Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alipongeza jeshi la polisi kwa kutenda haki katika mikutano yake ya kampeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,761
Mgombea urais wa JMT kupitia Chadema Tundu Lisu anasema jeshi la polisi limefanya kazi nzuri katika maeneo yote aliyopita na kufanya kampeni.

Lisu anasema polisi wasisingiziwe kwa lolote kwa sababu wanafanya kazi yao vizuri.

Source Ayo tv.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mgombea urais wa maccm hana tofauti na gari la kubebea mkaa.
Tripu moja shamba kufuata mkaa, Tripu ya pili gereji

Unaposhabikia dhulma miaka 5 na kushabikia watendaji wa dhulma; na ukikalia kimya maiti kuokotwa kwenye viroba, wananchi kutekwa na kupotea, watu kubambikiwa kesi, biashara za watu kufungiwa - basi ujue umekosa uhalali wa kuongelea amani
 
TL anacheza mind games na vyombo vya Ulinzi na Walimu ambayo ndio wahesabu kura.

Anawaaminisha Polisi kama ana imani nao na yuko nao pamoja ili likija kutokea wawe na 2nd thought.
 
Chadema Wana uadui na taasisi zote hapa nchini,

Anachokisema lisu hakina tofauti na namna anavyoisifia mahakama inapotoa maamuzi yanayoipa faida upande wake ila pale maamuzi yakiwa kinyume cha matarajio yao utasikia jaji au hakimu anafuata maelekezo toka juu.

Huyu jamaa sio wa kumuamini ni mbinafsi na hapo anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, wakifanya kinyume na matarajio yake utasikia wanafuata maelekezo toka juu.

Hakuna jipya hapo ni muendelezo wa tabia zao za kila siku.
 
Sasa kama wanataka kuongezwa mishahara na kupewa uniform nzuri kwani wasio na adabu
 
Ni kitu kizuri kupongeza kazi nzuri ya Polisi, kwa kweli wamekuwa waungwana. Wawe makini wasiruhu watu wasiojulikana kuvaa sare za Polisi na kunajisi Jeshi la Polisi.
 
Chadema Wana uadui na taasisi zote hapa nchini,

Anachokisema lisu hakina tofauti na namna anavyoisifia mahakama inapotoa maamuzi yanayoipa faida upande wake ila pale maamuzi yakiwa kinyume cha matarajio yao utasikia jaji au hakimu anafuata maelekezo toka juu.

Huyu jamaa sio wa kumuamini ni mbinafsi na hapo anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, wakifanya kinyume na matarajio yake utasikia wanafuata maelekezo toka juu.

Hakuna jipya hapo ni muendelezo wa tabia zao za kila siku.

Kada wa chama Dola kulichopoteza ushawashi,mnatumia malori na mabasi kuwasombea wanafunzi wa chekechea,shule za msingi na sekondari kwenye matamasha yenu ya wasanii. Taratibu mtapoteza ushawishi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hivyo kushindwa kuvitumia kwa maslahi yenu.
 
Lazima wamtii amiri jeshi mkuu wao ajaye. Kwa kifupi kwasasa serikalini hakuna mwenye uhakika nani atakua boss no. 1 novemba, ni lazima kuwa mtiifu na mtenda haki kwa wote.
 
Kweli kampeni hizi polisi nao wanaenda sambamba na kimbunga cha kokoto!

Wanasubiri Lisu aapishwe walipwe mara dufu kama watakavyoongezewa mshahara wafanyakazi wengine wote wa serikali na wale wa sekta binafsi

😀😀😀😀ulisikia wapi !
 
Mgombea urais wa maccm hana tofauti na gari la kubebea mkaa.
Tripu moja shamba kufuata mkaa, Tripu ya pili gereji

Unaposhabikia dhulma miaka 5 na kushabikia watendaji wa dhulma; na ukikalia kimya maiti kuokotwa kwenye viroba, wananchi kutekwa na kupotea, watu kubambikiwa kesi, biashara za watu kufungiwa - basi ujue umekosa uhalali wa kuongelea amani
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀we jamaa unawaza mbali
 
Kule Twitter kuna habari kamili juu magu na Afya yake ndiyo maana campaign zake zinaenda Kwa kusuasua
 
Back
Top Bottom