1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,255
- 7,931
Karne hii walafi na wanye nchi ni watawala wenye katiba kama hii tuliyo nayo.Afe nani kwa matoi hayo - CCM iko level nyingine - acha LIssu aendelee kula mikataba ya kuuza nchi
Kwa nchi yenye katiba bora na miiko ya uongozi bila kujali vyama na maslahi ya watawala hakuna mtu mmoja anayeweza kuuza nchi.
Natamani sana nchi iondoke mikononi mwa SiSeMi ili mujue umuhimu wa kuwa na katiba bora inayowadhibiti watawala. Mumejiwahau sana na kuwaona watawala kuwa ni miungu kwa sababu tu ya kuwapa mamlaka ya kuwateua maelfu ya marafiki zao na wale wanaowataka na kuwaweka kwenye ulaji. Lakini sikukifanyiwa mnayofanyia binadamu wenzenu mtajua umuhimu wa kuwa na katiba bora na miiko ya uongozi.
Haiwezekani waziri anatoka hadharani na kutoa wito wa kuua watu eti kisa wanapinga serikali. Kama ni kuuzwa nchi ilishauzwa zamani sana ndio mana kuna watu kama Musibamsibamkuu wanaoweza kutoka hadharani na kusema kuwa kundi moja la watu liteketezwe kwa kuuawa kwa kulisha nembo ya uhaini na usaliti. Hao ndio wenye nchi na Waitatara naibu waziri. Wanahamasisha mauaji ya binadamu wenzao lakini hawakamatwi utafikiri wanazungumzia kuuawa kwa mende aubu. Aibu kubwa
Kwa kuiachi nchi ipelekwe na watu kamab akina Musibamsibamkuuliachia ni bora iuzwe kwa Mabeberu wa nje kuliko Mabeberu wa ndani wanaokula na kushika na tumewapa kila kitu na kila jema la nchi liko mikononi mwao lakini wanataka na roho za watu.
Mabeberu wa ndani hawana shukrani wanataka kutawala mpaka akili na midomo yetu na roho zetu.
Mabeberu wa ndani wabaya kuliko Mabeberu waliowahi kutokea duniani.
Kuliko kulala na Koboko ndani ni bora upite kwenye pori lake mana utapita kwa tahadhari.
Adui anayekuulia ndani ni mbaya kuliko adui wa nje.
Watanzania hatuwezi kukubali propaganda zenu za kuruvurugia Diplomasia yetu iliyojengwa tangu awamu ya kwanza.
Awamu ya kwanza ilizunguka dunia nzima bila kufungamana na upande wowote na iliheshimika kwa kujenga mijadala yenye hoja sio mitutu ya bunduki na majeshi.
Tujisahihishe sio kuzidi kujenga chuki na uongo usio na tija.
Tundu Lisu hatoke kwenye nchi ya Kidikteta Bali nchi ya Kidemokrasia yenye Vyama vingi. Na yeye ni chama cha upinzani na ameacha mamilioni ya watanzania wenye mawazo kama yake na wanaomuunga mkono. Kumdhuru Tundu kwa Mara ya pili kutaleta hasira Kali kwa watanzania wengi sana.
Kuna wauaji wanaojifanya ni wazalendo kwa kuwadanganya watu kuwa wakimuua Lisu ndio watatawala milele. Ni upuuzi wa kutisha.
Marekani pamoja na kuathiriwa sana na Ugaidi lakini kuna watu walikua wanapinga nchi yao kuingia vitani na kusababisha watoto wao kufia vitani. Hata hivyo mawazo yao hayakupingwa kwa mtutu wa bunduki Bali kwa kura.
Sent using Jamii Forums mobile app