Tundu Lissu apata passport mpya, amshukuru Rais Samia, kurudi Nchini

Siku niliposema kitakachompata lissu, waliokuwepo waliona naota. In 24hrs happened what happened.

Sijui unabishia nini. Aache tamaa za madaraka ndani ya chama, atakuwa salama.
Tena anavyoendeleza ligi na jamaa wakati jamaa bado ana hasira za kukaa lupango kwa muda mrefu, tutamsikia tu.
 
Lisu anaonyesha ni careless kama hawezi tunza document ya kwake muhimu kama Passport na kupaka matope nchi za Ulaya kuwa kuna vibaka wa kumwibia mswahili lofa Passport!!
Watu wameishi Miaka nenda rudi Ulaya hawajakutana na pick pockets Lisu kachafua Ulaya kuwa wako vibaka wenye dhiki wawezao ibia mswahili lofa mkimbizi

Aiombe samahani jumuiya ya Ulaya kwa kuwachafua image yao

Akipewa document sensitive za nchi si atapoteza
 
Mh. Tundu Lissu, heshima kubwa sana kwako kwa kuwa Brilliant, Courageous na daring person. Mungu azidi kukupa Ulinzi wake peke yake kama ambavyo historia ilijiandika. Kwa unayoyawaza juu ya Rais Samia na kusita kwako kurudi Tanzania:
1. SSH akiwa Rais nakukutembelea hospital Nairobi kipindi ambacho JPM akiwa anakuchukia wewe kiwango cha "ufe".
2. Ni SSH aliyekubali kuonana nawe Brussels. Peke yake sio jambo dogo hata kama ilikuwa ni ku bow on certain world political pressures.
3. Kakupa passport haraka japo tutasema ni haki yako. Sawa.
4. Lakini Kapilima hayupo tena kwa system, JPM kaondolewa na Mungu, Ndugai kaondolewa na SSH, Kina Kingai & co ya kina Sirro imeumbuka hadharani na baba yao hayupo tena, Sabaya kufungwa haswaa, Makonda nae ameshaanzishiwa doze, naona nia njema ya SSH binafsi kwa kila mtu.
5. Kwamba SSH ametamka utaishi kama raia mwingine ukirudi Tanzania, kwa maana hatakupa ulinzi maalum, bado sijaona nia mbaya kwake. Tafuta ulinzi kama wa Mbowe siku ziende. Kama kulindwa, mbona JPM alilindwa sana? Mkono wa Mungu upo. USIOGOPE! Woga ukizidi hugeuka kuwa ugonjwa. Mwisho wa siku Mimi, wewe, SSH, Mbowe na kina Kapilimba tutakufa tu kwa ratiba ya MUNGU hata tujifiche wapi.
6. Unavyozidi kukaa mbali, ndivyo na relevance yako politically itafutika. Nakutia shime kwa jina la Mungu, nikiamini SSH hana genge la kuua watu. Mungu akulinde kuingia kwako na kutoka kwako tangu sasa na milele yote!
 
Godbless Lema, Ezekiel Wenje na Tundu Lisu huu ni wakati wa kurudi nyumbani tuje tuijenge nchi pamoja.

Japo washiriki wa mkutano wa Maridhiano hawajazungumzia kabisa swala la viongozi wa kisiasa mnaoishi uhamishoni lakini lililo wazi ni kuwa Rais wetu mama Samia anawapenda sana.

Tafadhali Lema, Wenje na Tundu Lisu karibuni tena nyumbani.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wapinzani wa Tanzania wanashangaza sana.

Mfano Tundu Lissu. Ambaye namuheshimubjwa kazi nyingi alizofanya, lakini bado anashangaza.

Anadai rais wa Tanzania ana mamlaka kubwa sana, apunguziwe mamlaka.

Halafu, tukija kwake Tundu Lissu tuangalie anavyoishi, tunaona yeye mwenyewe anampa rais madaraka ya mpaka kufuatilia passport.

That was rather weird.

Ukizingatia kuna mfumo wa kudai passport mpya ambao haumuhitaji rais.
 
