Tundu Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
maxresdefault.jpg

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anaandika Josephat Isango.

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.

Mwandishi alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.

Saanane ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa-Freeman Mbowe alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.

Wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakimsaka kiongozi huyo bila mafanikio yoyote jambo ambalo limeendelea kuzua hofu kama yu hai ama ameuawa.

Tarehe 14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam akiomba vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.

Chanzo: Mwanahalisi
 
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anaandika Josephat Isango.

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.

Mwandishi alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.

Saanane ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa-Freeman Mbowe alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.

Wafuasi wa Chadema wamekuwa wakimsaka kiongozi huyo bila mafanikio yoyote jambo ambalo limeendelea kuzua hofu kama yu hai ama ameuawa.

Tarehe 14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam akiomba vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo
.
Anaisaidia polisi?
 
Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.
Aonyeshe ile SMS aliyoutangazia ulimwengu ilikuwa inamtisha Ben, zama za uzushi zimepita..na kwa hili akae tu jela hadi pale atakapoleta ule ujumbe kwa ushahidi la sivyo ni mzushi na ashtakiwe kwa habari za uongo.
 
Tawire, afande Faru John
 
Hata mimi ningekuwa polisi basi lissu ningelala naye mbele yeye amepata wapi meseji aliyo tumiwa ben saa nane
 
Back
Top Bottom