Waachieni viongozi wenu walijadili hili kwa uangalifu.

Sio swala la kuwafurahisha CCM, bali ni swala la waTanzania wote.

Hakuna sababu ya kuwepo msuguano wowote katika hili. Na ni rahisi sana kuligeuza hili lionekane kuwa baya upande wenu katika macho ya waTanzania kama hamtachukua tahadhari.

Lissu atakaribishwa sana wakati wowote na popote na umati wa waTanzania wote wenye mapenzi na nchi yetu.

Ni kiasi cha kupanga tu vizuri mapokezi hayo.
 
Lissu wala hayumo kufikiriwa kuwa mgombea chadema. Mark my word atashindwa ama atakatwa jina
 
Hizi ni salamu kwa wenye usafiri wasitumie usafiri kwani mapokezi yawe ni kwa mguu. Siku hiyo shughuli zitasimama kutokana na umati wa maelfu ya watu. Hivyo napendekeza muheshimiwa abebwe begani akiwa kwenye kiti cha ufalme mpaka makao makuu ya chama.

Historia inakwenda kuandikwa upya
Makao makuu ya kupanga kwa baba mkwe, pumbffffff zenu.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Ni vyema hekima na busara ikatumika katika hili, Tayari Mh Rais ameshatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba ni vyema watu wote tukaheshimu mamlaka wakati huu wa majonzi ya Mzee wetu Mkapa.

TL anaweza kusitisha safari yake na akasogeza mbele tarehe kama kuna haja ya kupokewa kwa ndelemo na vifijo, lakini pia anaweza kushuka tu kimyakimya akaendelea na harakati zake..
 
Anaporudi ni kuwa na angalizo tu kuhusiana na muskatabali wa lolote linaweza kutokea dhidi yake, hii ni Afrika.
 
Mwanasiasa wa upinzani nchin Tanzania Tundu Lissu amesema anatarajia kurudi nchini humo Julai 28.

Lissu ametangaza nia ya kugombea urais kupitia chama chake cha CHADEMA Oktoba mwaka huu. Mwanasiasa huyo kwa sasa yuko ughaibuni ambapo alienda kupata matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017.

Akizungumza leo katika mkutano unaoendelea kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na taasisi ya The Resistance Bureau, Lissu amesema ameshakata tiketi ya ndege na watanzania watarajie kumpokea Julai 28.

Akijibu swali kuhusu kama anahofu kuwa anaweza kuzuiwa kuingia nchini mwake, Lisu amesema: ''Sina sababu ya kuamini kuwa nitazuiwa kurudi nyumbani, mimi si mhalifu niliondoka nje ya Tanzania nikiwa sina fahamu, nilishambuliwa kwa risasi mara 16 na watu ambao mpaka sasa hawajakamatwa hivyo ninarejea nyumbani kuikabili serikali iliyosema kuwa haina hatia katika tukio hilo la jaribio la kuniua, kunizuia kutadhihirishia dunia kuwa ilihusika na shambulio la mwaka 2017 kama nilivyosema sina sababu ya kuamini kuwa nitazuiwa kurejea nyumbani''. Alieleza Lissu kwenye mkutano huo.
Mbona mnatuchanganya mara tarehe 27 mara 28, tushike lipi maana tuna mzuka wa kwenda kumpokea na kumsindikiza Central Police
 
Back
Top Bottom