Tundu Lissu: Anayelishwa na kodi zetu ndio anasema Tanzania hakuna njaa

Sijaona point hapo...mim nasubir wiki mbili nivune mahind kama gunia 20...haya maisha ya siasa siyawezi...huku kwetu chakula shazi...njaa tunaiskia mitandaoni....
 
Tundu Lissu akihojiwa na DW muda mfupi uliopita anasema kuwa Magufuli anachukulia jambo la njaa kuwa ni habari za uwongo kwa sababu yeye anaishi vizuri kwa kodi za wananchi.

''Hakuna njaa kwa sababu Magufuli anakula, na mamlaka zinazohusika na kutangaza njaa haziwezi kutangaza kwa kuwa watafukuzwa kwa kutofautiana na msimamo wa Rais'', alisema Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Wakili katika Mahakama Kuu.

Tundu Lissu pia amesema mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa sana katika kuwapa jamii elimu kuhusu nchi yao na utendaji wa serikali lakini Magufuli anadhani mitandao na vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kumsifia tu.

Anaendelea kueleza kuwa, kukamatwa kwa sababu ya kumkejeli Rais ni udikteta kwa kuwa katika nchi za demokrasia kwa kuwa rais akifanya mambo ya hovyo raia akimkejeli hana hatia.

Amezungumzia uchaguzi wa jimbo la Dimani ni wa muhimu ukizingatia hali ya siasa ya sasa, katika mwaka mmoja wa utawala wa Magufuli amevuruga sana haki za kidemorasia na kutumia mabavu kukandamiza haki za Wazanzibar na ametanabasha kwamba wakifanya vizuri kwenye uchaguzi huo ni wazi kuwa wananchi wa Zanzibar wameona utawala huu haufai.

Lissu amezungumzia pia uchaguzi wa Kenya na kudai ndio kwenye afadhali kwa nchi za Afrika Mashariki na utatoa fursa ya kujifunza kwa nchi zisizozingatia demokrasia.

CHANZO: DW Habari

personal interest
 
Chadema tokea wamsafishe fisadi Lowasa hawatakuja kuaminika tena mbele ya macho ya watanzania.

Watabaki kushabikiwa na malofa tu.
Richmond ni ya kikwete wamemsafisha kwa kosa lipi? Ukweli ndiyo umemsafisha Lowasa toka kwa waliokuwa wakidanganywa na Timu membe na January.
 
Mtakwepa sana matone ya mvua. Lakini kamwe huweze kukwepa matone mvua.

Kauli ya Lowasa fisadi waanzilishi ni nyinyi na mkafikia kumwita fisadi papa hapo mwembe yanga.
Fitna ziliundwa na kikwete akapenyeza kwa Slaa kisha wakasambaza kwa bidii pasipo kumpa nafasi lowasa kujieleza,lakini alipokwenda chadema akapewa nafasi akawaelezea vizuri mchezo wote wa Richmond ulivyokuwa wakagundua kuwa Richmond ni ya kikwete.
 
Zile tuhuma za kushiriki kukiuza Chama kwa Nyeupe hadi leo hajakanusha. Tumwamini yeye ni nani? Mchumia tumbo mkubwa huyu, kama wanasiasa ni wanafiki huyu ndo babu wa unafiki. Hachelewi kuyatakasa matapishi yake na kuyala huyu! Hivi leo Tundu Lisu amekuwa ni mtu wa kumsifia Kikwete? Naanza kupata shaka labda tunao vichaa wanaoaminiwa.
Propaganda za kupewa pesa ziliundwa na Membe na January mkalishwa mkakariri hadi leo,lakini wenye Akili wanajua huo uzushi ulitengenezwa ili kudhoofisha Lowasa,ni wajinga pekee wanaamini hizo propaganda,watanzania wa sasa wanajua Ukweli wote hata mkiendelea kupakaza Uongo itakuwa ngumu kuwageuza waamini uzushi wenu.
 
Lissu is heroes... One day he will become a great leader of our national.. God bless
 
naomba niendelee kuwakumbusha, japokuwa habari hizi huwa haziwavutii wengi wenu..

Magufuli tutaendelea kumuona Ikulu hadi 2025
Mungu akimuweka hai..

Rafiki,
Let me tell u one thing. Mtawala yeyote akianza kujitwalia mamlaka kama anavyosema kuwa AKISIMAMA MAGUFULI NI MUNGU KASIMAMA! Mungu huwa hadhihakiwi! Mtu akianza kujifanya kuwa mungu, Mungu humwondoa mara!
 
Makonda alijidai Mungu sasa yupo marekani anajitibia ugonjwa usiojulikana.
 