Lisu muda wowote ataunga juhudi na kuingia CCM!! Poleni chadema!! Ataangalia maslahi binafsi zaidi!!
Mabeberu wamemçhoka!! Hana jinsi!! Muda si mrefu ataungana na Dr mihogo (Dr Slaa) huko ccm!
 

Tundu Lissu amepewa passport mpya na Serikali ya Tanzania baada ya ile ya awali kupotea kwa kuibwa kule Ujerumani.

Lissu amekabidhiwa passport yake leo na balozi wetu.

Lissu amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo Watanzania wote tumuunge mkono ili tujenge Tanzania mpya yenye Upendo na Umoja.

Tundu Lissu amemshukuru sana Rais Samia.
===

"Niko tayari kurudi nyumbani muda wowote baada ya masuala ya kiusalama kukamilika, siishi Ubelgiji kwa hiari yangu naishi kwasababu kuna watu katika nchi yetu ambao walijaribu kuniua, walinipiga risasi nyingi sana na watu hao mpaka sasa Serikali yetu inawaita watu wasiojulikana hakuna uchunguzi uliofanywa hakuna alie kamatwa, hakuna alieshitakiwa, hakuna anayejulikana, kwahiyo katika mazingira hayo inabidi tuangalie masuala ya kiusalama ili niweze kurudi nikiwa salama"- Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!

====

Lissu: Utendaji wa Rais Samia utaponya makovu​



Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema- Bara, Tundu Lissu amesema mwenendo wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unaonyesha kuwa unakwenda kuyaponya makovu ya mambo mabaya yaliyotokea siku za nyuma.

Lissu alisema katika utendaji kazi wake, Rais Samia amekuwa kiongozi wa kurekebisha mambo mabaya na kutaka mambo yafanyike katika hali ya usawa. Alisema Rais huyo akibaini kuna jambo halikufanyika sawa, analirekebisha.

Kiongozi huyo wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini, aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa akizungumza katika kipindi cha medani za siasa, kinachorushwa na runinga ya Star Tv.

Lissu alifanyiwa mahojiano hayo, kwa njia ya mtandao moja kwa moja akiwa Ubelgiji anakoishi kwa sasa.

Hata hivyo, alipoulizwa ikiwa anaungana na vijana wa sasa wanaosema “mama anaupiga mwingi” ikimaanisha anafanya vizuri sana, Lissu alisema: “Mimi sio mpiga vigerere, lakini kuna mambo Mama (Rais Samia) ameanza kuyafanya vizuri, kwa sababu ameyafanya vizuri, tutaungana naye ili ayafanye vizuri zaidi. Kuna kazi kubwa iliyopo mbele yake ambayo si rahisi, lazima tumpe moyo.

“Lazima tumwambie mama kwenye safari aliyoianza asiogope, unakwenda vizuri na dunia inakuunga mkono na sisi tutakuunga mkono kwenye hii safari ya kusaidiana kuiweka nchi yetu katika misingi bora ya kidemokrasia,” alisema Lissu.

Mwanasheria huyo alitolea mfano namna Serikali ilivyoshughulikia suala Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake kuachiliwa, baada ya kufutiwa mashtaka ugaidi.

Katika maelezo yake, Lissu alisema si yeye peke yake aliyefanikisha Mbowe kuachiliwa kwa kuzungumza na Rais Samia, bali wapo wananchi wengi wakiwamo wa ndani na nje waliopaza sauti zao.

Alisema kesi kubwa ya kisiasa kama ya Mbowe, mara nyingi huwa kunakuwa na jitihada nyingi zinazofanyika ndani na nje ya nchi kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana.

“Mimi ni mmoja kati ya watu wengi tuliomwambia Rais Samia aachane na kesi hii kwa sababu ilikuwa inamchafua, inaichafua nchi, chama chake, Serikali na ilikuwa inaligawa Taifa na inatesa watu,” alisema
Alisema kulikuwa na jitihada kubwa si za viongozi wa kidini pekee, bali hata wanasiasa ambao hawajahi kusemwa.

“Rais aliniambia atalifanyia kazi na amelifanyia kazi. Kwa heshima yake anaifanya sasa Tanzania ielekee katika misingi mipya ambayo mambo mabaya kama haya huenda yasitokee tena, ni vizuri tukasaidiana naye na kumuunga mkono ili asirudi nyuma na kutetereka,” alisema kiongozi huyo.

