Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058


Tundu Lissu anasema huo sio uamuzi wa bunge ni uamuzi wa wabunge wa CCM, pili amesema kuna kanuni za kibunge za kutoa adhabu kwa wabunge wanaokosea na kanuni ya kumfungia mbunge kwa miezi 10 hiyo kanuni haipo.

Ila inapofika kwenye masuala yanayowahusu wabunge wa upinzani wanapewa adhabu kubwa ambazo hazipo kwenye kanuni
Kanuni zinasema kiwango cha juu cha idadi ya vikao anavyoweza kufungiwa mbunge ni vikao 20.

Kanuni zinasema pia bunge linaweza kutoa adhabu nyinginezo ila adhabu nyinginezo haiwezi ikawa sawa na hiyo iliyotamkwa na sheria, kwa hiyo kama adhabu ni ya kufungiwa, adhabu nyinginezo haiwezi ikawa ni kumfungia mbunge kwa muda mrefu zaidi.
Ameendelea kusema bunge la Ndungai wanaelekea kufikiri kwamba bunge linaweza kumsimamisha mbunge kwa kipindi watakachojisikia wenyewe
Kwa tafsiri hiyo ya Ndungai ni kuwa mbunge anaweza kufungiwa kwa miaka 5 maana yake ni kukufungia usiwe mbunge kabisa.

Katiba inasema mbunge anaweza kuondolewa kwenye ubunge wake kwa shauri la uchaguzi linalofunguliwa mahakama kuu.

Ila kwa sasa watu wanazuiwa kuwa wabunge sio kwa shauri la mahakama kuu bali kwa udikteta wa watu walio wengi, udiktetea wa wabunge wa CCM

Jambo jingine ni mbunge anayeadhibiwa na bunge ni lazima apewe nakala ya mashtaka dhidi yake, apelekwe kwenye kamati ya haki kinga na mamlaka ya bunge akasililizwe na kamati ilete mapendekezo bungeni yanajadiliwa na mbunge apate haki ya kujitetea lakini waliofungiwa hawajapewa nafasi ya kujitetea.

Amesema Zitto Kabwe alipofungiwa miezi kadhaa mwaka 2007 alipewa nusu saa ya kujitetea lakini Ndungai anafikiri kwamba anaweza kuamua anavyotaka

Na kwa sababu ni makosa wataenda mahakamani, anasubiri warudi kutoka msibani na mahakama iwaambie bunge linaweza kumfutia mbunge ubunge wake kama Ndungai alivyotafsiri?
Bunge linaweza kutoa adhabu ambayo haipo kwenye kanuni? Bunge linaweza kumuadhibu mbunge bila kumpa nafasi ya kujitetea kwenye kamati wala bungeni?

Amesema tukiendelea hivi wabunge wa CCM wanaweza kuamua mbunge asiingie bungeni kwa miaka 5

Amesema mkakati wa kuuwa bunge ni mkubwa sana, umeanzia kwenye kulizima wananchi wasilione, kuvuruga uteuzi wa kamati zake, kamati za bunge zimeteuliwa na Magufuli Ikulu, Nfungai kazi yake ni kupiga mhuri tu

Serikali ndio inayoamjua wapinzani wake waikosoe vipi, wapinzani wanapeleka hotuba zao kisha wanaamua kipi kiondolewe kipi kibaki, wanawafundisha jinsi ya kuwa wapinzani

Amesema huo ni mkakati wa kuuwa bunge sio kuuwa upinzani, hawawezi kuuwa upinzani, wanalifanya lisiwe na maana halafu hata kulipiga marufuku inakuwa ni rahisi
 
~~~>>Kwakuwa sifa kuu ya Mbunge ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ndio maana wanafikia maamuzi ya kihayawani kama haya.



Wengine walifikia kutoa ushauri kuwa Mdee & Bulaya wafukuzwe...... Hawa walionyesha kiwango cha juu kabisa cha Ujinga wao
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom