Tundu Lissu amzushia kifo mlinzi huyu wa Rais Magufuli?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519
Nami nimeyatazama mahojiano ya Tundu Lissu na Shaka Ssali kwenye kipindi cha Straight Talk Africa kirushwacho na runinga ya Voice of America.

Bw. Lissu kaongea mambo mengi. Na kama kawaida yake kila apatapo wasaa au fursa ya kufanya hivyo, kwenye mahojiano haya na Shaka, katema nyongo yake dhidi ya Rais Magufuli.

Ila kilicho kamata uangalifu wangu ni madai yake yeye Lissu kuwa eti yule aliyekuwa mlinzi wa Rais Magufuli, naye kafa kwa C-19!

Naamini alikuwa anamzungumzia huyu jamaa. Jamaa ambaye ali stand out kati ya waliokuwa walinzi wa marehemu.

0862B970-EE2A-4EF3-AFCB-746474104660.jpeg


Hii picha hapa chini ni baada ya Magufuli kufariki. Hapa walikuwa kanisani [nadhani ni pale kwa Mtakatifu Petro].
BCDADE97-3F03-4439-95CD-5449E75DDFE7.jpeg

Huyu jamaa mpaka kule Chato nilimuona [kama sijakosea].

Sasa, endapo ni kweli amekufa [iwapo Lissu alimaanisha ni huyu], basi jamaa atakuwa amekufa baada ya tarehe 26, Machi 2021.

Lissu kasema “his security officer...the guy that you see...the dark guy that you see behind him all the time...is dead”

Lakini kwa nini tuandikie mate wakati wino upo? Msikilize mwenyewe ili usiseme labda namzushia au napotosha alichokisema.

Video ya mahojiano ni ndefu. Kwa kuokoa muda, anzia dakika ya 21:10 mpaka 21:36.



Tundu Lissu amechanganyikiwa? Ni nani aliyemwambia kuwa huyo jamaa [kama ndo yeye anayemzungumzia] kafa? Na amekufa lini?

Tuliokuwa tunafuatilia msiba wa Magufuli kwenye runinga tulimuona jamaa. Picha zake nyingi tu za wakati wa msiba zipo mtandaoni na hata humu JF zipo!

How can Tundu Lissu say this so confidently?

Where does he get his information from?

I don’t know about you guys but this is slander.

If I were the guy [don’t know his name], I’d be lawyering up right now, even though Lissu didn’t specifically mention his name, but in my view, the description he gave is sufficient enough to know who he was talking about.

I don’t know much about Tanzanian laws with regards to defamation and slander, but if I were the guy, I’d shoot my shot and sue the hell out of him.

Calumniating people’s deaths is not cool.
 
Back
Top Bottom