Apata pasipoti mpya
Akizungumzia suala la hati yake ya kusafiria, Lissu alisema ilipotea alipokuwa Frankfurt –Ujerumani alikokuwa amekwenda kumsindikiza kijana wake aliyekuwa anakwenda Marekani, lakini wakati akirejea Ubelgiji, begi lake lililokuwa na vifaa mbalimbali ikiwemo pasipoti lilikwapuliwa katika Kituo cha treni.

Hivyo, ilimlazimu kuomba hati nyingine kwa njia ya mtandao lakini kwa sababu za hofu kuwa muombaji ni Lissu, alipokutana na na Rais Saamia ilibidi amweleze hana hati ya kusafiria, na angetaja kurejea nyumbani ikiwa ataridhia.
“Rais aliniahidi atalifanyia kazi, nataka niwajulishe kuwa hati yangu mpya ya kusafiria imefikia leo (juzi), hapa Ubelgiji. Rais amelifanyia kazi ombi langu, nachukua fursa hii kumshukuru sana,” alisema Lissu.

Kurejea Tanzania
Kuhusu kurejea Tanzania, alisema kwa sasa anaendelea vema na yupo tayari kurudi muda wowote.
“Tusihesabu tena mwaka, miezi na wiki, nitarudi nyumbani. Nimemuomba Rais afanye kitu kimoja, aseme hadharani kwamba Lissu ‘njoo nyumbani utakuwa salama’…Nikamwambia akifanya hivyo, nitarudi nyumbani.

Alipoulizwa anadhani kwanini hadi sasa Rais hajatamka hilo, Lissu alisema “Rais Samia ana kazi na mambo mengi, sitaki kuamini amekataa kufanya hivyo, kwa sababu aliniahidi kulifanyia kazi.”
Lissu alisema masuala mengine aliyahidiwa na Samia kuwa atayafanyia kazi, yameshatekelezwa, hivyo anaamini hata hilo litatekelezwa muda si mrefu.

Pia alimshukuru kwa kumuahidi kushughulikia mafao na kiinua mgongo chake na fedha za matibabu ambazo hakuzipata wakati akiwa mbunge na aliumizwa kazini.

Atakubali uteuzi?
Alipoulizwa kutokana na mwenendo mzuri wa utendaji wa Rais Samia, ikitokea akamteua atakubali, Lissu alisema hataukubali uteuzi huo.

“Rais akaniteua nimwambia mheshimiwa Rais kumbe hunipendi kiasi hicho? Kama unataka nikusaidie ufanye kazi yako vizuri, naomba uniache niwe huru ili nikwambie mambo yanayokwenda vibaya bila kuogopa kwamba wewe unanilipa mshahara.

“Kwa sababu akishaanza kukulipa mshahara, atakuziba na mdomo hii kitu haitawezekana kabisa…
Itakuwa ni kitu kibaya kwa Tanzania kupoteza sauti imara nje ya Serikali,” alisema Lissu.

Chanzo: Mwananchi
Tundu Lissu haridhiki na chochote mpaka awe Rais. Sijuwi ni nani atampigia kura? Watanzania wengi WANAMUCHUKIA kwa matusi anayomutukana Hayati Magufuli. Raisi aliyekuwa kipenzi cha Watanzani. LAWAMA zisizokuwa na ushahidi. Hata waliokuwa wakimuonea huruma hawamuonei tena Huwezi kuendelea kumutusi mtu ambaye hawezi kukujibu huwo ni ujinga mkubwa haisaidii. Lawama zenyewe ni za kutunga bila ushahid. Tundu Lissu hana hadhi ya kuwa kiongozi. Akae huko huko Ubeligiji watu wapumuzike na kelele zake
 
Daaaa wajameni Mama Samia!! ni Mama zaidi na anapendeza kuwa Mama Rais jamani ana roho nzuri huyu Mama mwewe!!! mpaka mtu unatamani kuimeza uwe km yeye lkn sasa..... utanzia wapi??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom