa kupotezesha lengo!

  Baadaye iligundulika kuwa NEC hawakuyafuta kabisa majina ya wapinzani bali waliyahamishia kwenye vituo vingine vya mbali ili kuwahangaisha tu siku ya kupiga kura. Kuna baadhi ya wapinzani walinieleza baadaye (baada ya uchaguzi) kuwa majina yao yalionekana katika orodha za vituo vingine vya mbali.

  Nikaitafakari hii: Hivi kweli hii inawezekana? NEC kushirikmiana na CCM kiasi hicho?

  Nikaona inawezekana kabisa, ikiwa boT walisahirikiana na makada wa CCM kuibia wananchi hela zao – hili pia lawezekana. Na ndiyo maana CCM haitaki NEC iliyo huru.

  Angalizo kwa viongozi wa upinzani: waliangalie sana suala hili. Tena walivalie njuga sana, kwani NEC haina ubavu wa kuifanya uchunguzi wa dhati na kukataza. Inasemekana aina hii ya uibaji wa kura ulitumika Kenya mwaka 1992 na 1997 na Ethiopia mwaka 2005.

  Hapa kwetu mwaka 2000 walitumia njia ya kufungua vituo B karibu na vituo rasmi vya wapiga kura ambavyo vilitumika kutumbukiza kura za bandia. Mwaka huu, kama siyo kurudia uibaji wa 2005, sijui watabuni njia ipi watu hawa!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilikuwa najiuliza vipi majina ya wanaupinzani tu ndiyo hayakuwa yanaonekana kwenye orodha za wapiga kura? Kumbe jibu nadhani ni hilo, nakushukuru sana Kafiribangi kwa jutoa hii explanation ambayoi inaonekana kuridhisha. Wanahakiki, wanahakiki nini? Kwani kupiga kura ni siri ya mtu, mwanachadema anaweza kumpigia kura mgombea wa CCM, na kinyume chake, mradi iwapo anaonekana anafaa! Kwa nini CCM inapenda sana kuwaburuza wananchi?

  Mimi ntakubali iwapo wagombea watapita nyumba hadi nyumba kuomba kura, lakini siyo kuanza kuorodhesha wapiga kura, amnbayo ni kazi ya Tume pekee. na inafaa Tume iwakemee CCM kwa kuingilia kazi yao.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  NEC inawajibika katika kulikataza hili, maana bila shaka CCM inafaidika na iunavyofanya. Lakini kama NEc inashirikiana na CCM katika hujuma hii, basi haiwezi kusema chochote kwani ipo kwa kuhakikisha ushindi wa CCM!

  NEC ina tatizo kubwa la credibility, na sidhani kama wanalitambua hilo. It's always blantantly pro-CCM. nakumbuka katika uchaguzi wa 2005, kipeperushi kimoja kilimwonyesha mgombea wa Chadema, Mbowe huku nyuma yake kuna bendera ya taifa. Mwenyekiti wa NEC, Judge Makame alishangaza wengi alipokemea kipeperushi hicho -- hasa eti kwa nini kilikuwa na bendera ya taifa! Ebo! Bendera ya taifa inakatazwa kwenye kampeni? Nchi nyingi bendera ya taifa hutumika katika shughuli za kampeni kuionyesha umoja wa kitaifa, pamoja na mgawanyiko wa kisiasa. Nadhani Judge Makame aligundua kosa lake na hakulifuatilia sana.

  Lakini hili la makada wa CCM kuorodhesha wapiga kura linatakiwa kukatazwa kabisaa. nakumbuka katika uchaguzi mdogo wa Busanda mwaka juzi CUF waliilamamikia sana Tume kwa tabia hii ya CCM. Kinachotakiwa ni kwa upinzani kulipigia kelele sana katika mikutano yao na katika vyombo vya habari.
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Bwana Lisu madam umejiingiza kwenye siasa acha kulia lia gangamala, fanya kampeni vizuri, hakikisha wanachama wa chama chako wanajiandikisha na kupiga kura.
  Mimi ninadhani siyo jambo baya kwa vyama vyote vya siasa kufanya hivyo sababu kubwa ni kuwa baada ya kuwahamasisha wanachama [kivyama] inakuwa ni busara kufahamu wanachama wangapi wamejiandikisha na baada ya hapo ni kuhamisisha wanachama kujitokeza kupiga kura[ kama wawakilishi wa vyama watukuwa na coordination nzuri kati yao inakuwa ni rahisi kwao kujuwa wanachama wangapi wamepiga kura. CUF ni hodari sana katika uratibu wa namna hii.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Alivyosema mchangiaji (Reply No 2 hapo juu) ni sahihi kabisa. Hili suala la kuorodhesha wapiga kura ndiyo chanzo cha rushwa (takrima) katika uchaguzi, na ndiyo maana nyie CCM mnapenda kulin'gang'ania kwa sababu chama chenu kina mapesa tele yanayoibwa kutoka kwa wananchi kama vile BoT. Nyie hamuaminiki katika uchaguzi: Mna-control kila kitu, Tume, polisi na hata wasimamizi wa vituo huwa ni ma-DED wa halmashauri ambao huteuliwa na Rais (mwenyekiti wa CCM) na ambao bila shaka yoyote ni lazima awe mwanachama wa CCM.


