Tundu Lissu anastahili kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA lakini siyo Rais wa Tanzania

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Nimefuatilia kwa karibu harakati za wakili msomi Tundu Lisu tokea aingie nchini kutoka Ubelgiji hadi sasa anapogombea urais wa JMT.

Kiukweli ingependeza sana kama Tundu Lisu angekuwa ndiye mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu anamzidi sana Freeman Mbowe kimaarifa na kwa kukubalika.

Lakini kwa nafasi ya Rais wa Tanzania bado hatoshi, angejiandaa kwanza labda kwa 2030 anaweza kuwa amejijengea uwezo.

Itoshe tu kusema kwa urais TAL anapaswa kusubiri.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huu sasa ushabiki mbuzi,😁😁,jamani kada mwenzangu,lazima ujiamini,,kumsifia lisu haina maana kuwa ndo sasa atatushinda kwenye kura,
Lisu anafaa tu,ni presdential material
 
Mwombeni Kama mtaweza awe m. Kiti was mbogamboga awezekuwaokolea jahazi linalozama
 
Mh.Lissu hatoshi kwa vigezo gani labda?Urais ni Haki ya kila Raia wa Tanzania,mwenye umri stahili,mwenye akili timamu pamoja na sifa zingine kama Elimu,Uadilifu,Uwajibikaji,Uzingativu na Kufuata Katiba ya Wananchi.Kama huyu wa sasa na waliotangulia walitosha,anashindwaje Mh.Lissu?
 
Kama huna cha maana cha kuandika kaa kimya badala ya kuanzisha thread za KIPUUZI zisizo na mantiki yoyote.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom