Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Bado anatafuta kura za huruma?
kibaraka wa mabeberu hapewi nchi na watanzania, hata asimulie mwanzo mwisho wa tukio lake mpaka anarudi.
Kura za huruma kivipi? Kwani watanzania ni wajinga kama wewe? Watanzania watampa kura kwa sababu hakujipiga risasi mwenyewe bali wewe na kikundi chako cha kishetani ndiyo mlimpiga risasi, CCM acheni kuwaita wanaume wenzenu mabeberu kwani nyinyi CCM ni mbuzi jike?
 
Hii ni kashfa kubwa sana kwa Bw. Magufuli na serikali yake, ingekuwa kwenye nchi zilizostaarabika hangekuwa tena na nguvu za kuweza kusimama na kuomba kura, angelazimika tu kujiuzulu mara moja.

Lkn kwa kuwa ni huku uswahilini ambako rais anajiona Mungu mtu anajifanya kukomaa tu lakini kwa kuwa madai hayo ni ya ukweli hakuna anachoweza kumfanya huyo "mhanga" wake, itabidi tu ale pini japo sifa yake tayari imekwisha haribika kuwa yeye ni muuaji...!!! Very shameful for a Head Of State.

Mkuu kwani Lissu ndio msaliti na aliyekuwa ana tuhujumu?
 
Suppose uwe hujàelewa vibaya, yaani uwe umeelewa kwa usahihi kabisa....

Na suppose kuwa, Tundu Lissu ni msaliti wa nchi....

MASWALI HAYA NI MUHIMU SANA:

å Rais Magufuli anapata wapi uhalali wa kuamuru RAIA wake auwawe kinyume cha sheria kwa tuhuma za juu juu tu za eti "msaliti wa nchi???"

å Sheria zetu za nchi zinasemaje kuhusu hiki "the so called" - USALITI WA NCHI? Je, zinasema Rais ataamuru na kutuma kundi la majambazi akiwa amewapa na pesa na bunduki kumuua huyo mtu ambaye kwa vigezo vyake Rais amempa jina la "msaliti wa nchi??"

NI HIVI NDUGU YANGU;

• Kama yeye mwenyewe Rais Magufuli atajitokeza na kujitetea kwa hoja hii, basi atakuwa "mjinga" sana na kamwe hawezi kuchomoka kuepuka kifungo cha maisha gerezani....!!

• Na vivyo hivyo, kama wafuasi wake mnamtetea kwa hoja hii ya "kijinga" kabisa, basi hamtamsaidia kumwepusha na adhabu ya "kujaribu kuua kwa kukusudia" kamwe....!!

Kuwa Rais wa nchi ama kuwa na kinga ya "kutoshitakiwa" siyo ishu. Ukiua na wewe lazima uuwawe tu. Remember, KARMA IS A BITCH...!

USHAURI:

Magufuli ajitokeze hadharani na aweke sawa kauli yake.....

Ajitokeze na aseme, kauli yangu hiyo ilikuwa "just by coincidence", kwamba, nilisem vile na ikatokea siku hiyo hiyo niliyotamka Tundu Lissu akashambuliwa.....!!

Ila ukweli ni huu: kuwa, kauli yangu haikuwa ikim - refer Tundu Lissu kabisa. Na sikutoa amri yoyote auwawe....

Atoke sasa hadharani aseme hivyo japo ni hakika kuwa hakuna mtu timamu kiakili atamwelewa na kumwamini....

Else, asidhani kuwa MOYO WA DHAMBI YA UUAJI alionao HAUTAHUKUMIWA....

KINGA YA URAIS ya kutoshitakiwa haitamsadia. Natural justice haizuiwi na "kinga ya Rais kutoshitakiwa". Itapenya tu na lazima kila mtu alipie matendo ya dhambi zake....!!
Unauthibitisho wowote au ni bendera tu? Sisi ni wa JPM tu.



MAGUFULI4LIFE.
 
Kwani wewe bado tu hujamuelewa Jiwe?

Ni bingwa wa kutunga uwongo mchana kweupe!

Kwani wewe umejuaje kuwa aliyekuwa anaongelewa ni Lissu? Lakini kumbuka Lissu amekiri mwenyewe kuwa yeye ndiye alikuwa msaliti wa taifa
 
Huyu hapa mwingine kichwa maji....

Swali la kujibiwa ni hili moja tu na ndilo mnalopaswa kumjibu Tundu Lissu...

Hao mnaowaita "wasaliti wa nchi" ndiyo hukumu yao inakuwa hivi?

Ukijibu kuwa "ndiyo, hiyo ndiyo hukumu yao na Tundu Lissu alistahili", Mimi sitajibazana na wewe, nitakuacha kama ulivyo...!!

Lakini kama jibu ni HAPANA, siyo hivyo; basi Tundu Lissu aulizwe swali gani tena na wewe au Mimi??

Kwani ni msaliti gani umeona akitaka kuuwawa kamanda? Kwani kuna msaliti alitaka kuuwawa?
 
