Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Mtu asiye na hoja utamjua tu!Umeruka kutoka kwenye hoja umekimbilia Corona na kuanza kunijumlisha na kundi la watu!
Jikite kwenye hoja,watu 13 wamepigwa risasi,akina mama wawili wamebakwa na wengine wamejeruhiwa majina yametajwa halafu mnaleta porojo hapa!Mtu wa 14 amekufa leo,alipigwa risasi miguuni,wauaji wakubwa!
Mnaua wtz wenzenu utafikiri mtaishi milele?
COMPLETE LIE! Vipi wale mliotaka wafie barabarani??? Hawakuwa watu??? Nyie wasababishi na wachochezi wa machafuko na ghasia na vifo vya Watanzania ndio wa kwanza kukimbilia kwenye balozi na kukwea pipa kwenda kujificha mkiogopa mauti, ilhali mmewadanganyeni wenyewe. Basi wapeni hata hela za matibabu au mazishi.
 
Huyo Mr Mzungu hana hadhi yoyote ya upinzani kwa sababu kageuza siasa kama uwanja wa kulitafuta kwa nguvu zote. Ndiyo maana kwenye kampeni alipuuzwa lakini yeye analazimisha kujiingiza kwenye kumi na nane za mamlaka ya dola. Reasoning na "taa-get" yake ni kufunga "mar-goal-i" ya kimataifa anayodhani hupatikana kwa vurugu na ghasia na tafrani. Hizo ni siasa za South Sudan, Kongo na Nigeria huko.

Maalim Seif and Lissu are Savimbis!Period.
 
You must be seriously joking, japo haya maneno mawili huwa hayakai pamoja kirahisi. Nina mashaka sana na uwezo wako wa kuelewa mambo. Ninyi mlishindwa kura kihalali, full stop. Stori zaidi waulizeni wagombea wenu wakiwa sober mtajua. Imagine "wapiga-kura wenu" did not raise any appreciable concern!???

Kama Hadi jumuia za kimataifa zimethibitisha we ni nani upinge
 
Wadau ninawaza kwa sauti tu! Hivi kama kuna nia ovu kama tunavyoaminishwa, je Lissu ni tishio kabla au baada ya Uchaguzi?! Mbona kafanya kampeni kwa amani ,kalindwa na kulisifu Jeshi la polisi?! Kwa nini tishio la ghafla?!! Naomba msaada kwenye tuta.
Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA , ameondoka nchini humo leo Jumanne kwenda Ubelgiji huku akisema “sikimbii mapambano, ila nakwenda uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.”

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam (JNIA), Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), amesindikizwa na maofisa wa Ubalozi wa Ujerumani, Marekani, ndugu, jamaa na marafiki.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Lissu amesema, ameamua kuondoka nchini, pamoja na mambo mengi, kunusuru maisha yake na “kujipanga upya kisiasa.”

Lissu anasema, amekuwa akitishiwa maisha yake, mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi mkuu wa Oktoba, hali iliyomfanya yeye na wasaidizi wake watatu, kukimbilia kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani, jijini Dar es Salaam, ili kuomba hifadhi.

Mwanasiasa huyo amekuwa nyumbani kwa Balozi huyo tangu Jumatano ya tarehe 4 Novemba 2020.

Katika Uchaguzi huo, Lissu alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 1.9 milioni, huku Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitangazwa mshindi kwa kupata kura 12 milioni kati kura 15 milioni zilizopigwa.

Kupatikana kwa taarifa kuwa maisha ya mwanasiasa huyo machachari wa Upinzani nchini Tanzania yako hatarini, kunakuja miaka mitatu, tangu aliposhambuliwa kwa risasi na wanaoitwa, “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma

Shambulio dhidi ya Lissu, lilifanyika mchana wa tarehe 7 Septemba 2017, wakati alipokuwa akirejea nyumbani, akitokea viwanja vya Bunge, kuhudhuria mkutano wa Bunge la asubuhi.

Mara baada ya tukio hilo ambalo lilimjeruhi vibaya, mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisafirishwa hadi nchini Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye nchini Ubelgiji.

Lissu alirejea nchini Jumatatu, tarehe 27 Julai 2020, kutokea nchini Ubelgiji na kujitumbukiza moja kwa moja kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, mke wa Lissu, Alicia Magabe, ameondoka Tanzania kuelekea nchini Ubelgiji. Magabe aliondoka nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ameongeza, “mimi siyo mtu wa kukimbia vita. Maisha yangu yote, nimekuwa mtu wa mapambano,” amesema mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Alipoulizwa anatoa wito gani kwa wananchi waliompigia kura na Watanzania wengine, Lissu amesema, “ujumbe wangu kwao, ni kwamba mimi sikimbii mapambano. Nakwenda kufungua uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.”


 
Nani kapigwa risasi? Au na wewe ndo umekula matango pori ya kigogo halafu unakuja kuleta ushambenga huku JF
Waketajwa majina na uzi upo hapa kupitia taarifa rasmi ya ACT wazalendo!Kama ni uongo mbona Zitto hajakamatwa?
Kuwwni na huruma na watanzania wenzenu!
Halafu wazanzibar ni wajinga sana,inakuwaje kila mwaka wanakubali askari kutoka bara kupelekwa zanzibar kulinda amani mwisho wa siku wanawauwa bila kujali?
ingekuwa ni askari wazawa wa Zanzibar ,wasingefanya unyama huo kwa ndugu zao!
 
Na bado mpka akili ziwakawe sawa!

Eti ni yeye! My foot
Wewe mburura kuna unachofaidi kwani?
Watu wameuawa!
Watu wamebambikiwa kesi!
watu wamepigwa!
Watu wamefukuzwa kazi bila utaratibu!

Nauliza tena unafaidi nini?
Au wewe ni mmoja wapo wa kuburuzwa the hague kura za petition zilitosha kumbe!
Picha za mauaji na wizi wa kura na zipo mahakamani.
Nauliza tena unafaidi nini?
 
Wewe mburura kuna unachofaidi kwani?
Watu wameuawa!
Watu wamebambikiwa kesi!
watu wamepigwa!
Watu wamefukuzwa kazi bila utaratibu!

Nauliza tena unafaidi nini?
Au wewe ni mmoja wapo wa kuburuzwa the hague kura za petition zilitosha kumbe!
Picha za mauaji na wizi wa kura na zipo mahakamani.
Nauliza tena unafaidi nini?

Unamtolea nani hili povu?

Nilikutuma umshabikie huyo mbeligiji wako?
 
Tundu anakwenda kula mabilioni yake aliochangiwa na mabeberu
Kama alishindwa kuleta Mageuzi akiwa nchini,hatoweza kuleta Mageuzi kwa Twitter,ni majuha tu ndio watamuelewa
Tutegemee Tundu akirudi akiwa mzee ,kachoka Kama Abdulrahman Babu na Oscar Kambona,
 
Hapana ataitisha kikao cha Magufuli kukodi majeshi ya Burundi
Kwa hiyo hapa nchini pana wanajeshi kutoka burundi?

Hizi takataka huwa anawalisha kigogo muwe mnatapika huko huko mnakozitoa
 
Kwa hiyo hapa nchini pana wanajeshi kutoka burundi?

Hizi takataka huwa anawalisha kigogo muwe mnatapika huko huko mnakozitoa

Majeshi ya Burundi yapo na wengine wamevishwa sare za Polisi usilete uda hapa kila mtu anajua na hao majeshi wenu wanatuambia mitaani hakuna cha siri tena
 
Back
Top Bottom