Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aijibu NEC kutishia baadhi ya wagombea "wanaohatarisha amani" kwenye kampeni zao

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
å Ni majibu ya kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dr. Wilson Mahera Charles aliyoitoa jana alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari.

å Kwamba, baadhi ya wagombea katika mikutano yao ya kampeni wanakiuka kanuni na maadili ya uchaguzi mkuu wa 2020.

å Na kwamba, tume inaweza kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwazuia kuendelea na kampeni zao.

å Tundu Lissu akiwa Mbozi leo tarehe 16/9/2020 akichanja mbuga kuendelea na mikutano yake ya kampeni, kabla ya kuwahutubia wananchi alitumia dakika 12 kuijibu NEC juu ya kauli yake hii kupitia kwa mtendaji wake mkuu, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dr Wilson Mahera Charles.

å Katika kujibu, Tundu Lissu akaikaripia vikali NEC kuwa ndiyo mkiukaji mkubwa wa KANUNI na MAADILI hayo ya Uchaguzi mkuu 2020.

å Akataja makosa matano (5) ya ukiukaji KANUNI na MAADILI yanayofanywa na mgombea Urais wa CCM, ndg John Pombe Magufuli huku NEC wakiwa kimyaaa.

Tazama video hii

 
å Ni majibu ya kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dr Wilson Mahera Charles aliyoitoa jana alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari...
Lissu ni chaguo letu sio yule wa kuleta wanafunzi na wasanii kuaminisha anapendwa

Ndio maana anakuwa mkali na kutufokea wananchi mara nina sura mbaya mara mtajuta,

Mbona lissu kajawa furaha na amani?

Ni kwasababu anapendwa na watu bila kutumia nguvu fake.

Ni yeye
tapatalk_1600270550830.jpeg
tapatalk_1600270544402.jpeg
IMG_20200916_081205.jpeg
 
Wataelewa tu,kanun znavunjwa kila kukicha na bwana yule wala huwackii wakinyanyua mdomo
Lissu ni saiz yake,makavu ndiyo anayaelewa-shida Lumumba hawajawahi kufikiria siku moja mtu atatokea na kuwafungua macho wananchi kwa style ya lissu ya kuhutubia;Lissu ana skills ya kufikisha taarifa ngumu kwa mtu wa chini kwa jinsi rahisi ambayo ataielewa.

Mpaka uchaguzi uishe Mzee mkubwa credibility yake itakuwa imepungua mno kwa jinsi Lissu anavyo yafumbua mambo yake yake ya kificho hadharani sababu wananchi walikuwa wanamvumilia wakiamini hana scandal ila mambo ni tofauti
 
Duh,mbona kawavua nguo NEC.aibu iliyoje kama ndo Tanzania viongozi wenye dhamana akili zipo hivi!.


Kumbe Lisu yupo sahihi,kitakachotokea basi atakae beba mzigo in TUME.

Jamani watu walishaelimika Ccm iache vimbwanga.huu mwaka wa Shetani aliyeruka kiunzi cha kifo.

Dah,aliyesema upinzan umekufa nadhani yeye ndo moyo umeshakufa.

Nipo bize na bongofreva kwenye siasa sipo.amen
 
å Ni majibu ya kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dr Wilson Mahera Charles aliyoitoa jana alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari....

Mh. Tundu Lisu, andaa mapingamizi kwa:-

KAULI ZA VITISHO (Mkichagua UPINZANI MTAJUTA)

Ahadi za utendaji (Tatajenga Hospital au Shule)

Agizo kwa Mtendaji wa TANROAD/TARULA la kuanza Ujenzi wa barabara kule Sengerema na pesa za ujenzi AULIZWE Mgombea wa URAIS.

Kuongozana na Watendaji (Watumishi) wa UMMA na MAGARI YA UMMA kwenye KAMPENI.

KUMTUMIA WAZIRI MKUU KUZUNGUKA NCHI NZIMA AKIOMBA KURA KWA MGOMBEA URAIS WA CHAMA KINGINE.
 
Back
Top Bottom