Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aliwahi kuisaidia nini Tanzania? Mwenye uelewa atuelezee

Nyumbu ni CCM hata mbugani nyumbu ni wengi kama walivyokuwa wanaccm ambao hukariri zidumu fikra zisizo sahihi za mwenyekiti wa CCM
Minyoo Minyoo Minyoo Minyoo Minyoo

Nyumbu akipata minyoo anakuwa goigoi anaweza kuliwa hata mbwa.
 
Acha uvivu kaangalie video zake za ubunge. Utajua yeye kama mtunga sheria alitoa mawazo gani kwenye sheria za Ardhi, madini, elimu n.k. Wabunge si Kazi yao kujenga Barbara, reli.... Wenyewe ni watunga sheria. Uzuri wananchi wengi hata wa kijijini wanajua hilo. Usimwongelee Nyerere wakati wake Tanzania ilikuwa masikini sana
 
Uzwazwa ulionao ndio utakaufanya utakanwe mpaka uwakumbuke wazee wako kijijini, yaani mpaka leo hujajua umuhimu wa lissu? Kwanini hujiulizi kwanini walitaka kumuua mchana kweupe!?
Mtu hata ada za shule anaomba omba ovyo na kuchangisha kila leo sasa mtu huyo unataka asaidie nini,
ajisaidie mwenyewe kwanza kukidhi mahitaji yake na majukumu ya kifamilia yaliyo muandama kila kukicha.
 
Yaani unanukuu maneno ya mwalimu afu unapingana nayo.
Unasema mwalimu alisema tuchague kiongozi atakaye tusaidia kutuletea maendeleo afu we unauliza Lissu amelisaidia nini taifa.
Au ujui hata kuangalia nyakati?
Kama ulimwelewa mwalimu nenda msikilize Lissu ili ujue atalisaidia nini Taifa.
Msipende kunukuu maneno ambayo hata hamuyaelewi
 
Watu wamechoka na maisha magumu hakuna ajira, pesa ngumu, uhuru mdogo, na sinema la kihindi kuwa uchumi wa kati wakat wananchi wako choka mbaya.

unawezavitu vya miaka 50 mbele wakati utakuta usha kufa, sasa ulikuja duniani kufanya nn au kuishi kwa mateso
 
Yeye hajawahi kuisaidia nchi kama nchi bali amesaidia sana wananchi wanyonge tunaomfahamu toka miaka ya 1992,kwenye kuwapigania wachimbaji wadogo wa madini hadi anaingia bungeni bado aliwapigania sana!! Yeye ana asili ya uana harakati ndio maana toka miaka hiyo yeye na serikali ni matatizo tu, wanyonge ndio wanaufahamu umuhimu wake. Achana na hao wanaojiita watetezi wa wanyonge baada ya kupata madaraka!!
Inaelekea mleta uzi tangu atoke shule ya kata hajasomea hata kitabu kimoja wala gazeti. Kila siku mtandaoni tu anawangalia akina Wema Sepetu na Nandy! Unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyu. Anyway msameheni to. Angali kijana mdogo.
 
Umewlewa lakini, huyo mtu wenu hafai kabisa,
Kama angekuwa ana nia ya kuwa raisi angeepuka kutetea kesi zinzoibana nchi, lakini yeye akawa ananufaisha tumbo lake tu.
Sasa masuala ya kuongoza nchi awaachie wenye machungu na nchi
Kama kesi ipi?
 
Nimekusamehe kwa kuwa umejitanabahisha kwamba ulikuwa mtoto mdogo mwaka 1995. Ngoja nikueleze mambo matatu makubwa ambayo Tundu Lissu amelifanyia taifa hili:-
1. Wakati wa awamu ya 3 ya Mkapa Tundu Lissu ndiye alipinga vikali uanzishwaji wa shamba la kufuga prawns kwenye bonde la mto
Rufiji. Endapo shamba hili lingeanzishwa lingeharibu mazingira kwa kiasi kikubwa. Wakati TL anafanya jitihada hizi alikuwa hata
hajawa mbunge. Huyo mtu wako unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba uharibifu wa mazingira hayo ulikuwa haumhusu!
2. Kuanzia mwaka 2005 alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza hadi 2015, Tundu Lissu ndo alipinga vikali bungeni kuhusu
kupitishwa na kuwekwa saini mikataba mibaya ya madini ambayo ilikuwa inafanya Tanzania kama shamba la bibi. Wakati huo wabunge
wa CCM walikuwa wanasema 'ndiyoooooo' - wakati mikataba hiyo inapitishwa. Hata huyo unayemshabikia alikuwa bungeni lakini alikuwa bubu. Kwa taarifa yako, yale yote Tundu Lissu aliyokuwa anayepigia kelele ndo ambayo Rais Magufuli ameyachukua na kuyafanyia kazi.
3. Tundu Lissu ndo ambaye alipiga kelele bungeni kuhusu ufisadi mkubwa uliofanywa na viongozi wa CCM kuhusu EPA, Kagoda, Meremeta,
Deep Green Finance, n.k. Wakati anaibua ufisadi huu, huyo unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba ufisadi huo haumhusu.
Nadhani sasa kijana unaweza kuona jinsi ambavyo Tundu Lissu alivyo mzalendo, mwenye uchungu na nchi yake.
Hitimisho: Si lazima uwe Rais ndo utoe mchango kwa nchi yako. Hapo nimekuonyea kwa ufupi tu jinsi ambavyo Tundu Lissu amelisaidia
taifa lake. Naamini sasa umemwelewa huyu mpambanaji na utampa kura ili awe Rais wa JMT, au siyo?

ILA hao unaowapa ujumbe hawasikilizi kitu mpaka kitokee kwa POLEPOLE.

Kikishatamkwa na Chakubanga ni msahafu; hawachuji, hakuna yeyote kati yao anaefikiri wala kutafakari.

Wao wanaimba nyimbo zilezile kama watoto wa chekeachea, hakuna aliewahi kuchimbua malumumba wajameni.

Augustino Mrema akiwa Mwenyekiti wa NCCR pamoja na Lissu akiwa NCCR na Mwanasheria mwenzake wa LEAT/NCCR walipoanza kusakamwa na serikali awamu ya tatu, waliwahi kukimbilia kea Askofu Pengo kukwepa mkono wa Polisi.

Yote haya Jiwe anayajua vizuri sana, kwani alikuwamo kwenye Bunge lililopitisha sheria mbovu za madini, huku wabunge wa upinzani Lissu na wenzie wakatolewa nje Zitto akisimamishwa vikao. HATA sijui JIWE anapata wapi ubavu wa kumuita Lissu msaliti.Uzalendo wake ni upi?

YOTE yapo kwenye habari na records za bunge/ansard waende na huyo POLEPOLE, Bashiru na hata Kabundi wakasome waje wasimame watukosoe
 
Nakumbuka msaada mkubwa wa lissu Tz ni kuweza kuchongea nchi yetu kwa mabeberu
 
Back
Top Bottom