  Pamoja na hayo yote mnaongezea na hili la 'kuoredhesha' wapiga kura wenu - hiyo ni tamaa ya fisi. Tamaa yenu hiyo itakuja kuwaumbua siku moja. Kwanza tunashangaa kwa nini hadi sasa chama chenu hakijajibu hoja kuu ya wapinzani kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) siyo huru kabisa? Likizungumnzwa hilo mnauchuna tu kama vile mabubu!
   
 7. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hard Hitter or rather hard hater
  Naona umenisajili ccm kutokana na ushauri wangu kwa Tundu Lisu tayari umeniwekea stamp.
  Hivi unafahamu kuwa "On a clear day one can see forever" Tatizo la watu kama nyinyi mnapenda kuwa "mono thinkers' wakati tunatakiwa tuwe multi dimensional thinkers" Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa wala kuegemea chama chochote kile na hali hii inanifanya nione mambo more clearly kuliko ningekuwa mwanachama. Tuzungumze hoja kwa undani wake. Hivi vyama vya siasa vinaposema kuwa vimeibiwa kura na ccm huwa inatumia vigezo vipi???[ kwenye vituo vya kura kuna maajent wa vyama, ballot box transparent na kura zinahisabiwa hapo hapo kituoni mbele ya maajenti wa vyama. Kama vyama vya upinzani havina data za wanachama wao waliojiandikisha na waliopiga kura[baada ya uhamasishaji] mtajuaje idadi ya wanachama waliopiga kura ??? kama alivyonena Mao tse tung kuwa bila "data" huna haki ya kusema [kulalamika] na kama mtakuwa mnaendelea kulalamika tuu haitawasaidia wala haitaisaidia Tanzania.
   
 8. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Tundu Lisu analia nini? Amesahau yeye ndiye aliyemtetea Dr Slaa wakati wa petition dhidi yake na walala-
  mikaji walionyesha overwhelming ushahidi mahakamani wa jinsi hao watendaji wa kata ambao ni wateule wa CHADEMA
  wilaya ya Karatu walivyovuruga na kumsaidia Slaa? Sawa hukumu ilienda upande wao. Lakini JAJI yule
  alipokuwa naye UDSM alikuwa mwanaharakati mwenzie. Siasa ni kuzidiana ujanja. Hakuna habari ya fair
  play. Ndio maana Karatu CCM inabanwa sana na CHADEMA. Hio ndiyo habari yenyewe.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  May 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  maneno yako ya hovyo yamenilazimisha kusign leo, kwahiyo kusema hayo sio sehemu ya siasa, siasa ni nini basi ? hoja yako inawalakini . kwahiyo unampangia Lissu chakufanya katika siasa.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  May 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  sasa kama mahakama iliona hakukua na Hatia inakuwaje wewe ututhibitishie tofauti na vile Jaji alivyoiacha sheria ichukue mkondo.
   
 11. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nguvumali
  Kama umesoma vizuri utafahamu kuwa ule ulikuwa ushauri[siyyo lazima autumie] kama vile nyinyi mnavyotoa ushauri kwenye issue nyingine ambazo mnamshauri hata JK humu humu ndani ya JF. Sasa mimi kufanya hivyo kwa bw Lisu imekuwa nongwa?????

   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Mkuu acha Ushabiki Maandazi, inaonekana ile Kesi hukuifuatilia kabiasa, No research no right to speak
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hebu pitia hii topic Mkuu halafu ndio uje na hiyo maneno yako Mbofumbofu

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/7775-kesi-ya-dr-slaa-ushahidi-ni-wa-kutungwa.html
   
 14. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  RUshwa, Urasimu hauishi na watu wasilalamike kwani ndo chanzo cha kuharibu kura asante
   
 15. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #15
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Duhhh! Ipo kazi!
   
 16. p

  philly d New Member

  #16
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio kawaida yao hao CCM ila imefika wakati sasa tuwakomeshe
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hata hapa Dar es Salaamu zoezi hili linafanyika. Majuzi(Jumamosi) kiongozi mmoja wa shina la CCM alikuja nyumbani kwangu akitaka nyumba nzima tuandike majina na namba za vitambulisho vya mpiga kura. Niliistukia janja yao na kumwambia kwenye nyumba yangu hakuna aliyejiandikisha....akaondoka kimya kimya! Nilikuwa namsubiri aniulize kwa nini hatujajiandikisha nianze kumpa 'vidonge' vyake!
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu Abunuwasi ametoka wapi? Angalia jina lake! Kama yeye vile! Unajua Tz tukiwa na watu kama kina abunuwasi nchi inauzwa!
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mauzauza OOOPS Sorry Mageuzi
  You are hardly 2 months old and have started with with 'people labelling' Iwonder what sort of a person u will be when u grow up.
  This is a Forum for those who dare speak their mind freely without fear. Would you rather i become HMV[His masters Voice-robot]?
  Bro, that Era is long gone and will never come back.
  Hivi unafahamu kuwa " Diverse thinking is fertilizer of mind".
  Ushauri wangu kwako ni kuwa kama huna cha kuchangia basi fanya tafakuri za michango maana humu ndani ni chuo na kuna nguli wengi ambao wanatuendeleza kifikra.
  ingawa kuna wakati hatukubaliani na tafakuri hizo, lakini bado zina kuwa tafakuri za maana sana kwa wenye kutambua.
  Long live Tanzania Long live JF
   
Loading...