Uchaguzi 2020 Tundu Lissu atoa tamko baada ya Wakala wake kuchukua fomu, akumbusha sifa za wanaostahili kuwa wadhamini, asisitiza kurudi nchini

Amesema Ratiba kamili ya tarehe na siku ya yeye kurudi itatolewa na uongozi wa chama baada ya mashauriano.

Aongelea pia ukimya wa vyombo husika kuhusu usalama wake na kawatoa hofu Wanachama kuwa atarudi

Mungu ambariki sana Tundu Lissu, ili maono yake yote kwa ajili ya nchi yetu yakapate kutimia na kufikia ukamilifu wote alioukusudia. Huyu kwa hakika ni "icon" ya sasa ya uzalendo hapa nchini.
 
Ati mbona kama muoga.. wa nyie wenyewe.. ndani ya chadrama yenu.. tunamkaribisha sana sana aje jamani ajionee nchi ilivyo na maendeleo mengi.. Tena mumupe nafasi awanie ili atalii nchini huku akijua JPM ana 5 zaidi..

Musisahau kumuteli kwamba nchi tumeingia uchumi wa kati.. aje tusherekee.. Hapa Kazi tu.. huku beberus wa bahasha za khaki hawapo alivyokuwa amezoea..

Mzalendo cocochanel habari ya jumapili
Pamoja na mengine yooote bahasha za kaki zimepotea sana kwenye utendaji
Lisu akaribie nchi inahitaji watu wake wote ili kuongeza nguvu kwenye kujenga taifa imara
 
Hili swala liko wazi, halihitaji mwekezaji kutambua waliotaka kumuuwa Tundu Lissu
1. Waliomnyima pesa ya matibabu
2. Waliomfukuza ubunge
3. Waliosema hawawezi kupeleka maendeleo jimbo la Tundu Lissu
4. Waliokataa kufanya uchunguzi wa kupigwa risasi
5. Wanaotaka asirudi tanzania
6. Waliomkataliwa kuingia marekani

Ushahidi ni mwingi sana kiasi kwamba hata asiyesoma sheria anaweza kusimamia kesi yake

Tundu Lissu njoo, Tanzania ni yetu na sisi ndio watanzania tunaotaka uje.

Wanoshabikia ukabila uuuwaji na upotezwaji wa watu tutawakomesha
 
Haya sasa msiempenda huyoo anakuja!! Mliosema hawezi kuludi haya sasa aibu yenu hihyoo
 
Haya sasa msiempenda huyoo anakuja!! Mliosema hawezi kuludi haya sasa aibu yenu hihyoo
Mwanzo walisema hawezi kupona,hawezi gharama za matibabu na shombo nyingine nyingi.Sasa kapona na anarudi kugombea kihoro cha nini?waliyataka wenyewe.
 
Mzalendo cocochanel habari ya jumapili
Pamoja na mengine yooote bahasha za kaki zimepotea sana kwenye utendaji
Lisu akaribie nchi inahitaji watu wake wote ili kuongeza nguvu kwenye kujenga taifa imara

Jumapili ipo salama kwangu.. namshukuru Mola. Nawe nakusoma naamini upo salama.
Lissu tabu yake.. kesi na malalamiko nchi.. viporo kibao..
 
Jumapili ipo salama kwangu.. namshukuru Mola. Nawe nakusoma naamini upo salama.
Lissu tabu yake.. kesi na malalamiko nchi.. viporo kibao..
Kupigwa risasi kwa Lissu kulitushtua na kutuumiza sana watanzania.
Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari huko ughaibuni na kupaza sauti kwamba Tanzania sio sehemu salama pia kulituumiza watanzania kama Taifa katika nyanja zote.
Nina imani kubwa kwamba uchunguzi utakamilika na haki itatendeka
 
Amesema Ratiba kamili ya tarehe na siku ya yeye kurudi itatolewa na uongozi wa chama baada ya mashauriano.

Aongelea pia ukimya wa vyombo husika kuhusu usalama wake na kawatoa hofu Wanachama kuwa atarudi

Karibu the annointed president. Njoo utuokoe huku kwa Farao mateso yamezidi.
 
Kupigwa risasi kwa Lissu kulitushtua na kutuumiza sana watanzania.
Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari huko ughaibuni na kupaza sauti kwamba Tanzania sio sehemu salama pia kulituumiza watanzania kama Taifa katika nyanja zote.
Nina imani kubwa kwamba uchunguzi utakamilika na haki itatendeka
Mnafiki mkubwa wewe
 
Anasema eti kurudi kwake kunategemea mashauriano na chama!!!!! hii kali chama kiachane naye
 
Sa kama anahofia usalama si asirudi? Mbona mambo mengine mepesi tu

Kwa watu hapawezi kuwa pazuri kuliko nyumbani mkuu. Hata mtoto mdogo ukimwacha nje ya nyumbani kuna saa ikifika anamiss wazazi, ndugu, mazingira na kudai kurudi nyumbani. Kumbuka familia ya Lissu, jamaa, marafiki, makazi na kazi viko hapa nyumbani
 
Katiba imempa mtu ruhusa ya kupigania haki yake ya kuishi. Lisu ana haki hiyo. Kama kuipigania ni kuishi nje ya Tz hana budi kufanya hivyo na hatakua wa kwanza.
 
Back
Top Bottom