Jpm hana haki ya kumuita mtu yeyote kuwa ni msaliti wa taifa kwa sababu sheria zote za nchi zina simamiwa na mahakama so kama alimuita mtu yeyote kuwa ni msaliti alikuwa ana ikanyaga katiba ya nchi wenye haki ya kusema kuwa mtu fulani ni msaliti ni mahakama tena ni baada ya kufuatilia vifungu vya sheria ambavyo vinathibitisha kuwa kwa hiki alicho kifanya fulani sheria inamtaja kuwa ni msaliti

Kwani ni msaliti gani alikuwa anaongelewa pale? Wewe unamjua msaliti wa taifa?
 
Sijui ni kwanini watetezi hawa wa Rais Magufuli hawana uwezo wa kuelewa...

Ni wazi kabisa ndani ya mioyo yao wanajua kuwa Mzee wao huyo alichemka na anaendelea kuchemka siku hadi siku...

Sasa wameamua kuuvaa ujinga kutetea kila ujinga na upumbavu ili mradi wao wanalipwa....

Mkuu kwani ni sisi ndio tumemlazimisha Lissu kujiita msaliti wa taifa?
 
Lisu Ni msaliti baada ya serikali kuona mkataba una kasoro (Japo serikali ndio iliyoingia mkataba na kutaka kuuvunja) mabeberu walimpa fedha lisu na ndio akawa wakili wao na kuanza kututisha kuwa haturuhusi kuvunja mkataba na tukiuvunja tutashitakiwa MIGA na tutalipa milioni ya dollar Cha ajabu tulimpuuza na tukavunja mkataba tukawapa mkataba tunaotaka sisi(sio wa lisu na mabeberu) na tukalipwa sisi mamilioni ya dollar,lisu Ni msaliti na ni wakala wa mabeberu
Magufuli ni sehemu ya usaliti wakati mikataba ikipelekwa bungeni mwaka 1998 alikuwepo Bungeni hakusema chochote, lisu hakuwa wakili wao bali lisu alisimama kwenye ukweli baada ya kugundua kuwa magufuli kaingilia mikataba ili wazungu wampe Rushwa cha juu kabla ya kurekebisha mikataba ambayo ina mapungufu pia na bado kesi zinafukuta hazijaisha zitaibuka mda wowote kwani wazungu hawakulizika na kuwavurugia mikataba waliyopewa na mkapa kipindi hicho, wewe umemuua mkapa baada ya kulalamika ukaona anakupigia kelele.
 
Tundu lisu ndiye aliwaleta wachimbaji madini wa kizungu Tanzania? Uwekezaji wa mkapa na Lisu wapi na wapi? Aliyewaleta hao wazungu Nchini ndiye msaliti, Usikute wewe ndiyo umemuua mzee mkapa kwa kisingizio cha usaliti , kumbe tunahangaika kujua nini kilimuua mkapa? Kumbe wewe ndiyo ulimuua mkapa na upo unadunda

Mkuu ni Lissu mwenyewe ndio amekiri kusaliti taifa na kulihujumu
 
Kwani ni msaliti gani alikuwa anaongelewa pale? Wewe unamjua msaliti wa taifa?
Wazungu waliletwa na CCM kuja kuchimba madini mikataba mibovu ulitengenezwa na CCM kama ni usaliti ni CCM ndiyo wasaliti kwa kuwaleta hao wazungu Nchini
 
CCM ndiyo wasaliti kwani ndiyo waliwaleta wazungu Nchini mwaka 1998
 
..Jpm aliharibu zaidi baada ya tukio kutokea.

..SERIKALI ilipaswa kuchukua jukumu la kumtibu popote pale duniani.

..tungeweza kuomba hata kwa nchi WAHISANI zitusaidie ktk matibabu ya TL.

..badala ya kufanya hivyo Magufuli na Ndugai wakaendelea kumuadhibu TL kwa namna ambayo inaonyesha hawana UTU/UBINADAMU.
Aibu kubwa sana !
 
Kwa hiyo ni kweli magufuli ndo alipanga jaribio la mauaji ya Lissu??? Sema mwana CCM mwingine, sie tunakusanya ushahidi tu
kielelezo hiki hapa
 

Attachments

  • Subpost 2 - Connect dot's utaelewa tu... - NoHateNoFear - SasaBasi - TunduLissu2020 ( 264 X 48...mp4
    1.1 MB
Sasa kwanini akikuwa anasaliti nchi kwa kuwatetea?
Alisimama kwenye ukweli kuwa mbinu anazokwenda nazo zingeigharimu Taifa na ndipo magufuli akabadili mbinu akatumia njia zingine lakini nazo bado zina mapungufu makubwa ingawa watanzania wamefichwa vingi hakuna uwazi
 
Sasa kwanini akikuwa anasaliti nchi kwa kuwatetea?
Kwa iyo ni kweli kuwa Magufuli ndiye aliyeamuru Lissu kupigwa risasi????

Nafurahi sana wana CCM mnavyozidi kutupa ushahidi humu!!! Tunaweka rekodi sawa hapa!!
 
Back
Top Bottom