Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
- Thread starter
- #21
Lissu katufungua macho,na mwenye macho haambiwi tazama!Tuchukulie mfano mdogo-kikao cha BAJETI kinajadili bajeti ya wizara isiyohusika na muungano-wanashiriki wabunge toka bara na visiwani.Kushiriki kwao kunawahalalishia kulipwa posho za ushiriki ambazo zinatokana na kodi yangu mimi na wewe mbara mwenzangu! tujiulize ushiriki wa huyu mwakilishi toka Znz una tija gani mpaka ahalalishiwe kukamua kodi yangu mie ninayeendelea kunyauka kwa ugumu wa maisha? yaani yeye akamue vikao vya bunge bara na vya uwakilishi znz kwa kodi zetu? Kuna haja ya wanajamii forum mlio na upembuzi mpana zaidi wa maswala haya mtupembulie ili wabara wengi tuone umuhimu wa kudai haki sawa ktk katiba ijayo.Kwa katiba ya sasa wabara ndo wanakamuliwa zaidi ili wa visiwani ndo mabingwa wa kulalamika kuonewa na kupunjwa! wana jf tafadhali fanyeni kazi ya ziada ya kupembua mambo bila ushabiki wa kivyama!
Hayo ndiyo tunayotaka, maana kodi zetu zinatumika hadi visiwani na pengine wengine kung'ang'ania kushika uongozi wa kamati za bunge wakati mengi yanayojadiliwa yanawahusu wabara. Wanachong'ang'ania wavisiwani ni ulaji huu tu, ebu mbara atie pua visiwani utadhani ametenda kosa la jinai wakati anatoa huduma halali.