Tundu Lissu atangaza rasmi Zitto kuvuliwa uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.

sir.JAPHET

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2012
Messages
699
Points
170

sir.JAPHET

JF-Expert Member
Joined May 18, 2012
699 170
Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA.

Screenshot from 2015-03-10 12:57:22.png
Kupitia taarifa zilizosambaa kuhusu kufukuzwa kwa Zitto Kambwe uanachama CHADEMA, mwanasheria wake Albert Msando kaandika kupitia Instagram taarifa hii..

Taarifa kuhusu maamuzi ya Mahakama Kuu leo tumezipata kupitia mitandao ya kijamii kwa sababu kesi awali ilikuwa imepangwa tarehe 12.03.2015 lakini inaonekana kwenye rekodi imerudishwa nyuma na maamuzi hayo kusomwa leo bila sisi kuwa na taarifa. Tunafanya utaratibu tupate nakala ya maamuzi hayo ili kujua nini cha kufanya.

Hatuna taarifa rasmi ya kufukuzwa Mh. Zitto Kabwe uanachama.

Taratibu zote zitafuatwa pindi tukipokea taarifa rasmi kutoka mahakamani na kwenye chama. Ni matumaini yetu jambo hili halitaendeleza chuki zisizokuwa na sababu au kujenga kati ya wahusika. #Demokrasia #Haki #UtawalaBora #Taratibu
Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa - JamiiForums

Picha: TUNDU LISU akiwa Mahakamani pamoja na ZITTO KABWE - JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,366,166
Members 521,386
Posts 33,362,074
Top