Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akishinda Urais, Nchi imeshinda, Afrika imeshinda

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Habari za Jioni wana Nzengo!

Sasa iko wazi kutokana na umahiri, uwezo, nia na ari aliyonayo Mh Tundu Lissu Mgombea wa Chama cha Demokrasia na maendeleo ktk ngazi ya Urais atashinda uchaguzi huu.

Mbingu na Ardhi vimethibitisha hilo. Kwani kila anapopita ni shangwe na vigelegele kwa kuwa ni wazi Tundu akishinda ni Tanzania imeshinda.

Tundu Lissu akishinda ni watanzania wameshinda kwani wataondokana na utawala kandamizi wa kutunga sharia za kikoloni, kujilimbikizia mali, utawala usiozingatia sheria, ufujaji wa mali za umma na upendeleo kwenye ngazi mbali mbali za maamuzi ikiwemo mahakama na bunge.

Ni tanzania itakuwa imeshinda kwani ana dhamira ya dhati ya kutokomeza umaskini na changamoto zingine za maisha. Uwezo wake na historia yake havina shaka juu ya hili.

Ukifatilia namna Tundu Lissu alivyokuwa toka utoto wake hadi leo hajawahi kupita njia nyepesi kwenye mafanikio yake. Kila alipopita alikutana na vizingiti na njia yenye mawaa tele. Hata hivyo hakuwahi kukata tamaa siku zote amekuwa mshindi.

Mifano iko mingi, amewahi kushitakiwa mahakama mbalimbali kwa makosa mbali mbali zaidi ya 1000 lakini hata moja hakuwahi kukutwa na hatia.

Amewahi kusimamia kesi za wanyonge zaidi ya 500 hata moja hajawahi kushindwa kusimamia haki zao.

Tundu amewahi kushtakiwa ktk kesi ya ushindi wa ubunge wake alipokata Rufaa akalejeshewa ubunge wake.

Lissu aliwahi kupigwa risasi takribani arobaini, chini ya nusu yaani 16 tu ndio zilifanikiwa kufika kwenye mwili wake huku zingine ziki- repel. Hata hizo 16 hakuna hata moja iligusa cephalo body (kichwani) na hakuna hata moja ilileta kifo kwake. Wakati hata tembo au Mbogo wanyama wenye mguvu na mwili mkubwa wakipigwa risasi moja tu hawaamki tena.

Tundu Lissu ilikadiriwa kuwa hataweza kugombea kutokana navizingiti alivyokwisha andaliwa kumzuia asipate fursa hiyo. Pamoja na NEC, Mahakama, polisi na idara zingine za dola kutia jambajamba kila mahali mwisho wa siku alifanikiwa kupata wadhamini elfu 2000 alioweza kuonana nao physically uso kwa uso nchi nzima ndani ya wiki moja(ndio mgombea pekee alitimiza vigezo vya neck (sorry NEC)

Ikafika siku ya kurejesha fomu alizinguliwa kiasi ikatarajiwa huenda NEC pale dodoma wasipokee fomu zake, hadi jioni sana saa 12 ndio zikapokelewa.

Siku ya kupokea matokea ya NEC Lissu alikalishwa ofsi za NEC tar 26 August hadi saa nne usiku ili hali wagombea wengine Lipumba na Magufuli ilichukua dakika chini ya 30 kupitishwa.

Hata hivyo mambo hayakuishia hapo. Polisi na Mkurugenzi waliendelea kuvurumusha vitisho vya hapa na pale ili kukatisha tamaa hatima yake kadri walivyo mzuia ndivvyo nyota yake ilizidi kung'ara

Kwa sasa wooote nchi nzima ikiwemo na vyombo vya dola vimeshakubali yaishe. Maana ameshashinda kabla ya uchaguzi.

Nini tufanye!! Tusiogope eti hatatangazwa! Hicho kitu hakipo. Tujiandae ushindi Mgumu sana october 28.

Ebwanaeeh! Hakuna goli tamu kama la kuhangaikia na kukaba.

Chadema Safiiiiiiiiiii!

Tundu Lissu akishinda Nchi Imeshinda Afrika imeshinda.

Nyerere wa sasa amerudi

images (3).jpeg
 
Hata Libya walifanya mabadiliko nini wameambulia?

Binadamu ni binadamu tu, asili yetu ni moja
Yeyote anaweza kutuvusha au kutuangusha
 
Takbirr
Allah Akbar
Inn shaa Allah Mara hii tunakwenda kupata rais muadilifu ambae hata watesa mashekh wetu na watanzania kwa ujumla
Ewe Mola wa haki tunakuomba umlinde huyu kiongozi wetu muadilifu dhidi ya yule katili Pombe na genge lake

Ewe Mola wa maajabu onyesha maajabu safari hii lissu ashinde dhidi ya yule katili Pombe Tumechoka kuona damu
Amiin yarabi Amiin
 
Takbirr
Allah Akbar
Inn shaa Allah Mara hii tunakwenda kupata rais muadilifu ambae hata watesa mashekh wetu na watanzania kwa ujumla
Ewe Mola wa haki tunakuomba umlinde huyu kiongozi wetu muadilifu dhidi ya yule katili Pombe na genge lake
Ewe Mola wa maajabu onyesha maajabu safari hii lissu ashinde dhidi ya yule katili Pombe Tumechoka kuona damu
Amiin yarabi Amiin
Jiachie Shekhe mkombozi karudi sio mwingine ni yuleyule Muadilifu Tundu Lissu
 
Hicho kibabu cha Lumumba kitafute kazi nyingine ifikapo tarehe 28/10/2020 Watu wenye Akili tunataka Haki Uhuru na Maendeleo ya watu. Kikigomea ikulu hicho kibabu kidhaifu tutakifurumusha kwa mawe tuu na kukikabidhi I.C.C
 
Takbirr
Allah Akbar
Inn shaa Allah Mara hii tunakwenda kupata rais muadilifu ambae hata watesa mashekh wetu na watanzania kwa ujumla
Ewe Mola wa haki tunakuomba umlinde huyu kiongozi wetu muadilifu dhidi ya yule katili Pombe na genge lake
Ewe Mola wa maajabu onyesha maajabu safari hii lissu ashinde dhidi ya yule katili Pombe Tumechoka kuona damu
Amiin yarabi Amiin

Unavyoomba ndivyo wanavyoomba, hii ngoma haichezwi kivivu.
 
Back
Top Bottom