Rafiki,
Let me tell u one thing. Mtawala yeyote akianza kujitwalia mamlaka kama anavyosema kuwa AKISIMAMA MAGUFULI NI MUNGU KASIMAMA! Mungu huwa hadhihakiwi! Mtu akianza kujifanya kuwa mungu, Mungu humwondoa mara!
Mkuu..! Unajua Lema anafanya nini muda huu?
Wewe hata dhamana haitazungumziwa kabisa
 
Sijaona point hapo...mim nasubir wiki mbili nivune mahind kama gunia 20...haya maisha ya siasa siyawezi...huku kwetu chakula shazi...njaa tunaiskia mitandaoni....
Nimekupenda bure!nikaribishe tafadhali nikusaidie kuvuna.acha watoto wakalale.
 
*Tundu Lissu anafikiria kwa kutumia nini?*

Amesikika leo akimnanga Mh Rais Magufuli kua eti analishwa na kuveshwa kwa kodi za watanzania ndo maana haoni uchungu wa kutangaza kua Tanzania kuna naa.

Huu ni wivu ambao tumeuozoea kufanywa na watu wenye jinsia ya kike pekee.

Tundu Lissu anahoji stahiki za kisheria anazolipwa Mh Rais.Huu ni ujuha.

Tundu Lissu kama anajua wajibu wa mtu anayelishwa na kuvishwa kwa kodi ya wananchi katika kuleta maendeleo na usawa, mbona yeye kule jimboni kwake (Singida Mashariki) amegeuka kua muasi kwa kuwachochea wananchi wagome kutekeleza miradi ya kimaendeleo ,wakati na yeye analishwa na kuvishwa kupitia kodi wanazolipa watanzania kupitia mshahara wake wa kibunge.

Tundu Lissu amesema jimboni kwake kuna njaa , amesahau kwamba ni yeye ndio alikua kinara katika kuwaambia wananchi wahujumu miundombinu ya mradi mkubwa wa kilimo cha kisasa ulioanzishwa na kampuni Singida Agriculture Ltd . Mradi huo ulikua ni shirikishi kwa kuwasaidia wakulima nyenzo za kilimo kama vile trekta, mbegu na mbolea lakini kwa vile mkurugenzi wa kampuni hiyo ni kada wa CCM Tundu Lissu kwa ulafi wake wake wa madaraka akaona maslahi yake ya kisiasa yanatishwa akaamua kuratibu hujuma za wazi wazi dhidi ya mkurugenzi (Ally Mohamed) na kampuni yake.

Pia alikua mstari wa mbele akiwachochea wanachi wasifanye kazi wasubiri fedha kutoka serikalini.

Amewaharibu wananchi katika kata za Unyagumpi, Mkiwa,Kimbe ambao wakaacha kulima kwa ulaghai na ghilba zake za kisiasa matokeo yake wamegeuka ombaomba katika barabara kuu ya Singida Dodoma.

Ni vema Tundu Lissu akaacha kua kuhani wa wapiga dili ,wezi , walarushwa na mafisadi.

Arudi jimboni kufanya kazi na sio kulala mahotelini kila uchwao katika jiji la Dar es Salaam huku wanachi wakiwa na kiu ha kumuona mbunge wao bila mafanikio.

©Augustino
 
Augustino
Wewe unadhani anakula rais anakula dona la nyumbani kwenu.kiazi wewe
 
Tundu Lissu akihojiwa na DW muda mfupi uliopita anasema kuwa Magufuli anachukulia jambo la njaa kuwa ni habari za uwongo kwa sababu yeye anaishi vizuri kwa kodi za wananchi.

''Hakuna njaa kwa sababu Magufuli anakula, na mamlaka zinazohusika na kutangaza njaa haziwezi kutangaza kwa kuwa watafukuzwa kwa kutofautiana na msimamo wa Rais'', alisema Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Wakili katika Mahakama Kuu.

Tundu Lissu pia amesema mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa sana katika kuwapa jamii elimu kuhusu nchi yao na utendaji wa serikali lakini Magufuli anadhani mitandao na vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kumsifia tu.

Anaendelea kueleza kuwa, kukamatwa kwa sababu ya kumkejeli Rais ni udikteta kwa kuwa katika nchi za demokrasia kwa kuwa rais akifanya mambo ya hovyo raia akimkejeli hana hatia.

Amezungumzia uchaguzi wa jimbo la Dimani ni wa muhimu ukizingatia hali ya siasa ya sasa, katika mwaka mmoja wa utawala wa Magufuli amevuruga sana haki za kidemorasia na kutumia mabavu kukandamiza haki za Wazanzibar na ametanabasha kwamba wakifanya vizuri kwenye uchaguzi huo ni wazi kuwa wananchi wa Zanzibar wameona utawala huu haufai.

Lissu amezungumzia pia uchaguzi wa Kenya na kudai ndio kwenye afadhali kwa nchi za Afrika Mashariki na utatoa fursa ya kujifunza kwa nchi zisizozingatia demokrasia.

CHANZO: DW Habari

Ameharibu tu hapo alipoisifia Kenya.

John Mensah Pondamali yuko na RAO na EL yuko na UK..
 
Back
Top Bottom