Tundu Lissu anatufikirisha - Hivi wangekuwa Watano (5, ingekuwaje? Tungekuwa wapi?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
974
1,525
Ichukulie vyoyote vile, iwe kwa mtazamo chanya au hasi, Jina la Mh. Tundu Lissu hivi sasa lina trend na linagonga vichwa vya watu wengi, vijiweni, misibani, kwenye vyombo vya habari vya kawaida hadi mitandaoni - ndani na nje ya Tanzania. Kuanzia wanasiasa, wanasheria wenzake, jumuiya ya kimataifa hadi wananchi wa kawaida.

Nakumbuka katika vikao kadhaa vya bunge la zamani, ambalo Mama Anna Makinda alikuwa Spika, pamoja na tofauti za vyama, bado Mama Makinda alikuwa akimtumia sana na kumuomba Mh. Tundu Lissu achangie katika kuboresha hasa baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo Spika Makinda aliviona huenda vingeweza kuleta utata na mgongano wa kisheria.

Mama Makinda aliutumia vema umahiri wa Mh. Tundu Lissu ambaye kwa hakika ni mmoja kati ya wanasheria nguli kuwahi kutokea hapa nchini.

Sakata la Tundu Lissu ni fursa nzuri sana kwa wanatanzania kujifunza namna ya kukabiliana na hali kama hizi. Mazingira ya kisiasa ya Tanzania kwa sasa yanahitaji ‘masakata’ mengi zaidi kama haya ili tueweze kufikirishwa zaidi na zaidi, badala ya kuwa na maisha ya ‘business as usual’. Sakata kama hili linatupa fursa ya kujifunza sio tu kutoka kwa Tundu Lissu mwenyewe, bali hata wale ‘wanaoitikia mdundo na muziki’ unaimbwa na Tundu Lissu. Tunajifunza kuona nani ana hekima na nani hana.

Katika watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 55, najaribu kuwaza ingekuwaje laiti kama watu wenye mtazamo, uwezo na kaliba ya Mh. Tundu Lissu wangekuwa angalau watano. Ingekuwaje? Tanzania kama nchi tungekuwa wapi?

Bila shaka tungekuwa tumefikirishwa kwa kiasi kikubwa,
 
Kwanza kumpata mtu kama Tundu Lissu kwenye taifa ni hazina. Mtanzania gani angetandikwa risasi zile za kutosha YET akaendelea na harakati zake.

Yupo wapi Ulimboka, hadi wa leo alituahidi atarudi kimyaaaaaa!!

Lazima mmoja ainuliwe kwa faida ya wengine - Tumshukuru MUNGU kwa hili - leo hii Lissu akiamua kuachana na SIASA kwa namna yoyote ile basi siasa za upinzani nchini zinafikia mwisho wake kabisa yaani kifo cha mende.

Mungu mbariki Lissu.
 
Ichukulie vyoyote vile, iwe kwa mtazamo chanya au hasi, Jina la Mh. Tundu Lissu hivi sasa lina trend na linagonga vichwa vya watu wengi, vijiweni, misibani, kwenye vyombo vya habari vya kawaida hadi mitandaoni - ndani na nje ya Tanzania. Kuanzia wanasiasa, wanasheria wenzake, jumuiya ya kimataifa hadi wananchi wa kawaida.
Nakumbuka katika vikao kadhaa vya bunge la zamani, ambalo Mama Anna Makinda alikuwa Spika, pamoja na tofauti za vyama, bado Mama Makinda alikuwa akimtumia sana na kumuomba Mh. Tundu Lissu achangie katika kuboresha hasa baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo Spika Makinda aliviona huenda vingeweza kuleta utata na mgongano wa kisheria. Mama Makinda aliutumia vema umahiri wa Mh. Tundu Lissu ambaye kwa hakika ni mmoja kati ya wanasheria nguli kuwahi kutokea hapa nchini.

Sakata la Tundu Lissu ni fursa nzuri sana kwa wanatanzania kujifunza namna ya kukabiliana na hali kama hizi. Mazingira ya kisiasa ya Tanzania kwa sasa yanahitaji ‘masakata’ mengi zaidi kama haya ili tueweze kufikirishwa zaidi na zaidi, badala ya kuwa na maisha ya ‘business as usual’. Sakata kama hili linatupa fursa ya kujifunza sio tu kutoka kwa Tundu Lissu mwenyewe, bali hata wale ‘wanaoitikia mdundo na muziki’ unaimbwa na Tundu Lissu. Tunajifunza kuona nani ana hekima na nani hana.

Katika watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 55, najaribu kuwaza ingekuwaje laiti kama watu wenye mtazamo, uwezo na kaliba ya Mh. Tundu Lissu wangekuwa angalau watano. Ingekuwaje? Tanzania kama nchi tungekuwa wapi?

Bila shaka tungekuwa tumefikirishwa kwa kiasi kikubwa,
TL kiboko yao, Tl chaguo la watz
 
Kwanza kumpata mtu kama Tundu Lissu kwenye taifa ni hazina. Mtanzania gani angetandikwa risasi zile za kutosha YET akaendelea na harakati zake.

Yupo wapi Ulimboka, hadi wa leo alituahidi atarudi kimyaaaaaa!!

Lazima mmoja ainuliwe kwa faida ya wengine - Tumshukuru MUNGU kwa hili - leo hii Lissu akiamua kuachana na SIASA kwa namna yoyote ile basi siasa za upinzani nchini zinafikia mwisho wake kabisa yaani kifo cha mende.

Mungu mbariki Lissu.
Lissu ametumwa na Mungu, tazama toka harakati zake siasa, hak binadam n kirai ulishaawahi siki skendali yoyote?
 
Back
Top Bottom