- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Ni upi uhalisia wa video hizi mbili ambazo nafikiri zimetokana na mahojiano ya Jambo TV na Tundu Lissu kuwa amekiri kuwa migogoro ndani ya chama ndiyo chanzo cha kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
- Tunachokijua
- Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba 27, 2024 ulitoa nafasi kwa watanzania waliokidhi vigezo na kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji. Uchaguzi huo ambao ulikumbwa na matukio mbalimbali yaliyolalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa sehemu ya mambo yaliyokwamisha uchaguzi huo kuwa huru na wa haki. Baada ya uchaguzi kumalizika, Siku moja baadaye waziri wa nchi ofisi ya Rais na serikali za mitaa Mohamed Mchengerwa alitangaza matokeo ya uchaguzi ambapo Chama tawala kiliibuka na ushindi mkubwa wa asilimia 99.10%
Kutokana na uchaguzi huo televisheni ya mtandaoni ya Jambo TV ilirusha matangazo mbashara baaza ya zoezi la uchaguzi kukamilika ambapo matangazo hayo yalihusisha waandishi na wanasiasa kutoka vyama mbalimbali wakitoa tathmini dhidi ya namna ambavyo uchaguzi ulifanyika. Tundu Lissu alikwa ni mmoja kati ya waliohojiwa ambapoKumekuwapo na upotoshaji ulioibuka kutokana sehemu ya matangazo hayo aliyohojiwa dhidi ya masuala mbalimbali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Je ni upi uhalisia wa kauli inayodaiwa kuwa Lissu amekiri kuwa mgogoro ndani ya CHADEMA ni sababu ya kushindwa uchaguzi serikali za mitaa?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa kipande cha video hiyo kimepotoshwa kutoka kwenye uhalisia wake kwa kukatwa sehemu ndogondogo na kuunganisha hatimaye kupoteza maana halisi ambapo Lissu hakukiri kwamba mgogoro ndani ya CHADEMA kuwa sababu ya kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Kama kama unataka kusema kwamba tumeshindwa kwa tofauti zetu ndani ya vyama vyetu, basi kama ingekuwa hivyo CCM wasingehitaji kutumia majeshi kwa kiwango walichotumia, CCM wasingehitaji kutumia mfumo mzima wa serikali, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wafanyakazi wao wote, kuhakikisha kwamba wanaharibu uchaguzi huu, sababu ingekuwa tofauti ni ndani ya vyama vyetu haya ambayo yametokea leo na ambayo yalitokea mwanzo wakati wa mchakato wa uchaguzi yasingetokea, ukweli ni kwamba pamoja na tofauti zetu ambazo nakubali, ukiangalia wagombea tulioweka mwaka huu ukilinganisha na tulioweka 2019, hata ukiuliza nguvu ilikuwa kiasi gani kuhakikisha wagombea walioenguliwa wanarudishwa kwa mfano, kulikuwa na matatizo kama hayo, lakini hadithi kubwa za uchaguzi huu sio mgawanyiko ndani ya vyama vya upinzani, hadithi kubwa ya uchaguzi huu ni Samia amefanya kama alivyofanya Magufuli 2019 na 2020” Lissu alisema.
Tazama video halisi inapatikana hapa tazama kuanzia 01:27:20 mpaka 01:29:39
View: https://www.youtube.com/live/ClBKnAxUpG4?si=6V4EBgVxfl3CDRJo
Je ni ipi kauli halisi ya Lissu baada ya kuulizwa kama mpasuko au kutokuelewana kwa viongozi ndani ya chama kama haiwezi ikachangia kwa kiwango kikubwa nguvu ya chama kushuka?
JamiiCheck ilibaini kuwa kipande cha pili cha video kilikatwa sehemu ndogondogo na kuunganishwa hatimaye kutengeneza muunganiko uliotofautiana na uhalisia hatimaye kupotosha.
Akijibu swali liloulizwa na Mwandishi Edwin Odemba juu ya mpasuko au kutokuelewana kwa viongozi ndani ya chama kama haiwezi ikachangia kwa kiwango kikubwa nguvu ya chama kushuka Lissu alisema idadi ya wagombea waliowekwa na Chama chake mwaka huu ni ndogo ukilinganisha na ile ya uchaguzi wa miaka mitano iliyopita akitaja kuwa hilo ni tatizo ndani ya chama huku akisema hiyo peke yake haielezei yaliyotokea katika uchaguzi huu akiongeza kuwa pengine kosa lao kubwa ni kumwamini Rais Samia na serikali yake.
Tazama video halisi hapa kuanzia 01:30:44 mpaka 01:31:57
View: https://www.youtube.com/live/ClBKnAxUpG4?si=3RhbevciRmHfZKts