Tundu Lissu: Background murua kwa ushahidi wako

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,468
Nakumbuka Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Bwana Yusufu Makamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alisema kuwa karibu wagombea wote wa CCM - madiwani na wabunge (sasa sijui kwa nini akusema na Urais) walitoa rushwa ila walizidiana kiwango tu. Sasa hawa watoa rushwa watashindwaje kupokea rushwa ili kurudisha walichotoa? Hii ni ishara tosha kuwa wabunge walio wengi ndani ya CCM ni vinara wa kutoa na kupokea hiyo rushwa. Ukiongea na wagombea wengi wanakiri kufanya hivyo!!

Corruption report ya 2009 (angalia attachment ya vol. 1) ambayo TAKUKURU wamegoma kuitoa hadharani inaonesha kuwa karibu sekta zote ni vinara wa rushwa. rushwa ndogo ndogo imeshamiri kwenye household level na ile kubwa kwa big shots.

Mhe. Tundu Lissu tumia reports hizi muhimu kama background ya ushahidi wako ili kuwakaanga vizuri akina Ole Sendeka wasiojua katiba wala kanuni za Bunge kwa kuomba mwaongozo kwa Spika wa kutaka kumpeleka Lissu mahakamani.

Mwanakijiji mimi ninapungukiwa na volume 3 ya hii report ya corruption ya 2009, tafadhari, je waweza kutuwekea kwa muda au kututumia kwenye e-mail zetu privately kwani ulisema ni kubwa sana!!
 
Mkuu hiyo attachment Vol. 1 ya report nayo haipo! tunakuomba utuwekee jamvini mkuu
 
Back
Top Bottom