themagnificient
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 1,021
- 3,654
Tundu Lissu akihojiwa na DW muda mfupi uliopita anasema kuwa Magufuli anachukulia jambo la njaa kuwa ni habari za uwongo kwa sababu yeye anaishi vizuri kwa kodi za wananchi.
''Hakuna njaa kwa sababu Magufuli anakula, na mamlaka zinazohusika na kutangaza njaa haziwezi kutangaza kwa kuwa watafukuzwa kwa kutofautiana na msimamo wa Rais'', alisema Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Wakili katika Mahakama Kuu.
Tundu Lissu pia amesema mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa sana katika kuwapa jamii elimu kuhusu nchi yao na utendaji wa serikali lakini Magufuli anadhani mitandao na vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kumsifia tu.
Anaendelea kueleza kuwa, kukamatwa kwa sababu ya kumkejeli Rais ni udikteta kwa kuwa katika nchi za demokrasia kwa kuwa rais akifanya mambo ya hovyo raia akimkejeli hana hatia.
Amezungumzia uchaguzi wa jimbo la Dimani ni wa muhimu ukizingatia hali ya siasa ya sasa, katika mwaka mmoja wa utawala wa Magufuli amevuruga sana haki za kidemorasia na kutumia mabavu kukandamiza haki za Wazanzibar na ametanabasha kwamba wakifanya vizuri kwenye uchaguzi huo ni wazi kuwa wananchi wa Zanzibar wameona utawala huu haufai.
Lissu amezungumzia pia uchaguzi wa Kenya na kudai ndio kwenye afadhali kwa nchi za Afrika Mashariki na utatoa fursa ya kujifunza kwa nchi zisizozingatia demokrasia.
CHANZO: DW Habari