Tundu Lissu baada ya Kisutu, atarejeshwa Singida kwa mashtaka mengine ya uchochezi

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Kamanda wa Polisi mkoani Singida amesema kuwa baada ya Tundu Lisu kuachiwa huko Kisutu, atarejeshwa Singida kwa ajili ya kujibu mashtaka ya uchochezi dhidi ya serikali alioufanya juzi katika mkutano wake alioufanya jimboni kwake, pamoja na ujumbe wa uchochezi alioutuma kwa njia ya simu kwenda kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA. Akitoka hapo kilo 3 hana.

Kwakuwa leo ni Tundu Lisu day kumake headlines, acha tufanye hivo.

=====updates====

Wakuu wasalaam,

Tukiwa bado tupo maeneo ya Kisutu kusubiri hatima ya mwanasheria wetu mkuu wa chama ndugu Tundu Lissu mahakamani leo, tumepata taarifa na huenda ikawa ni taarifa sahihi kabisa.

Ndugu Tundu Lissu leo atasomewa shitaka la kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya rais yaani kumuita "dikteta uchwara" na kuingilia uhuru wa mahakama kwa kutaka kujenga hoja nje ya mahakama kuwa alikuwa sahihi hapo kabla kwa kuainisha baadhi ya mambo yanayodaiwa kuipa uhalali kauli yake kisha atawekwa wazi kwa dhamana.

Lakini atakamatwa tena kwa madai ya kusambaza ujumbe wa uchochezi kwa njia ya simu yaani "sms" na huenda akapelekwa mahabusu hadi jumatatu atakapoletwa tena mahakamani.

Tuko pamoja!

C&P
 
kama hadi sasa hawabaini lissu is not scared wangemuacha,huyu guru wa sheria won't. retreat won't surrender!jpm timiza ahadi zako usipoteze muda na lissu sababu hupitia sheria halafu anaongea!

Jpm yupo zake chato, lisu yupo dar wewe unamhusishaje na raisi? Jeshi la polisi ndo linafanya kazi yake. Kwani huko dar alipelekwa ikulu? Hata yule kijana wa Mamunyange ulishaona huyo mkuu wa jeshi kahojiwa popote kuhusu huyo dogo? Hebu uwe na elimu japo ya std 4 ya kujua mambo.
 
Lissu amewatia ujasiri vijana sijapata kuona.................jana usiku nilikuwa na watoto hapa home, age 6 -12 wameniuliza Lissu anafanya kazi gani, nikawaambia, ni mwanasheria.............wakaanza kuparurana kila mmoja akiigombea hii fani.
Sikujua ni kwa nini
 
Huyu mwanaukawa anapenda sana publicity kupitia knowledge yake ya sheria, ni makosa, sioni kama ni sifa kwa mtu kufanya makosa makusudi tu eti kwa kua anauelewa wa jambo flani, that is more likely than an abuse of knowledge, amepoteza sifa ya uungwana wacha ashughulikiwe,
 
Very intelligent kids !
 
Unahisi anashughulikiwa au anawashughulisha?
 
kilo 3 atatopoteza sasa!
Akina Aun San Sukyi, Mandela, Kenyatta, Nyerere etc walisumbuliwa kwa kuwekwa kizuizini karibu nusu ya maisha yao lakini mwishoni waliibuka mashujaa ktk hoja zao.

Kupoteza kilo tatu kwa kupigania taifa liwe la kidekrasia si shida
 
Back
Top Bottom