Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,289
2,000
Mwanasiasa wa upinzani nchin Tanzania Tundu Lissu amesema anatarajia kurudi nchini humo Julai 28.

Lissu ametangaza nia ya kugombea urais kupitia chama chake cha CHADEMA Oktoba mwaka huu. Mwanasiasa huyo kwa sasa yuko ughaibuni ambapo alienda kupata matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017.

Akizungumza leo katika mkutano unaoendelea kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na taasisi ya The Resistance Bureau, Lissu amesema ameshakata tiketi ya ndege na watanzania watarajie kumpokea Julai 28.

Akijibu swali kuhusu kama anahofu kuwa anaweza kuzuiwa kuingia nchini mwake, Lisu amesema: ''Sina sababu ya kuamini kuwa nitazuiwa kurudi nyumbani, mimi si mhalifu niliondoka nje ya Tanzania nikiwa sina fahamu, nilishambuliwa kwa risasi mara 16 na watu ambao mpaka sasa hawajakamatwa hivyo ninarejea nyumbani kuikabili serikali iliyosema kuwa haina hatia katika tukio hilo la jaribio la kuniua, kunizuia kutadhihirishia dunia kuwa ilihusika na shambulio la mwaka 2017 kama nilivyosema sina sababu ya kuamini kuwa nitazuiwa kurejea nyumbani''. Alieleza Lissu kwenye mkutano huo.
 

nyaiya01

Member
Apr 26, 2020
18
45
Nahisi kuja kwake kutakuwa ni uthubutu wa kuwania huo urais. Issue ni hadi afanikiwe kuchukua ile form kubwa pale NEC.
 

nG'aMBu

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
1,546
2,000
Mh, hapa serikali ya jiwe iwe makini na Tundu Lisu, wasimletee ujinga inawezekana kuja kwako ukawa mtego kwa serikali hii mbovu mbovu isifuate misingi ya utawala bora
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
52,404
2,000
Toka aanze kuahidi kurudi hii ni mara ya 5 anageresha tu
Lissu anapima upepo tu harudi ng'o
Chadema haeamtaki agombee,ACT wanamtaka Membe,labda arudi NCCR alipofukzwa
Mataga tulia Lissu anakuja tarehe 28 na ndiyo mgombea, labda kama mtammiminia mvua ya njugu tena.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,163
2,000
Toka aanze kuahidi kurudi hii ni mara ya 5 anageresha tu
Lissu anapima upepo tu harudi ng'o
Chadema haeamtaki agombee,ACT wanamtaka Membe,labda arudi NCCR alipofukzwa

Matamanio yako ni Membe kuwa mgombea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom