Uchaguzi 2020 Tundu Lissu atoa salamu kwa wakulima

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,637
24,746
Dodoma, Tanzania

MHE. TUNDU LISSU AKITOA SALAMU KWA WAKULIMA IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA NANE NANELeo ni NaneNane sikukuu ya wakulima, tufikirie hali ya mkulima popote katika nchi hii, tufikirie hali ya mfugaji na mvuvi katika nchi hii.

Wakulima hawa wana umasikini mkubwa wakati wanatulisha wanatulisha chakula, nyama na maziwa nchi hii.

Hebu tufikirie hali hii tuachane na msemo wa Kiswahili kuwa " Mpaji ni Mungu" . Ukweli ni kuwa umasikini huu wa wakulima, wafugaji na wavuvi hautokana na Mungu.

Huu ni umasikini wa kutengenezwa siyo na Mungu, hivyo basi tunaweza kuurekebisha.

Chanzo: CHADEMA MEDIA TV
 
Mbona kama anaongea pekee yake aloo. Ila wagogo siyo watu wazuri haki ya Mungu!
 
Mbona kama vile anamuiga Magufuli kuongea yale yale ya kila siku, tena anaiga mpaka uwasilishaji wake.

Magufuli: nasema kweli sio kweli ndugu zangu
Wananchi: kweli

CDM kama chama basi ni CCM wanna be kila anachofanya Magufuli wanataka kuiga. Katoka kuchukua form kaongea na CCM na wao pia.

Uchaguzi utakuwa rahisi kama choice ni kati ya original na imitation.
 
Aisee nimemsikia mh lissu huyu bwana kichwa chake sio chi hii da da da aisee hii hatari sana , huyu mkuu kama huna hoja za mkujibu bora ukakaa kimia kazi ipo
 
aisee nimemsikia mh lissu huyu bwana kichwa chake sio chi hii da da da aisee hii hatari sana , huyu mkuu kama huna hoja za mkujibu bora ukakaa kimia kazi ipo
mkuu hizi sio spana ni hatari yahani kusikia clip hii da lissu shikamoo , na wadau walikua wanasema kwamba anazungumza mambo ya kujerhiwa tu , sasa jamani jamaa kafungua kidogo tu leo na naomba tuache ushabiki kabla ya kuchangia clip tafadhali isikilize mpaka mwisho do mwafaa
 
Hapo ni kuhusu Maendeleo ya Watu kuondoa umasikini uliotengenezwa.

CCM Mpya wao wamewatupa watu kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi na hata wafanyabishara ambao wote wanafanya shughuli za siku zote kwa bidii sana.

Lakini CCM Mpya inawebeza kuwa ni wapiga dili, wavivu au hawataki kulipa kodi wakati fedha yote inaenda kutengeneza Maendeleo ya Vitu visivyo leta mguso katika maisha yao.

Kwa hakika twaweza kulinganisha vitu hivyo kwa mfano wa ma-toy ya kuringishia kuwa tuna Maendeleo ya Vitu lakini havina maana ktk maisha ya mtu mzima anayepigania familia yake ipate mlo, mavazi, sehemu ya kulala, matibabu bora na elimu ya kukabiliana na changamoto za mazingira anayoishi.
 
8 August 2020
Mbeya, Tanzania

Wakuu wa mikoa 4 wazungumza sikukuu ya wakulima ya NaneNane, watoa angalizo uchaguzi, wamfariji Albert Chalamila 2020Wajigamba mikoa yao inakwenda kubaki CCM chini ya Rais bora kuliko wote kwa sasa barani Afrika. Wamewabeza wapinzani watabaki kuwa waigizaji kama comedian anayejiita Baraka Magufuli.

Hayo yamesemwa na wakuu wa mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa huku wakimpa matumaini mwenyeji wao RC Albert Chalamila wa mkoa wa Mbeya asiwe na wasiwasi safari hii mambo yatakuwa mazuri 2020.

Pia wakuu hao wamesema hawataruhusu kampeni za matusi, kejeli na fujo katika mikoa yao.
Source: Haroub TV
 
8 August 2020
Mbeya, Tanzania

Dr. Tulia azungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, siku ya wakulima Nane Nane .


Dr. Tulia Ackson akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Mbeya, amewafahamisha wakuu wa mikoa na wananchi kuwa serikali imeamua kuweka mkazo katika kuimarisha vyama vya ushirika maana wakulima wamekata tamaa katika ukulima. Dr. Tulia amesema pia serikali imefuta kodi 17 katika mazao ya wakulima.
Source: Haroub TV
 
8 August 2020
Mbeya, Tanzania

Maonesho ya Kikanda NaneNane 2020 KAULI MBIU “KWA MAENDELEO YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020Dr. Tulia Ackson, mgeni rasmi katika maonesho ya NaneNane sikukuu ya wakulima yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya atembelea mabanda ya washiriki mbalimbali kuadhimisha siku hiyo ya wakulima.

MKUU WA MKOA WA MBEYA MHE. ALBERT CHALAMILA,KWA NIABA YA WAKUU WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI,ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA SHEREHE NA MAONESHO YA NANENANE 2020 KIKANDA YATAFANYIKA KATIKA UWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA KUANZIA TAREHE 01 HADI 08 AGOSTI 2020.

EWE MKULIMA, EWE MFUGAJI, EWE MSINDIKAJI JITOKEZE KUSHIRIKI KWENYE MAONESHO HAYA YENYE KAULI MBIU ISEMAYO “KWA MAENDELEO YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”

WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWAKUJIFUNZA TEKNOLOJIA MBALIMBALI ZA UZALISHAJI NA USINDIKAJI WA MAZAO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. Source : Sherehe za Nanenane 2020
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom