Tundu Lissu azidi kutapatapa baada ya juhudi zake kugonga mwamba

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,890
14,339
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa mara ya pili, imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ya kujaribu kupinga uamuzi wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalitupwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Joseph Mlyambina, baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na jopo la mawakili kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

“Baada ya kusikiliza hoja za mapingamizi na majibu, mahakama inakubaliana na hoja za Serikali na inaona maombi hayana msingi kisheria kwa kuwa sheria hairuhusu rufaa kwa kesi inayofafana na hiyo,”alisema.

Katika maombi hayo namba 42 ya mwaka 2019 ya kutaka ridhaa ya Mahakama Kuu kumruhusu kukata rufaa yaliyofunguliwa Oktoba 10, 2019,Tundu Lissu alikusudia kupinga uamuzi wa yeye kuondolewa ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Kudumu za Bunge kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao zaidi ya vitatu vya Bunge pasipo ruhusa ya maandishi ya Spika.

Maombi hayo yalipingwa vikali na mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa madai hayakustahili kusikilizwa kwa kuwa yalikinzana na kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Rufani kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Na. 25 ya mwana 2002.

Upande wa Serikali, ulidai Lissu hakuwa na haki kisheria kupinga uamuzi wa Jaji Sirilius Matupa ulitolewa Septemba 9, mwaka jana wa kumnyima ridhaa kufungua shauri la mapitio ya kiutawala uamuzi ambao uliishia kwa yeye kupoteza ubunge.

Ilielezwa na mawakili wa Serikali, uamuzi wa Jaji Matupa haukupaswa kupingwa kwa njia ya rufaa kwa kuwa uamuzi huo haukumaliza shauri kama inavyopaswa kisheria.

Upande wa Serikali uliishawishi mahakama katika kesi mbalimbali, Mahakama iliamua kuwa rufaa haiwezi kukatwa kwa shauri ambalo limeisha katika hatua za awali kama ilivyokuwa kwa kesi ya Lissu ambaye alikuwa akiomba ridhaa ya kuwasilisha maombi ya mapitio na akanyimwa ridhaa kwa kuwa maombi yake hayakuzingatia Sheria.

My take : bwana huyu atulie huko huko ughaibuni au aje atuombe radhi watanzania wote kwa kosa lake la kuinajisi nchi yetu.
 
Lissu alivimbishwa kichwa kwa ile mikwara yake akaamini yeye ndiye Raia pekee mwenye akili Tanzania

Yaani anadharau watu wengine anaita rubbish, nk

Tundu lissu rudi brother uombe radhi Watanzania maisha yaendelee
Kweli kabisa yaani alidiriki kusema eti Rais wetu mzalendo namba moja hawezi kuunga hata sentesi moja ya kimombo! Sasa si angekuja kupambna na Mlyambina kupangua hizo hoja za serikali aje atetee kitumbua chake!
 
Mbona inaonekana mtoa uzi ni yule yule kwa ID tofauti anaanza kucomment.. Swala Tundu Lissue ni aibu kwa Taifa, kwa kile kilichomtokea toka Kupigwa marisasi hadi Kuvuliwa ubunge wake ni maajabu ya dunia. Hii Kama unaifurahia ni wewe tu Mtoa Mada maana unyama aliofanyiwa Lissu unahakisi ukatili wa hali ya juu dhidi ya binadamu"kupola mtu haki ya Kuishi". Ni Mungu tu ndiye anatuondolea haki ya Kuishi na wala si vinginevyo. Wewe endelea kufurahia wakati binadamu mwenzako apatapo machungu.wewe leo unaona mtizamo na mapenzi yako kisiasa ndio maisha yameishia hapo. Wazungu wanamsemo "what goes around comes around", Kuna siku utajagundua kufurahia unyama afanyiwao mwenzako ni dhambi isiyosameheka hapa Duniani.
 


















Wanalumumba achaneni na Lissu tokeni hapo nje ya ofisi zenu kuna maiti ya corona ipeleni kunakohusika mkaizike usiku usiku
 
Kweli ukisikia anavyomshambulia hayati Nyerere unajiuliza Mbona lissu anajiaibisha hivi!

Naweza kuamini kweli kuwa lissu ana matatizo hayo

Sijawahi kuona Mbowe ambaye ni boss wake hata kwa bahati mbaya anashambulia Baba wa Taifa

Ila yeye kila kinachomjia kichwani anabwata
Mkuu huyu lissu ni mgonjwa wa akili ambapo imepelekea akapata tatizo jingine la kuropoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata km ana akili hawezi kufika mbali kisiasa kwa dharau zake

Mtu mwenye elimu tena public figure unaita ripoti ya mtu mwingine rubbish hapo Ndio nlimuonaga lissu ana Tatizo
Wanaokupa like wajinga sana
 
Mkuu hata km ana akili hawezi kufika mbali kisiasa kwa dharau zake

Mtu mwenye elimu tena public figure unaita ripoti ya mtu mwingine rubbish hapo Ndio nlimuonaga lissu ana Tatizo
Unajua yeye ni "mwanasheria msomi"
 
Back
Top Bottom