Tundu Lissu: Baadhi ya wateule wa Rais Magufuli ambao, kwa kauli yake mwenyewe, hawako 'nyutro' ni hawa wafuatao

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
(1) Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Serikali za Mitaa ambao, kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, ni wasimamizi wa uchaguzi.

Ukiachia Wakurugenzi wa Majiji, Rais hana mamlaka kisheria ya kuteua Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Serikali za Mitaa.

Hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, ni mamlaka ya Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa.

Na kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, Wakurugenzi hawa ni 'watu wanaohusika na uchaguzi' na kwa hiyo ni marufuku kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kwa maneno mengine, wote hawa wanatakiwa na Katiba kuwa 'nyutro.'

(2) Wakuu wote wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, Wakuu wa kamandi au vikosi au taasisi nyingine za kijeshi na maafisa wengine wa kijeshi wanaopewa kamisheni zao na Rais. .

Wanajeshi wote hawa, kama ilivyo kwa wanajeshi wengine wote, nao wamekatazwa na Katiba ya nchi yetu kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Nao wanatakiwa na Katiba kuwa 'nyutro.'

(3) Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi (TISS) na Naibu wake.

TISS imepigwa marufuku na Sheria yake mahsusi kufanya ujasusi (surveillance) dhidi ya watu wanaotumia haki yao ya kikatiba ya kuendesha shughuli za kisiasa.

Na wala TISS haina mamlaka ya kipolisi ya kukamata wahalifu wa aina yoyote ile. .

Lakini nani asiyejua mambo yanayofanywa na ma-DSO na ma-RSO mikoani Na wilayani dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM na viongozi wake???

(4) Jaji Mkuu, Majaji wa Rufani, Jaji Kiongozi na majaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama Kuu na wasajili wengine wote wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama Kuu na Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Wote hawa wamekatazwa na Katiba ya nchi, Sheria mahsusi pamoja na mila na desturi za kimahakama kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Nao wanatakiwa kuwa 'nyutro.' . . (5) Mwenyekiti na makamishna wote wa Tume ya Uchaguzi pamoja Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Kama ilivyo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa, Mwenyekiti na makamishna wa NEC nao ni 'watu wanaohusika na uchaguzi' na wamekatazwa na Katiba kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Kwa kauli ya Rais Magufuli mwenyewe, wote niliowataja sio 'nyutro', kwa sababu wameteuliwa na yeye Mwenyekiti wa CCM!!!

Kuna siku niliwahi kusema hadharani kwenye press conference fulani, 'tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea....' Nilikamatwa na kulazwa mahabusu ya Central siku moja au mbili baadae.

Nilipoandika maelezo polisi kuhusu kauli yangu hiyo, nilipelekwa mahakamani Kisutu kesho yake na kushtakiwa kwa kosa la kueneza chuki za kidini wakati wa kampeni za uchaguzi wa marudio Dimani Zanzibar!!!!

Ama kweli wapinzani tutapata tabu sana!!!!!!
 
Ina maana haya hakuwa anayajua? Nadhani labda alikuwa anawakumbusha kuwa licha ya unyutro huo lakini watekeleze ilani ya chama kilicho madarakani.!
 
saluti ya mwegelo !
kkkkkkk !
IMG_20180804_084527.JPG
 
Anyone to correct me please!
Was the president's statement not meant for the newly appointed DC's and RC's and RAS?
Watu ambao kikatiba wanateuliwa ili kumsaidia yy mwenyewe rais kutekeleza ilani ya chama?
 
Anyone to correct me please!
Was the president's statement not meant for the newly appointed DC's and RC's and RAS?
Watu ambao kikatiba wanateuliwa ili kumsaidia yy mwenyewe rais kutekeleza ilani ya chama?
Does the sentence 'wateule wangu' end with DC's, RC's and RAS's? Does the president speech in an event necessarily meant specifically for the particular event?
 
Huyo Tundu Lisu ana matatizo kichwani, hivi hata alifaulu vipi Mitihani Chuoni na kuhitimu?
 
Sasa hivi jiwe ndiye katiba, ndiye Sheria, angekua na uwezo kila kiungo cha mwili wake angekigawia cheo yaanni pua ingekua TISS, mdomo ungekua msemaji wa serikali, mkono ungekua jaji mkuu nk.
Umesahau aliposema I WISH I COULD BE IGP??

Kama ingekuwa uwezo wake ange-wish angekuwa katika nafasi yoyote ya Utendaji katika serikali yake ya awamu ya 5!
 
Anyone to correct me please!
Was the president's statement not meant for the newly appointed DC's and RC's and RAS?
Watu ambao kikatiba wanateuliwa ili kumsaidia yy mwenyewe rais kutekeleza ilani ya chama?
Hata kama wangekuwa hawajateuliwa na yeye lazima tujue kuwa ni ukweli ulio wazi kila mtumishi ana tekeleza ila ya chama kilicho madarakani na hilo halijaanza leo ...sema watanzania hatujazoea kuusikia ukweli lakini sio kwamba hatuuoni....
 
Does the sentence 'wateule wangu' end with DC's, RC's and RAS's? Does the president speech in an event necessarily meant specifically for the particular event?
To my thinking that sentence was meant specifically for that particular event.
To me it doesn't make sense saying it "kwa wateule wote" while he knows there are constitutionally neutral appointees.
 
Back
Top Bottom