Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akifanya hili kwa Watanzania anashinda Urais asubuhi na mapema

manafyale

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
277
158
Aombe msamaha Watanzania kwa ile biti ya hatari aliyoichimba maana Watanzania wote kutoka katika vyama vyote na wasio na vyama, haja kubwa ilikuwa inagonga nguo za ndani kwa hofu.

Watanzania wengi waliingiwa na hofu kuu hasa ukinzingatia hatuna uzoefu wala mazoea ya kuvamiwa kivita kwani hata ile vita ya Uganda kumwondoa Fashisti Idiamini Kaidada, ile vita ilipigwa upande wa Uganda pekee hivyo kwa Tanzania wanaokumbuka vita ni ile ya Mkwawa, Kinjekitile na wengine

Lissu alichimba biti hiyo wakati wa makinikia, yale makontena yaliyokamatwa kule bandarini yaliokuwa na mchanga wa kujengea nyumba. Lissu ndiyo wakati ambao aliongea sana kuliko wakati wowote tangia aingie katika siasa za TZ.

Alisema, namnukuu: "Kama Rais Magufuli hata yaachia hayo makontena ya mchanga na kuyaruhusu yaende kwa wazungu hakika tutapigwa kama Gadafi na tutachakazwa ndani ya masaa 48 tutakuwa tumekwisha"

Alienda mbali zaidi na kusema kuwa Tume ya Profesa Osolo na Profesa Mluma zilikuwa Rabishi yaani takataka. Nakumalizia sheria za kimataifa pia zitatubana kwani kule tutanyolewa na chupa bila maji na mwishoni kuvamiwa kijeshi na NATO. Huyo ni mgombea urais kupitia Chadema Tundu Antipas Lissu.

Sasa kwa kuwa hadi leo hawajatuvamia ila walikuja omba msamaaha na badala yake wakalipa hata kiduchu. Lissu aombe samahani tumpe miaka miaka 5 na yeye akafanye yake, au siyo?
 
Mkuu unayo hiyo video clip akiongea maneno hayo kama ulivyom qoute? Please hebu share na sisi hapa jukwaani maana wengine ni kina Tomaso.
 
Alisema, namnukuu: "Kama Rais Magufuli hata yaachia hayo makontena ya mchanga na kuyaruhusu yaende kwa wazungu hakika tutapigwa kama Gadafi na tutachakazwa ndani ya masaa 48 tutakuwa tumekwisha"
Na jiwe alishayaachia yale makontena baada ya tume iliyokurupuka kufuatilia na kudai mchanga una thamani ya trillioni 120 lakini hadi sasa jiwe ameshindwa kufuatilia kulipwa chochote. Kwa hili atawajibika October.
 
Watanzania ni watu ambao tumesitaraabika sana, hata Kama ukimuudhi mtu anaweza akaja kwenye kamati zako katika maandalizi ya sherehe yako, siku ya sherehe akahudhuria kama mtazamaji tu.
 
Na jiwe alishayaachia yale makontena baada ya tume iliyokurupuka kufuatilia na kudai mchanga una thamani ya trillioni 120 lakini hadi sasa jiwe ameshindwa kufuatilia kulipwa chochote. Kwa hili atawajibika October.
Tuliahidiwa Noah kila mtanzania.. Yale makinikia tuliambiwa yalikuwa na dhahabu inayojaza malori 27 ya tani saba...

Proffeserial rubish kutoka kwa maprofesa wetu wasomi. Si haba lakini Bwana yule akawazawadia vyeo waachane na kupambana na vumbi la chaki
 
Back
Top Bottom